E-PLUS MEDIA
Ir al canal en Telegram
1 307
Suscriptores
+124 horas
-27 días
-1330 días
Archivo de publicaciones
1 307
"Nina Baba yangu asieshindwa kamwe. Asante kwa Uzima, Pumnzi, Afya na kibali🙏🙏🙏"- Grace Mapunda ameposti picha hiyo kisha kuambatanisha na maneno hayo.
Ikumbukwe siku za hivi karibuni Picha za Mwigizaji huyo Mkongwe wa Filamu zilisambaa mtandaoni zikimuonyesha akiwa amedhoofika, jambo ambalo lilizua maswali mengi na kuacha sintofahamu kwa mashabiki zake na wapenzi wa Tamthilia ya Huba.
1 307
FULL VIDEO NA MATUKIO MAZIMA UTAYAPATA KWA KU BONYEZA HAPA KWENYE INSTAGRAM LINK:-https://instagram.com/e_plus_media?utm_medium=copy_link
FACEBOOK PAGE FOLLOW:-https://www.facebook.com/eplusmediatv/
1 307
UMOJA wa Walimu Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania (TAHOSSA), wamechangishana kiasi cha shilingi milioni 1.6 kwaajili ya kumsaidia Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kuchukua fomu ya kugombea urais kwa mwaka 2025 ambao wameuita kama kapu la mama.
1 307
Ruby Alisema Kipindi Cha Mwanzo Laikua Hampendi Kabisa Kusah Ila Alipopelekwa Ukweni Tanga Tu Akashangaa Ameanza Kumpenda Kusah!! 😂😂😂
1 307
Utafiti binafsi nilioufanya hivi karibuni kuhusu TUZO zote Duniani.
Kwanza kabisa TUZO ni zawadi anayopewa Mtu (au kiume) baada ya kufanya kazi bora kwa muda fulani. Mtu huyo hupewa TUZO kufuatia kuwashinda wengine kwa kupigiwa kura na Wadau (au Jopo maalum au Majaji).
Nilichokigudua ni kuwa, wale Wasanii, Wachezaji, Wadau, huwa wanazilalamikia TUZO (Waandaaji) kwa sababu ya uelewa mdogo kuhusu TUZO. Kivipi, kawaida huwezi ukatoa malalamiko bila kujua unachokilalamikia ni kitu gani. Wao huwalalamika tu kwa utashi, ushabiki, mapenzi,... na kuacha utaratibu, sheria, kanuni na msingi ya TUZO zenyewe.
Ili lionekane kosa lazima kuwe na sheria, utaratibu, kanuni iliovunjwa. Swali ili ulalamike kanuni, Sheria na utaratibu vimevunjwa wapi, jiulize swali hilo kabla haujaanza kulalamika. Takribani TUZO zote Duniani zina utaratibu, Sheria, kanuni zake. Hawa Walalamikaji huwa hawaangalii sheria, utaratibu, kanuni,... na ndio maana nasema uelewa na elimu kuhusu TUZO ndio chanzo cha malalamiko hayo. Kivipi?
Baadhi ya TUZO au zote zina utaratibu wa kuchagua baadhi ya Watu (Wasanii, Wachezaji, Wadau,...) ili waingie kwenye kinyang'anyiro (TUZO) alafu wapigiwe kura na atayepata kura nyingi kuliko wote ndiye anatangazwa Mshindi. Baadhi ya hawa Walalamikaji hawataki kusikia kabisa huu utaratibu. Wao hujali kupata ushindi bila kupitia kwenye kanuni, Sheria na utaratibu.
Kitu kingine ambacho hawa Walalamikaji hawataki kusikia ni kwamba baadhi ya TUZO nyingi Duniani huwa zinachukua kazi BORA na sio kazi NZURI kwenye kinyang'anyiro. Kivipi?
Nimechunguza TUZO karibu zote huwa zinatumia neno la kiingereza (au lugha nyingine) BEST na sio NICE au BEAUTY 😂 yaani BEST=BORA/ NICE (BEAUTY)=NZURI. Hawa Walalamikaji huwa wengi wao huwa na kazi nzuri na bora na ndiyo maana kwenye TUZO wanashindwa. Kivipi?
Kuna utofauti mkubwa kati ya BORA na NZURI (Tembelea kamusi "Dictionary" ikusaidie haya maneno mawili). Kazi Bora au Mtu Bora ndiye anashinda na sio kazi nzuri au Mtu mzuri. UKITAKA kushinda TUZO, fanya kazi BORA kwanza kisha fuata maelekezo, utaratibu, kanuni na sheria.
1. Kazi Bora
2. Ingia kwenye TUZO
3. Hamasisha Watu wakupigie kura kwa mwingi
4. Subiri matokeo ya TUZO
5. TUZO ina matokeo mawili (Kushinda au kushindwa)
6. Unaweza kupata matokeo yote mawili kwahiyo usiwe Mtu wa kusubiri kushinda tu alafu ukatae kushindwa. "Asie kubali kushindwa sio Mshindani"
Baada ya kusema hayo, narudia tena Walalamikaji huwa hawafuati sheria, utaratibu na kanuni. Pia wengi wao hawajui kutofautisha kati ya BEST na NICE/BEAUTY.
NB : Najua swala la rushwa, ushkaji,... litazungumzwa kwenye comenti lakini swala hili ni ngumu kupata ushahidi wake kwa hiyo Mtu asikimbilie kwenye hiki kichaka kwa sababu utaonekana kama LOSER. Waswahili husema, "aliyeshindwa hakosi sababu"
Toa maoni yako
1 307
⚠️🥰 Shilole asherehekea kutimiza miaka 36 kwa kujizawadia mwenyewe gari jipya aina ya Toyota Land Cruiser Prado lenye thamani si chini ya shilingi milioni 70 ambazo amezilipa mwenyewe kwa awamu kwa wauzaji
Shilole anayejulikana kwa kuwa mwanamke mchapakazi, ni mama wa watoto wawili ambaye mbali na kuwa msanii pia ni mkulima na mfanyabiasha wa chakula anayemiliki mgahawa maarufu, Shilole anajwa pia kumiliki nyumba zaidi ya moja
Shilole ambaye pia ameolewa, mumewe ni Rommy ambaye ni mpiga picha
Picha nzuri za gari tuzisubiri .....
1 307
⚠️ Comrade Qayllah Nurdin Bilal ameshinda nafasi ya mwenyekiti wa chipukizi wa CCM taifa, ni baada ya kupata zaidi ya kura 300 kati ya kura 435 zilizopigwa na Wajumbe
Qaillah ni mtoto wa Shetta mwanamuziki wa kizazi kipya
1 307
⚠️😳 Amanda Poshy awabamiza wanaume, awakoromea na baadhi ya wanawake. Mwigizaji huyo Kibongo ambaye kwasasa anaishi nchini Uingereza na familia yake ameandika yafuatayo....
"Hakuna mwanamke mkaidi mbele ya mwanaume mwenye kumpenda na kumheshimu
Siku hizi naona imekuwa ni mchezo au imekuwa mazoea kwa baadhi ya wanaume wenye (akili ndogo)kuchepuka na kutoa kisingizio cha kwa kuwa wanawake wana midomo sababu za wao kuchepuka🙉yaani hii sababu kila page mpaka za wale washauri wa ndoa ambao ndio wanaoaminika nao wameipatia sehemu ya kukandamiza wanawake kwa hiyo style..
Wanaume kelele,viburi,ugomvi,chuki mnatengeneza wenyewe ndani za nyumba zenu kisha mnageuza ndio sababu za kuhalalisha umalaya. Hivi kwa akili yako mwanaume umetoka kufanya upuuzi na mwanamke anajua unataka akukaribishe kwa cake ya hongera?unategemea atakuchekea na kukukandakanda mwili kwa shuhuli uliyotoka kuifanya huko?
Amini nakuambia huyo atakuua mapema afadhari ya anayeongea angalau atakuvutia muda wa wewe kugundua unachofanya ni ukosefu wa akili na ukaamua kubadilika
Wanaume acheni kunyanyasa wanawake maana hata wao pia ni binaadamu furaha unayotaka wewe upewe hata yeye pia anaitaka na furaha unayoenda kuitafuta huko hata yeye pia ana uwezo wa kwenda kuitafuta ila tu anakuwekea heshima
Wanaume msiwageuze wanawake zenu kama wanyama na mnavyojitetea wanaume mmeumbwa na tamaa huo ni UONGO NA UASHERATI mmeuendekeza, binaadamu yoyote ana tamaa kikubwa ni kujizuia
Wanaume nawatahadharisha amini nawaambia msijione nyie ni wajanja HAKUNA narudia hakuna na hakutatokea kiumbe mbaya kama mwanamke chini ya jua hili bora ukutane na Simba kuliko mwanamke aliye/unayemjengea sumu ndani ya moyo kisasi chake mpaka shetani huwa anakaa kando anavuta sigara kujifunza jipya
Na wanawake manyanyaso muda mwingine mnayataka, unakaa tu uletewe kila kitu mpaka pesa ya Panadol hujishughulishi hapo kwanini usinyenyekee hata mtu anayetoka kulala na mwanamke mwengine??. .amka tafuta shughuli ya kufanya manyanyaso yatapungua kama siyo kuisha kabisa"
1 307
⚠️😳Mashabiki wamshangaa H.Baba kwa kuhangaika kila mwaka kumpost Irene Uwoya ambaye ni ex wake, wamlipua kwamba anataka watu wajue kuwa aliwahi kuwa mpenzi wa Irene Uwoya kwa kupenda kupost picha hiyo kila mwaka.....
"Happy birthday Irene Uwoya, Allah Akupe Maisha Marefu Yenye Baraka Tele ... Akupe Mwisho Mwema kwa Mema Yako Uliyotenda Duniani Nakwangu pia… Una roho Nzuri Saaààna Bac tuu sijui nilirogwa! tuendelee kutunza yai letu lisipasuke
"Happy birthday Kipenzi Irene Uwoya furaha yako furaha yangu nichukue fursa hii kukuomba msamaha kwa yale yoote yaliotokea japo ukomavu wa akili ulikuwa finyu utoto ulitutawala sasa tumekuwa nikuombe msamaha najua nilikukwaza" - H.Baba ameandika
H.Baba hakuishia hapo baada ya muda akarudi tena kumpost Irene Uwoya kwa kuandika..
"Happy birthday Irene Uwoya tulipotoka tunajua sisi tulivyopendana tulipendana sisi tulivyoachana tuliachana sisi, akaolewa, nikaowa ana mtoto, nina watoto ana maisha yake nina maisha yangu likija swala la kumkumbuka X wangu watu wa Insta msituingilie amjui nimekumbuka nini kwake au nimemic mautundu yake mnajuaje msitupangie nimempost X wangu kama umeumia njoo nikuumize wewe
ila Mama la mama Irene Uwoya ntakupenda daima tunza yai lisipasuke watu awakujui kama ninavyokujua mimi wanaongea nawachora tuu ila Dear X nimekumic sana nimemic cheko lako, tabasamu lako, ucheshi wako Una roho nzuri kuliko wanawake woote duniani tutaonana chimbo letu na zawadi yako Mama la mama Irene Uwoya ENJOY Siku yako ya kuzaliwa huna baya!!"
Irene Uwoya baada ya kumaliza kushiriki Miss Tanzania 2006 haikuchukua miezi mingi akawa mpenzi wa H.Baba ambaye kipindi hicho ndie alikuwa maarufu kuliko Uwoya wa sasa. Hawakukaa sana waliachana Uwoya akapata umaarufu zaidi kupitia filamu na maisha binafsi
Baada ya kuachana H.Baba aliwahi kumtamkia Irene Uwoya maneno ya kashfa yasiyofaa kwenye magazeti ya udaku, pia miaka michache iliyopita H.Baba aliyarudia kuyaandika maneno husika mtandaoni ingawa Uwoya mara nyingi amekuwa hamjibu H.Baba
1 307
⚠️😳 Edo Kumwembe mwanahabari wa mambo ya michezo amepost picha hiyo ya Ronaldo kisha kuandika yafuatayo...
"Mpaka leo kuna watu wanaamini kwamba ukila ugali unakuwa na nguvu sana....eti unakuwa mgumu...eti Waafrika ni wagumu kwa sababu ya ugali.....nilishtuka zamani wakati Rooney akiwazidi ubavu akina Kolo Toure.....lisheni watoto vitu bora sio dude zito linaloenda kukaa tumboni.....msosi wa mwamba huo hapo (Cristiano Ronaldo)... Je alikuwa laini uwanjani?....(Sema Janabi naye kazidi) 😀😀
1 307
⚠️😳 "Wanawake mlioolewa mnisikilize kwa makini, hii sio miaka ya mume wako akikugusa unamwambia niachie, kwasababu kitu unachomkatalia wewe anaweza kukipata bure Tiktok, Instagram na Facebook
Zamani ilikuwa ili mwanaume apate mwanamke kahaba inabidi aende pale Sinza wanapojipanga na maeneo mengine wanapojipanga makahaba"
"Siku hizi hakuna haja ya kwenda huko wameweka namba zao kwenye mitandao, wameweka namba zao Instagram wana page zao wanaonyesha mapicha yao, kwahiyo mwanaume anakuwa najua kabisa mali anayoitaka anachagua ananyanyua tu simu anapiga
Hii sio miaka ya kumnyanyasa mwanaume kwamba haumpi tendo la ndoa, kwasababu ukimuwekea ugumu ndani ya nyumba unampa urahisi wa kwenda kuchepuka nje" - Amesema Mchungaji Rose Shaboka
1 307
Prof. Janabi ana wafanyakazi zaidi ya 3500 (Upanga na Mloganzila)
Jana amewapa kila mmoja zawadi ya sikukuu ya Krismasi
1. Sukari kilo tatu
2. Mafuta ya kupikia lita moja
3. Miche miwili ya sabuni
Boss wako amekupa nini kazini?
1 307
HAWA HAPA WASANII WALIOIBUKA NA KUPATA UMAARUFU 2023.
Kumekuwa na utaratibu kila mwaka wanaibuka wasanii au watu maarufu wapya ambao wengine huwa mastaa wakubwa lakini wengine hupata umaarufu wa muda mfupi kisha wanatokomea kusikojulikana. Mwaka huu wameibuka watu maarufu kadhaa ambao baadhi yao wanafanya vizuri kwa sasa, na baadhi yao ni hawa hapa
1. Obby Alpha; Huyu amekuwa miongoni mwa watu waliopata Baraka/kibali cha kutambulika mwaka huu na anaendelea kufanya vizuri mpaka sasa. Wimbo wake wa (Bora kushuku) umempa heshima kubwa na umemfuta jasho baada ya kusota kwa muda mrefu ambapo alikuwa anatoa nyimbo za Injili lakini zilikuwa hazifiki popote, Obby Alpha ni moja ya mtu anayethibitisha kwamba wakati wa Mungu ni wakati sahihi.
2. Appy; Huenda wakati anarekodi wimbo wake wa (Watu feki) hakujua kama ungekuwa ndio wimbo unaoenda kubadilisha maisha yake, baada ya wimbo huo kutoka umefanikiwa kupendwa na mamilioni ya watu, umeweka rekodi kadhaa kwenye platforms za muziki lakini pia umempa heshima na kufanya watu waliokuwa wanamuona wa kawaida wamzingatie.
3. Zuwena; Huyu ni moja ya watu maarufu ambao umaarufu wao ulikuja baada ya kuhusika kama video vixen kwenye wimbo wa Diamond Platnumz (Zuwena) ambapo wimbo huo ulipendwa sana na miongoni mwa wahusika waliochochea wimbo huo upendwe zaidi ni Zuwena mwenyewe kutokana na miondoko na manjonjo yake kwenye video hiyo. Kabla ya kuonekana kwa Diamond Platnumz, Zuwena alishaonekana kwenye video kadhaa ikiwemo kwenye video ya Martha Mwaipaja (Sitaki kujibu) lakini wakati wake ulikuwa bado haujafika.
4. Kiredio; Ukizungumzia watu waliopata umaarufu mwaka huu kupitia mtandao wa Tiktok, huwezi kuacha kumtaja Kiredio, aina yake ya kipekee ya uburudishaji imemfanya ajizolee umaarufu kutoka kwa wanachuo lakini pia watu baki wa mtaani. Ni ngumu kuendelea kumdadavua kwasababu hana muda mrefu kwenye game, tumuache tuone juhudi zake mwakani (2024) lakini binafsi namuona mbali sana endapo ataendelea na ubunifu wake huu.
5. D Voice; Awali alikuwa na jina mtaani, lakini alikuwa anatambulika mtaani kwao na sehemu kudogo ya jiji la Dar es salaam, kutokana na upekee wake kwenye muziki wa Singeri, Diamond Platnumz alivutiwa nae akampandisha thamani akamtambulisha duniani na sasa D Voice amekuwa ni miongoni mwa wasanii wenye majina makubwa lakini wanaofatiliwa sana, kama alivyotenda wema kwa Zuwena, Diamond Platnumz ametenda pia wema kwa D Voice.
Wako wengi na unaweza pia ukaongezea idadi hapo chini kwenye komenti
