ch
Feedback

不要被骗子欺骗!Telemetrio 会找到并标记这些频道 👉 如果想查看标记,请订阅

E-PLUS MEDIA

E-PLUS MEDIA

前往频道在 Telegram

Get the latest news,videos,and more everyday.

显示更多
1 307
订阅者
+124 小时
-27 天
-1330 天
帖子存档
"Mama yangu anasema ananiona mimi kama bado nina Umri wa miaka 13 tu kwa sababu licha ya changamoto zote nilizopitia, misuli
"Mama yangu anasema ananiona mimi kama bado nina Umri wa miaka 13 tu kwa sababu licha ya changamoto zote nilizopitia, misuli iliyokasirika na mishipa iliyovunjika lakini bado ninafanya kazi" amesema Mama Mzazi wa Mwigizaji maarufu Nchini India Salman Khan. Toa maoni yako

SERIKALI IMESEMA HAKUNA UHABA WA SUKARI NCHINI. Serikali imesema hakuna uhaba wa Sukari nchini na kwamba upungufu uliopo hivi Sasa kwa mikoa ya kaskazini unatokana kiwanda cha TPC cha Moshi mkoani Kiilimanjaro kupunguza uzalishaji na Manyara Sugar cha mkoani Manyara kusitisha uzalishaji kutokanana ukosefu wa mali ghafi. Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Ashatu Kijaji wakati akiwa kwenye ziara ya kutembelea kiwanda cha Sukari cha Manyara Sugar kilichopo kijiji cha Matufa Wilayani Babati ambacho kimesitisha uzalishaji kutokanana ukosefu wa mali ghafi. Kauli hiyo ya Waziri Kijaji inakuja wakati huu ambapo Sukari imeadimika mitaani ambapo kilo moja ya Sukari iliyokuwa inauzwa shilingi 3,200 kwa rejareja katika miji ya Babati na Karatu Sasa inauzwa kati ya shilingi 3,800 hadi 4000, hali ambayo Wananchi wanaomba Serikali ifuatilie na kutafuta ufumbuzi. Afisa uhusiano Kiwanda cha Manyara Sugar John Jeu amesema wamesitisha uzalishaji kwa sababu ya ukosefu wa malighafi za kutengenezea sukari. Amesema kwa sasa serikali inaangalia utaratibu wa kusambaza sukari kutoka mikoa ambayo kuna hodhi kubwa kwenda mikoa yenye upungufu ili kukabiliana na ongezeko la bei ya bidhaa hiyo, huku akitoa wito kuwataka wakulima kuchangamkia fursa ya kilimo cha miwa ili kuondoa changamoto ya ukosefu wa Sukari nchini. Amesema kwa sasa serikali inaangalia utaratibu wa kusambaza sukari kutoka mikoa ambayo kuna hodhi kubwa kwenda mikoa yenye upungufu ili kukabiliana na ongezeko la bei ya bidhaa hiyo Kwa sasa Viongozi ngazi zote kuhamasisha kilimo cha miwa ili kuondoa changamoto ya ukosefu wa sukari na bei kupanda. Hata hivyo ameshauri uwepo wa mpango wa muda mrefu ukiwemo uchimbaji wa mabwawa makubwa yatakayosaidia kuhifadhi maji kwa ajili ya umwagiliaji ili kuwaondolea wakulima wa miwa utegemezi wa msimu wa mvua pekee. Amesema serikali imeandaa Mpango wa visima Zaidi ya 680 ambapo 150 vitachimbwa katika Wilaya ya Babati na ameelekeza 30 vichimwa katika mashamba ya miwa ya Magugu. Mfafanyabiashara Peter Mallya wa Mjini Babati amesema kwa sasa wanapata sukari kwa tabu kutokana na kiwanda cha TPC alikokuwa anachukulia kupunguza Uzalishaji. @viwandabiashara

photo content

⚠️ Steve Nyerere na watoto wake
⚠️ Steve Nyerere na watoto wake

⚠️ Nandy na mwanae kwa Mwamposa
⚠️ Nandy na mwanae kwa Mwamposa

Ni Birthday ya Naveen mtoto wa kwanza wa Rose Ndauka
Ni Birthday ya Naveen mtoto wa kwanza wa Rose Ndauka

MANGE KIMAMBI AKATAA KUSAMBAZA PICHA ZA UTUPU ZA MTOTO WA HAJJI MANARA. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mange Kimambi amep
MANGE KIMAMBI AKATAA KUSAMBAZA PICHA ZA UTUPU ZA MTOTO WA HAJJI MANARA. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mange Kimambi ameposti picha ambazo zinamuonyesha mtoto wa kike wa Hajji Manara (Hameeda) akiwa mtupu huku akiziba sehemu zake nyeti kisha kumtaka Hajji Manara akae vizuri na mwanae muda anaopoteza kuhangaika na Zaiylisa angeutumia kumpa malezi mazuri mwanae. Mange amesema kuna mtu alimtumia picha hizo za utupu ili azisambaze, lakini kwa busara aliyonayo akaamua kuzinunua na kumpa onyo mtu aliyemtumia azifute asizisambaze kwenye magroup ya WhatsApp. Mange amesema kamwe hawezi kuwadhalilisha watoto kisa tu ana ugomvi na wazazi wao. Pia amewataka mabinti wa siku hizi wapunguze tamaa, kwasababu itawapeleka pabaya watashindwa kutimiza ndoto na malengo yao.

😂😂 Kuzeeka ni kuchagua mwenyewe .... CR7 vs ROONEY Wewe unazani kitu gani kimefanya Rooney kuzeeka mapema wakati huo CR7 ba
😂😂 Kuzeeka ni kuchagua mwenyewe .... CR7 vs ROONEY Wewe unazani kitu gani kimefanya Rooney kuzeeka mapema wakati huo CR7 bado ni bwana mdogo tu wakati miaka wako sawa

#HABARI Mwandishi wa habari wa Gazeti la Uhuru na Katibu Msaidizi wa chama cha waandishi wa habari mkoani Mwanza (MPC) Blandi
#HABARI Mwandishi wa habari wa Gazeti la Uhuru na Katibu Msaidizi wa chama cha waandishi wa habari mkoani Mwanza (MPC) Blandina Aristides (34), aliyefariki wakati akijifungua Jijini Mwanza anatarajiwa kuzikwa leo ambapo taratibu za kuaga mwili zinaendelea katika viwanja vya kambi ya polisi Mabatini. Blandina alifariki alfajiri ya Desemba 26, 2023, yeye pamoja na mtoto wake katika hospitali ya Rufaa ya kanda Bugando baada ya kufanyiwa oparesheni wakati wa kujifungua. Miongoni mwa walioshiriki zoezi la kuaga mwili huo ni Kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Mwanza Wilbroad Mutafungwa. #RIPBlandina

Inafikirisha kumbe tulikuwa na mamba mrefu zaidi duniani na hatujui ? Kama tulikuwa tunajua mbona hatukutangaza mapema kuhusu mamba huyu ili kuitangaza nchi ? Au kama tulikuwa tunajua mbona tukaruhusu awindwe like seriously ? Kama hatukuruhusu kwahiyo muwindaji katupiga je kwa kushirikiana na WAKINA nani ? Kama muwindaji katupiga je ni hatua gani za kisheria za kuchukulia? Kama muwindaji kawinda kwa sheria za nchi je nchi imefaidikaje ? Je ukipma faida ambazo nchi ingepata ni bora alivyowindwa au angeachwa kwa utalii ?

KUTOKA MITANDAONI Kwa habari zaidi SUBSCRIBE kupitia YOUTUBE channel yetu kwa ku bonyeza hapa chini.👇.kwenye link https://yo
+8
KUTOKA MITANDAONI Kwa habari zaidi SUBSCRIBE kupitia YOUTUBE channel yetu kwa ku bonyeza hapa chini.👇.kwenye link https://youtube.com/@E-PlusMediaTv?si=JjehK80_nkzrHGNK

#HABARI: Wanandoa waliojulikana kwa majina ya John Hennessee, mwenye umri wa miaka 76 na mkewe Melody Hennessee, mwenye umri wa miaka 64, wameamua kutumia muda wa maisha yao yote wakisafiri katika sehemu mbalimbali ulimwenguni kwa kutumia usafiri wa meli, ambapo walibainisha kuwa miaka mitatu iliyopita waliamua kuuza kila kitu walichokuwa nacho, ikiwemo biashara na makazi yao, kisha kununua gari maalumu lenye makazi ndani yake, ili waweze kusafiri wakizunguka sehemu mbalimbali za nchi ya Marekani. . Wanandoa hao wenye asili ya Florida nchini Marekani, wamesema baada ya kuzunguka kwa muda mrefu na gari walichoka kuendesha gari hilo ndipo walipoona tangazo kupitia mtandao wa facebook la safari ya siku 274, la kampuni ya meli ya Royal Caribbean, ndipo safari yao ya kudumu baharini ilipoanza. . Wawili hao ambao hadi sasa wametembelea sehemu mbalimbali ikiwemo Australia, New Zealand, Canada, Misri na Pasifiki ya Kusini, wamesema maisha ya ndani ya meli ni rahisi wakilinganisha na ya ardhini na kwamba hivi karibuni watachukua makazi ya kudumu kwenye meli ya kitalii ya Villa Vie ambayo 30% ya wasafiri wake watakuwa ni wakazi wa kudumu. . Wanandoa hao wamesema maisha hayo ni rahisi kwa sababu hayana gharama nyingi kama Bima ya gari, ankara za nyumba na bima za mali, na kwamba gharama za melini hajazijafikia hata nusu ya maisha ya ardhini.

photo content

⚠️👏 By Jimmy Mafufu - "Sina Vingi Wala Sina Kipato Kikubwa Kama Wasanii Wengine Lakini Kile Kidogo Mnachonichangia Katika Filamu Zangu Nami Nimefanikisha Ujenzi Wa Fensi Ya Shule Ya Msingi Sinde Mahali Ambapo Nilipata Elimu Yangu Ya Msingi Niliguswa Baada Ya Kusoma Gazeti Kwamba Kuna Watoto Wawili Walitoroka Shule Kisha Wakakutwa Wamefariki Vichakani, Niliumia Sana, Ndipo Nikawapigia Cm Waalimu Kwenye Shule Hiyo Ambayo Nilimaliza Darasa La Saba Mwaka 2000 Naweza Kuwa Sijafanya Jambo Kubwa Kwa Sababu Ya Uwezo Wangu Wa Kiuchumi Lakini Hata Hapa Ashukuriwe Mungu Aliyenifanikisha Katika Ujenzi Huu Ndugu Zangu Endeleeni Kunisapot Pengine Wakati Ujao Naweza Kufanya Zaidi Ya Hapo, Mungu Awabariki Sana Wote Mlionitia Moyo Katika Jambo Hili, Nikijaaliwa Natamani Kujenga Vyoo Vya Kisasa Shuleni Hapo Na Ofisi Za Waalimu Mwisho Nenda Kwa Bio Yangu Hapo Juu(Instagram) gusa Link Itakupekeka Moja Kwa Moja Kwenye Chanel Yetu Ya You Tube Subscribe Like Share And Coment Huko Ndiko Chanzo Changu Cha Mapato" - ameandika mwigizaji huyo filamu

photo content

"Lazima ujiamini katika kitu chako kabla ya kumwaminisha mtu, watu wanasema wewe unajiita Goddess (Mungu), hapana!. Sijasema
"Lazima ujiamini katika kitu chako kabla ya kumwaminisha mtu, watu wanasema wewe unajiita Goddess (Mungu), hapana!. Sijasema mimi ni Mungu, lakini mimi ni mtoto wa Mungu," - Rosa Ree, Msanii wa muziki wa Hip-hop Tanzania Toa maoni yako #MvanoUdaku #MvanoMtangazaji #M32

Kama baba Kama mtoto😍
Kama baba Kama mtoto😍

Baada ya kusambaa kwa video ya Mwindaji wa Marekani, Josh Bowmer akifurahia kuwinda mamba mkubwa nchini Tanzania mwenye rekodi ya dunia na kuleta taharuki, Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori (TAWA) imesema inaendelea na uchunguzi kuona kama kuna ukiukwaji wa Sheria za uwindajim Taarifa ya TAWA imesema mara baada ya uchunguzi kukamilika taarifa kamili itatolewa na hatua za kisheria zitachukuliwa iwapo ukiukwaji utabainika. “TAWA inapenda kufahamisha Umma kuwa uwindaji wa kitali hufanyika kwa kuzingatia sheria ya Uhifadhi wa Wanyamapori sura ya 283 pamoja na kanuni za uwindaji wa kitalii za mwaka 2015 na marekebisho yake ya mwaka 2017, 2019 na 2020, uwindaji wa kitalii pia husimamiwa na Mkataba wa Kimataifa wa Biashara ya Wanyamapori na Mimea iliyohatarini kutoweka (Convention on International Trade In Endangered Species of Wild Fauna and Flora - CITES) ambao Nchi yetu imeridhia. “Mamba ni miongoni mwa wanyamapori wanaolindwa na mkataba huu na wamewekwa katika kundi la pili (Appendix II) ambalo linaruhusu matumizi ya uvunaji ikiwemo windaji wa kitalii, masharti ya uwindaji wa mamba kwa muibu wa Kanuni na Mkataba wa CITES ni kuhakikisha mamba wote wanaowindwa chini hawazidi 1,600 kwa mwaka, mamba anavewindwa ana urefu usiopungua sentimita 300, vibandiko maalum (Skin tags) vinafungwa katika ngozi za mamba wanaowindwana (iv) Vibali vya CITES (CITES export permit) vinatumika kusafirisha nyara zitokanazo na mamba waliowindwa” imeeleza taarifa ya TAWA. “Chini ya Sheria na Mkataba huo, Mtu yeyote anaruhusiwa kufanya uwindaji wa kitalii baada ya kupata kibali kutoka TAWA na kutimiza masharti kama ilivyobainishwa hapo juu, TAWA inawajibu wa kusimamia uwindaji huo katika hatua zake zote, kumbukumbu tulizonazo zinaonyesha kuwepo kwa vibali vya uwindaji wa wanyamapori ikiwemo mamba katika maeneo mbalimbali nchini” — TAWA

photo content

Inafikirisha kumbe tulikuwa na mamba mrefu zaidi duniani na hatujui ? Kama tulikuwa tunajua mbona hatukutangaza mapema kuhusu
Inafikirisha kumbe tulikuwa na mamba mrefu zaidi duniani na hatujui ? Kama tulikuwa tunajua mbona hatukutangaza mapema kuhusu mamba huyu ili kuitangaza nchi ? Au kama tulikuwa tunajua mbona tukaruhusu awindwe like seriously ? Kama hatukuruhusu kwahiyo muwindaji katupiga je kwa kushirikiana na WAKINA nani ? Kama muwindaji katupiga je ni hatua gani za kisheria za kuchukulia? Kama muwindaji kawinda kwa sheria za nchi je nchi imefaidikaje ? Je ukipma faida ambazo nchi ingepata ni bora alivyowindwa au angeachwa kwa utalii ?