1 307
订阅者
+124 小时
-27 天
-1330 天
帖子存档
1 307
CHRISTINA SHUSHO ATAWALA KWENYE VINJWA VYA WAKENYA, WAMPA JINA LA (WOMAN OF GOD)
Kama ulitarajia kusubiri anguko la Mwimbaji wa nyimbo za Injili nchini Christina Shusho basi utangoja sana, na ikiwezekana utaanguka kwanza wewe kisha yeye atakuja kukunyanyua. Hii imekuja baada ya Mwanamama huyo kuendelea kufanya vizuri kila kukicha na awamu hii anaenda kimataifa zaidi, kama mtakumbuka pia ni kama wiki mbili tu zimepita alikuwa na ziara nchini Marekani, sio jambo rahisi kwa mwimbaji wa nyimbo za Injili.
Siku za hivi karibuni, Shusho amekuwa akiongelewa sana na vyombo vya habari nchini Kenya, ametapakaa kila mahari na wamekuwa wakimsifia kuwa nyimbo zake zimekuwa faraja kwa mamilioni ya watu na zinadumu kwasababu mara nyingi anatoa maneno ya kwenda biblia anayageuza kuwa wimbo.
Wakenya hao hao wamesema Christina Shusho ni (Woman of GOD) na hakuna wa kumfikia wala kulipinga hilo, na kwa kuonyesha wanamjali zaidi wamemuita kwenye usiku wa Overnight tarehe 31 December 2023 kwenda kuwaburudisha.
Hata hivyo tangu alipoanza muziki wa Injili, Shusho amekuwa akifanya matamasha mengi zaidi nchini Kenya kuliko Tanzania, lakini awamu hii hamasa na hamu ya Wakenya kumuona Shusho imekuwa mara dufu zaidi.
1 307
⚠️ Mange amepost picha za Rushayna akionekana amepigwa usoni na Manara kipindi walipokuwa mke na mume kisha kusema yafuatayo....
"Haji Manara wewe ni abuser wa wanawake. Hizi picha niliposti kwa app kipindi mnaachana na Rushaynah
Ungekuwa nchi zetu hizi ungekuwa jela na ungekuwa cancelled, hakuna kampuni ingekupa huo usemaji, hakuna redio zingekuita kukupa kiki. Na huyu sio mke wa kwanza uliekuwa unambutua, nilishaposti picha pia za mke wako wa nyuma uliekuwa unambutua hivi. ulimpiga Rushy mpaka akakimbia hotelini huko Dubai
Na hizo redio za Tz jamani mwanaume anasema kabisa hadharani alioa mtu hampendi ili amkomeshe mke wake alafu wanamchekea hawaoni ni unyanyasaji wa kijinsia
Kweli mtu mzima unafanya harusi kabisa ili umkomeshe mke? Basi Rushy hakuwahi kuwa na kosa kwa kiburi alichokufanyia maana hukuwahi kumpenda.Ulikuwa unamtreat vibaya, mtoto wa watu alilazwa wiki nzima hujatokea hospitali ukatumia muda huo kuingiza machangu home,Rushy anakuuliza hapo kwenye chat utetezi wako ni kwamba ooh siwezi kuja coz unatumia bima ya mtu mwingine na jina feki.
Kwanza unatakiwa kufunguliwa mashtaka ya fraud ya Bima. . . Jamani msione naongea sana, undugu na huyu mtu umeisha.
Sasa tuko vitani baada ya kumposti na wale machangu juzi kanitumia vitisho DM eti yeye, na kina Giggy wamejiunga wanakuja Marekani kunifungulia kesi. . Pumbav zenu njoooni, tutapelekeshana vizuri tu na mtaishia kunilipa mimi lawyer fees. Msinitishie maisha.Njooni nimejipanga. . . Eti linanitishia llinasema unaonea wabongo sababu hawajui haki zao mbona Wamarekani huwaposti unaogopa
Mtz star alieko Marekani ni Roma tu, mwambie achafue hali ya hewa kama sitoposti.Au unataka niwaposti wabeba boxi ambao hakuna mtu anawajua? . . Kwenda kina Wendy Williams wamechachafya mastaaa wa Marekani miaka na miaka kwa kutoa umbea wao na mpaka kastaafu kwa raha zake ndo nyie vishanshuda mnitishie mimi?
Mimi naandika habari za ukweli, huku kuna gazeti la national enquirer hawa wanaandika story za uwongo za mastaaa wa Marekani mpaka mimi mwenyewe naachaga mdomo wazi na hakuna alieweza kuwashinda kesi ndo mnitishie mimi naeandika habari za kweli?
Mje nakwambia tupelekeshane . . Haji Manara na ukome kunitishia maisha embu kanyonye huko. Eti ooh tutamlipia mpaka Zari na viongozi woote uliowatukana, yani limeongea shit Dm hili baba." - ameandika Mange
1 307
⚠️😭 Bibi harusi na mama yake wafariki dunia kwa ajali wakati wakielekea Marangu, Moshi
Watu wa tatu wamefariki dunia akiwemo Rehema Dias Chao (37) anayetajwa kuwa ndiye alikua akiendesha moja ya magari yaliyohusika katika ajali hiyo akielekea nyumbani kwao Marangu kwa ajili ya maandalizi ya Harusi yake.
Taarifa ya jeshi la Polisi imesema tukio Hilo limetokea Novemba 28, 2023 saa 7:00 mchana katika barabara kuu ya Moshi - Mwanga eneo la Kichwa cha Ng’ombe, Wilaya ya Mwanga mkoa wa Kilimanjaro,
ambapo gari lenye namba za usajili T.770 AHV aina ya Scania Lori lenye tela namba T.705 AHV mali ya AVCO Investment Ltd ya mkoani Arusha, likitokea Arusha kuelekea Dar es Salaam, liligongana na gari ndogo lenye namba za usajili T.121 CYM aina ya Toyota Raum .
Rehema Dias Chao, (37), mwalimu wa Shule ya Sekondari SUA na mkazi wa Morogoro, aliyekua akitokea Morogoro kuelekea Marangu, Moshi anatajwa kufariki dunia pamoja na abiria waliokuwa kwenye gari hilo Agnes Dias (75), mkazi wa Marangu, Moshi na Arine Shija (15), mkazi wa Geita.
Katika ajali hiyo watu wawili ambao ni Veronica Dias Chao, (35), mkazi wa Geita na Jayden Erasto (2) mkazi wa Morogoro wanejeruhiwa vibaya. Chanzo cha ajali hiyo bado kinachunguzwa na kwamba Jeshi la Polisi linamshikilia dereva wa gari T.770 AHV Scania kwa mahojiano zaidi.
Miili ya marehemu imehifadhiwa katika kituo cha afya Kisangara, Mwanga.
Credit Dixon usagaga, Clouds habari
1 307
⚠️😳 "Kwasasa siwezi kuongea chochote kama mimi na Zaiylissa ni wapenzi au laah! muda ukifika sheria za kiislamu zikifuatwa mtajua ukweli maana mimi huwa sifichi. Lakini niseme tu Zainabu ni mrembo hakuna mwanaume shababi ambaye anaweza kumuacha" - Manara ameiambia Wasafi Media
"Kwanza ni mwanamke mrembo, mrefu na ana shepu, ni wanawake wachache sana ambao unakuta ni warefu na wana shepu, wengi wao hawaeleweki. Lakini pia ni mweupe na mimi nazingatia sana rangi, ukiwa na rangi isiyoeleweka hata mimi sikuelewi kwasababu nina rangi zangu" - Haji Manara
Manara anaelezwa alishaona mara 6 na ndoa zake zote kuvunjika kiasi kwamba katika ndoa ya Rushayna, alisikika Mama Manara akisema ameichoka tabia ya mwanae huyo kuoaoa kila wakati
1 307
⚠️ Zuchu atundika mvuto wake mpya kwenye urembo wa matairi mapana na vipini vya mapazia mikononi
Tazama nakshi za meno yake na miwani yake kwenye comments section
1 307
Mkurugenzi mtendaji wa Google ni Mhindi 🇮🇳
2. Mkurugenzi mtendaji wa Microsoft ni Mhindi 🇮🇳
3. Mkurugenzi mtendaji wa YouTube ni Mhindi 🇮🇳
4. Mkurugenzi mtendaji wa Adobe ni Mhindi 🇮🇳
5. Mkurugenzi mtendaji wa World Bank Group ni Mhindi 🇮🇳
6. Mkurugenzi mtendaji wa IBM ni Mhindi 🇮🇳
7. Mkurugenzi mtendaji wa Albertsons ni Mhindi 🇮🇳
8. Mkurugenzi mtendaji wa NetApp ni Mhindi 🇮🇳
9. Mkurugenzi mtendaji wa Palo Alto Networks ni Mhindi 🇮🇳
10. Mkurugenzi mtendaji wa Arista Networks ni Mhindi 🇮🇳
11. Mkurugenzi mtendaji wa Novartis ni Mhindi 🇮🇳
12. Mkurugenzi mtendaji wa Starbucks ni Mhindi 🇮🇳
13. Mkurugenzi mtendaji wa Micron Technology ni Mhindi 🇮🇳
14. Mkurugenzi mtendaji wa Honeywell ni Mhindi 🇮🇳
15. Mkurugenzi mtendaji wa Flex ni Mhindi 🇮🇳
16. Mkurugenzi mtendaji wa Wayfair ni Mhindi 🇮🇳
17. Mkurugenzi mtendaji wa Chanel ni Mhindi 🇮🇳
18. Mkurugenzi mtendaji wa OnlyFans ni Mhindi 🇮🇳
19. Mkurugenzi mtendaji wa Motorola Mobility ni Mhindi 🇮🇳
20. Mkurugenzi mtendaji wa Cognizant ni Mhindi 🇮🇳
21. Mkurugenzi mtendaji wa Vimeo ni Mhindi 🇮🇳
Hawa wahindi wana nini ?
1 307
***Juu ni Van damme na Dolph Lundgren Enzi zao* Chini ni Ida Lundgren , binti wa Dolph Lundgren na Bianca Van Damme, Binti wa Jean Claude Van Damme🥊🥋***
1 307
ASKARI TAWA KIZIMBANI KWA MAUAJI
Mahakama Kuu kanda ya Tabora imeanza kusikiliza shauri la jinai namba 111 la mwaka 2023 linalowakabili askari sita wa Mamlaka ya Uhifadhi Wanyamapori (TAWA) wilaya ya Mlele, Katavi.
Askari hao wanakabiliwa na mashtaka ya mauaji ya watu sita wakati wakiwa katika doria ndani ya hifadhi ya Ugala wilayani Sikonge, Tabora.
Mahakama hiyo hii leo Novemba 29 imesikiliza ushahidi wa shahidi wa kwanza, ASP Kisu Mwapongo ambaye ni mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai wilayani Sikonge kati ya mashahidi 26 wa kesi hiyo.
1 307
Of course tumezoea kuwaona Wasanii katika viwanja mbalimbali vya bata waki-pop up champagne🥂, nyama choma au wakipata moja baridi moja moto na yote ni katika kuhakikisha wanatumia 'good time' zao kufurahia maisha, hali hiyo ni tofauti kidogo kwa msanii @Alikiba.
Kupitia Insta Live aliyofanya siku ya jana wakati akisherehekea kuongeza mwaka mwingine, #Alikiba ali-share na mashabiki zake mtindo wake wa kila siku wa maisha uliowashangaza wengi.
Kupitia Live hiyo Kiba anasema, kikawaida yeye hula milo miwili tu kwa siku, mmoja baada ya kuamka na mwingine baada ya kutoka mazoezini (Gym). Lakini pia hatumii nyama nyekundu wala vile vinywaji vingine (Pombe), ambavyo hakuvitaja direct kwa sababu ya kuepuka kuviharibia biashara zao.
Kauli ambayo ilipokewa kwa mshangao mkubwa na mashabiki zake.
Tujuze kwenye comment ni mtindo gani wa maisha wa kitofauti ambao unao wewe na ungetamani kufunguka?
1 307
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limesema limepokea taarifa kuwa November 29,2023, saa sita usiku maeneo ya Sinza Mapambano Kinondoni Askari wawili walimjeruhi kwa risasi Mtu mmoja aliyefahamika kwa Jina la Razaki Azan mwenye umri miaka 29 Mlinzi binafsi wa Bar iitwayo Board room iliyopo Sinza Dar es salaam ambaye baaade alipoteza maisha.
Jeshi la Polisi limesema tayari limewakamata Askari hao na mambo ya kisheria yanakamilishwa na watachukuliwa hatua za kisheria haraka kadri iwezekanavyo kwa kufuata mifumo ya kisheria ikiwa ni pamoja na kuwafikisha Mahakamani.
“Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa Mwananyamala kukamilisha uchunguzi”
#MillardAyoUPDATES
1 307
AJALI MANYONI YAUA WATU 13 YAJERUHI 25
Watu 13 wameripotiwa kufariki Dunia, huku wengine 25 wakijeruhiwa katika ajali ya basi iliyohusisha basi la abiria la kampuni ya Allys Star lenye namba za usajili T 178 DVD, baada ya basi hilo kugonga kichwa cha treni, katika eneo Manyoni, mkoani Singida.
1 307
HUYU HAPA MISS UNIVERSE 2023
Anaitwa Sheynnis Palacious, ana umri wa miaka 23 ni Raia wa Nicaragua 🇳🇮 na huyu ndiye mrembo aliyefanikiwa kutwaa taji la Miss Nicaragua 2023 lakini pia taji la Miss Universe 2023.
Hakika ni mrembo sana na kingine kilichonivutia sana ni jinsi alivyoupokea ushindi wake, alionyesha kweli alikuwa ana uhitaji wa kutwaa taji hilo.
1 307
FULL VIDEO NA MATUKIO MAZIMA UTAYAPATA KWA KU BONYEZA HAPA KWENYE INSTAGRAM LINK:-https://instagram.com/e_plus_media?utm_medium=copy_link
FACEBOOK PAGE FOLLOW:-https://www.facebook.com/eplusmediatv/
1 307
Ameandika Lukamba baada ya Clam Vevo na Kicheche kukamatwa..
"😄 MNAYAPI YAKUONGEA NDUGU ZANGU CONTENT CREATOR … SAMAANI LAKINI ME NAFKIR BODI YA FILAMU ILITAKIWA KUWA INATOA ELIMU MAPEMA SANA KAMA KUNA SHERIA MPYA IWE INAPEWA PROMO WATU WAJUE .. ME NI MMOJA NAFATILIA SANA KAZI ZA HAWA VIJANA SIONI KIBAYA AMBACHO WANAKIFANYA KINAWEZA POTEZA JAMIII WANAANGAIKA SANA HAWA WATU MPAKA NYIE MMEFIKIA KUWAONA NA KUWAKAMATA TRUST ME WAMEUMIA SANA .. KUNAWATU WANAISHI NÓW KWA AJILI YA HAWA VIJANA ..
YOUTUBE ILI UPATE PESA UNATAKIWA KUWA ACTIVE SANA SIO KITOTO MPAKA MWANZE KULETEWA MKAGUE KAMA UNAVYO JUA POZI ZILIVYO 🤲🏻😊YAANI KIFUPI NI KUFELISHA SANAAA YA UIGIZAJI
WASANII TU HATA LOCATION TU IMEKUWA TABU UKITAKA POLISI SHIDA YAANI KIFUPI SHIDA MPAKA HAWA MADOGO WANAAMUA KUIGIZIA ZAO VIJIJINI
WALIPO FIKA NA WAFUASI WALIO PATA MNATAKIWA KUWASHIKA MIKONO KAMA WALIWEZA KUJA INAMAA KUNA KIBUNDA HUENDA KILITAJWA.. HAWANA HELA NI AMSHA AMSHA ZA MITANDAO TU
BONGO MOVIE MPAKA LEO HATA SOKO LA FILAMU TU SHIDA UTAUZA WAPI NJIA RAHISI WANAONA YOUTUBE
TUPENI ELIMU WEKENI SEMINA TANGAZENI WATU WAJUE HAKUNA ASIE TAKA KUTIII SHERIA
KAMA MNAWEZA PELEKA WATU MAHAKAMANI KUPOTEZA MUDA WHY MSIWEKE NGUVU KWENYE KUWAPA ELIMU HAWA CONTENT CREATOR MAANA NI WENGI SANA
SAMAANI WAKUU 🙏 " - Lukamba, Msanii wa muziki na filamu Tanzania.
Clam Vevo na Kicheche wamekamatwa na Polisi kupitia Bodi ya Filamu Tanzania baada ya kukiuka sheria ya filamu Tanzania kwa kutozipeleka filamu zao katika Bodi hiyo ili zikaguliwe kabla ya kurushwa kwenye mtandao wa YouTube.
Toa maoni yako
