E-PLUS MEDIA
Ir al canal en Telegram
1 307
Suscriptores
+124 horas
-27 días
-1330 días
Archivo de publicaciones
1 307
"Furniture zangu za sebreni tu zina thamani ya milioni 20 za Kitanzania na huwa nabadilisha kila baada ya miezi mitatu, nazigawa nanunua mpya na nafanya hivyo kwasababu napenda sana furniture. Nina apartment yangu Masaki ambayo huwa silali naitumika kwa ajili ya kukodisha tu. Mimi hapa Tanzania naishi kwa bahati mbaya nina mpango wa kwenda kuishi Marekani siku za usoni"- amsema Diva ambaye kwasasa anaishi Palm Village ambako amepanga na anaishi na mume wake Sheikh Abdul.
1 307
Erik Ten Hag:
"Bado nina imani na hawa wachezaji, naamini tutaimarika baada ya mwanzo mgumu wa msimu".
1 307
🗣️ Zinedine Zidane:
“Nilipokuwa mchezaji, nilikuwa na uwezo wa kuchagua klabu yoyote ya kwenda, Lakini nikiwa Kama kocha, Kuna uwezekano nikachagua mbili au tatu.
" Kwenye kuchagua klabu ya kwenda, nazingatia sana kushinda makombe. Nasema hivi kwa unyenyekevu wote. Ndio maana siwezi kwenda popote.
“Sababu nyingine ninazozingatia ni lugha, hili tatizo la lugha linaweza kufanya mambo kuwa magumu"
"Mfano, Watu wanaponiambia: 'Je, unataka kwenda Manchester?' Ninakielewa Kiingereza lakini sikielewi vizuri.
“Najua kuna makocha wanaweza kwenda kwenye klabu tofauti tofauti bila kujali lugha, lakini kwa upande wangu huwa nafanya kazi tofauti.
Ili niende kwenye klabu, huwa natumia vipengele vingi sana vya maamuzi kwasababu najua ninachohitaji.”
1 307
#Repost @officialfelixtz
Wanaowania tuzo ya Golikipa Bora barani Afrika katika tuzo za CAF 2023
☑️ Djigui Diarra 🇲🇱
☑️ Mohamed El Shenawy 🇪🇬
☑️ Yassine Bounou 🇲🇦
☑️ Andre Onana 🇨🇲
☑️ Ronwen Williams 🇿🇦
☑️ Edouard Mendy 🇸🇳
☑️ Oussama Benbot 🇩🇿
☑️ Youssef El Motie 🇲🇦
☑️ Pape Mamadou SY 🇸🇳
☑️ Landing Badji 🇸🇳
#CAFAwards2023
1 307
Klabu zinawania tuzo ya Klabu Bora ya Mwaka katika tuzo za CAF 2023
☑️ Young Africans 🇹🇿
☑️ CR Belouizdad 🇩🇿
☑️ USM Alger 🇩🇿
☑️ Asec Mimosas 🇨🇮
☑️ Al Ahly Sc 🇪🇬
☑️ Raja CA 🇲🇦
☑️ Wydad AC 🇲🇦
☑️ Mamelodi 🇿🇦
☑️ Marumo Gallants 🇿🇦
☑️ Espérance Tunis 🇹🇳
#CAFAWARDS2023
1 307
Mabingwa wa Kanda ya CECAFA, JKT Queens wameondoka kuelekea Ivory Coast kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa wanawake yatakayofanyika Novemba 5-19, 2023. @cafwomenfootball @jktqueens2023
1 307
***Mbeya ukiagiza chips za Tshs 2000 kama watu wa dar wanavyoagiza basi watu wanakushangaa. Watakuuliza una tumbo kubwa kama pipa mpaka uagize chips zinazojaza ndoo?* kule agiza za Tshs 200 au za Tshs 500 utaletewa sinia zima au Ungo mzima umejaa utakula utashiba na zitabaki***
1 307
Tangazo la Tanesco, 1975
Tanesco ilikata umeme hazina, mahakama kuu, Bank Kuu, Ikulu, HQ yao wenyewe, Polisi HQ ili waunge umeme Ubalozi wa Zambia. Imekaaje hii?😂
1 307
1980-2000s, Wananchi wakipasua Bonde la Jangwani Magomeni - Dar es Salaam wakielekea kazini. Hili eneo sasa hivi lina kituo cha Mwendokasi.
1 307
Katibu Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Paul Makonda amewataka Viongozi mbalimbali wastaafu na ambao walikuwa na na nafasi fulani na kwa sasa hawana kukaa kimya na kuwaacha wenye nafasi kufanya kazi walizopewa.
Amesema hata yeye baada ya kumaliza muda wa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam alikaa kimya na sio kila siku kuongea au kutuma watu waongee kuhusu watu wengine.
Aidha, amewapa ujumbe kuwa kama wakihitajika wataitwa kama yeye alivyoitwa na kupewa nafasi hiyo baada ya kukaa kwa muda bila nafasi yoyote.
1 307
Lawrence Faucette, mtu wa pili aliye hai kupandikizwa moyo wa nguruwe uliobadilishwa vinasaba kwa ajili ya majaribio, amefariki dunia ikiwa ni wiki sita baada ya kufanyiwa upasuaji.
-
Taarifa zinasema moyo ulianza kuonyesha dalili za kutokufanya kazi katika siku za hivi karibuni.
-
Cc:
bbc swahili
1 307
Simba SC imetangaza kuingia mkataba wa udahmini na kinywaji Cha Plisner Lager kutokea kampuni ya Serengeti Breweries Limited Kwa muda wa miaka mitatu wenye thamani ya TSH Billion 1.5
1 307
𝗡𝗔𝗡𝗜 𝗔𝗧𝗔𝗜𝗖𝗛𝗨𝗞𝗨𝗔 𝗛𝗜𝗜 𝗠𝗪𝗔𝗞𝗔 𝗛𝗨𝗨
CAF Awards Imepangwa kufanyika
Disemba 11 nchini Morocco kwa upande wa
Mchezaji Bora wa Afrika nafasi unampa nani zaidi
Victor Osimhen
Kudus
Mo Salah
Riyad Mahraz
Sadio Manè
Yassine Bounou
Nani kati yao anastahili kura yako_
1 307
Ikitokea Msanii Mpya Wa WCB WASAFI Akaja Kuwa Mkubwa Kimuziki Kumzidi Vanilla, Ibraah, Macvoice Na K2ga Basi Nitaamini Tanzania Lebo Ni Moja Tu WCB WASAFI, Na Ni Mtihani Mwingine Kwa Lebo Za KINGS MUSIC, KONDE MUSIC, Na NEXT LEVEL MUSIC Kuonesha Ukomavu.
Zuchu Amekuwa Mkubwa Kuliko Wenzie Walio Tambulishwa Pamoja Kwenye Lebo Zao Huyu Nae Akikuwa Zaidi Ya Hawa Basi Ni Wazi Swala La Kusaini Wasanii Na Kuwafanya Wawe Wakubwa Kimuziki Na Wenye Thamani Tutawaachia WCB Peke Yao.
1 307
#NUKUU ''Kwa mujibu wa sheria ya ndoa hata wanandoa wakiachana, mwanaume ataendelea kumhudumia mkewe mpaka pale ndoa itakapovunjwa kisheria'' - Consolata Chikoti Mwanasheria kutoka Kituo cha Msaada wa sheria kwa Wanawake (WLAC).
1 307
FAHAMU KUHUSU CHUMA ULETE
Chuma Ulete ni hali ya kutumia pesa kidogo ili upate nyingi kwa njia ya mazingaombwe (kiini macho) bila kushitukiwa na uliyemfanyia kitendo hicho kwa macho ya kawaida.
Inasemekana kuna watu huwa wanatembea nazo wakienda dukani au sokoni kwa ajili ya mahitaji. Wanatumia hizo pesa kulipia ili ukiichukua ukichanganya na nyingine kwenye droo basi utaweza kuta zimepungua yaani zimehamia kwa aliyekupa kwa mazingara.
Pasipo we kutambua kama zimetoweka kwa staili hiyo lakini utazidi kufahamu kama utaendelea kupata udhoefu zaidi katika biashara yako.
Kuna baadhi ya wafanyabiashara hasa sokoni huwa wanakisia kuwa mtu flani anachuma ulete. Kutokana na mienendo yake yaani yule mtu ambaye hana kazi yoyote lakini anaishi vizuri zaidi ya mwenye kazi. Pia kutoa pesa anakupea mkono wa kushoto na ikiwa imechakaa vya kutosha.
Mara nyingi wazee wa kiume wamekuwa wakikumbwa na changamoto hii ya kuhisiwa kuwa wanamiliki chuma ulete. Kwani wanaweza kwenda kununua mahitaji dukani au sokoni wakanyimwa huduma ila akituma mjukuu anapatiwa huduma.
Je we unaamini kuhusu hizi imani za chuma ulete 🙄
