1 307
订阅者
+124 小时
-27 天
-1330 天
帖子存档
1 307
Wachezaji wa Timu ya Soka ya Wanawake ya Ivory Coast 🥶🥶🥶🥶
Video kamili hapa👉🏻 HIZI NDIO HESABU ZA SIMBA SC KIMATAIFA
Meneja Habari wa klabu ya Simba @ahmedally_ amesema kuwa hesabu zao ni Mechi 4 za Awali zitawapeleka Robo Fainali
"Sijawapa hesabu zetu kwenye ushiriki wetu wa Champions League
"Tunachukua Alama Tatu Dhidi ya Asec Mimosas Then tunakwenda Botswana Kuchukua Alama 3 nyingine, tukitoka Botswana tunakwenda Morocco Kwa Wydad Kuchukua Alama 1 then tunageukanae Tunakuja kumnyoa Wydad Hapa Tanzania tunachukua Alama 3 nyingine..
Tunakuwa tumefikisha Alama 10 Mnyama anakwenda Robo Fainali Baada ya Mechi NNE za Mwanzo na Uwezo huo tunao Tubaingia Robo Fainali mapema" Ahmed Ally
Una maoni Gani ✍️
Follow Ukurasa Wetu wa Instagram 👇
https://instagram.com/sportslitetv?igshid=OGQ5ZDc2ODk2ZA==
1 307
TV station gani wana vipindi vizuri zaidi kati ya hizi?
1. Eatv
2. Tbc
3. Wasafi tv
4. Clouds tv
5. Itv
Follow ukurasa wetu wa Instagram 👇
https://instagram.com/sportslitetv?igshid=OGQ5ZDc2ODk2ZA==
1 307
"Yupo anayekaa na kufurahia hili la mwenzenu hata hofu ya Mungu unakosa aiseee. Yanaumiza haya mambo usiombe yakukute, ila kuna mijanaume ina mambo ya kiwaki sana, unajisikiaje kumdhalilisha mtu alafu unapata nini kama sio laana tu. Hata Allah anasema kila atakayemdhalilisha binadamu mwenzie kwa makusudi basi nae atadhalilishwa na Allah"- Ameandika Mwigizaji Husna Sanjenti kufuatia mambo yanayoendelea kwenye Mange Kimambi App
1 307
AJALI YAUA WATU 14 LINDI
Watu 14 wamefariki dunia leo Novemba 26, 2023 katika ajali ya barabarani iliyohusisha basi la Kampuni ya Baraka lililokuwa likitokea Tandahimba, mkoani Mtwara kuelekea Dar es Salaam.
Ajali hiyo imetokea majira ya saa moja asubuhi katika eneo la Mtama na chanzo cha ajali hiyo kikielezwa kuwa ni breki za basi hilo kufeli.
Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, John Imori amesema miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya Nyangao pamoja na majeruhi 26 wanaendelea na matibabu.
#AzamTVUpdates
Habari ya Mohamed Nyaulingo imehaririwa na Claud Mshana
1 307
"Mimi kuonekana naanza kuzeeka si ajabu kwa sababu hiyo ni safari yetu sote, hata bibi alikuwa binti kwahiyo kuzeeka ni jambo la kawaida. Sijawahi kuolewa na hii ni kwa sababu bado sijapata mume sahihi wa kunioa"- Blandina Chagula maarufu Johari, Mwigizaji wa filamu Tanzania.
Toa maoni yako
1 307
Mchezaji wa kimataifa wa Tanzania, Enekia Kasonga Lunyamila anaecheza katika timu ya Wanawake ya Eastern Flames FC ya Saudi Arabia usiku wa jana amefunga magoli nane (8) kwenye ushindi wa mabao 18-0 katika mchezo wa kwanza wa Kombe la FA (Women's Cup).
1 307
"Mimi binafsi sioni uhusiano wa Milioni zako miangapi bank na kumsafisha mume wako miguu, kumsafisha masikio, kumkata kucha, kumpikia chakula wewe mwenyewe, kumfulia nguo mwenyewe. Licha ya kwamba nina pesa lakini nafanya kila kitu kwa mume wangu, hata ukiniangalia mikono yangu hii ina sugu hauwezi kunikuta nimefuga kucha, wala sina dada wa kazi, kazi zote nafanya mwenyewe hasa zinazomhusu mume wangu"- Maznat Bridal, mmiliki wa Maznat College
1 307
NJ: RONALDO NI ROLE MODEL WANGU NDIO MAANA NASHANGILIA KAMA YEYE.
"Nilipokuwa mdogo, nilimpenda Cristiano Ronaldo. Nilikuwa na jina lake kwenye jezi yangu ambayo nilikuwa nikivaa kila mara."
"Haikuwa jezi orijino kwa sababu ni jezi orijino ni ghali sana.... lakini nilikuwa na jezi ambayo nilivaa ikiwa na namba 7, na na Jina la Ronaldo limeandikwa kwa kalamu."
"Nilifanya (kuandika) hivyo mwenyewe nilipokuwa mtoto. Kusema kweli nilitamani sana kuwa kama yeye, lakini ilikuwa vigumu kutazama mechi anazo cheza kwa sababu ulihitaji kulipa kiingilio kwenye kibandaumiza cha ili uangalie mechi zake akiwa Real Madrid"
"Nilicheza nikiwa na viatu vyangu vya shule au kwa miguu peku. Labda miaka 16 ndipo nilipopata viatu vyangu vya kwanza."
"Mama yangu alininunulia, vilikuwa ni vya bei nafuu, sio kama kiatu chenyewe kile orijino bali kilikuwa kiatu cha mitumba. Sikukichezea mwanzoni baada ya kununua kwa sababu sikuzizoea."
"Nilizoea kucheza peku. Kwa hivyo ilichukua muda ili kuweza kukizoea kidogo."
NICOLAS JACKSON 🇸🇳,Mshambuliaji wa Kimataifa wa Senegal na timu ya Chelsea.
1 307
HAMAS WANAACHIA MATEKA WA ISRAEL, WAKATI ISRAEL WANAACHIA WAFUNGWA WA KIPALESTINA.
Leo Israel na Hamas zimebadilishana wafungwa na mateka, baada ya makubaliano yaliyofikiwa mapema wiki hii ya kuwaachilia mateka 50 waliozuiliwa Gaza dhidi ya wafungwa wa Kipalestina wakati wa mapumziko ya siku nne ya mapigano.
Mkataba huo unapaswa kuona jumla ya Wapalestina 150 wanaoshikiliwa katika jela mbali mbali nchini Israel kuachiliwa huru, ikiwa ni pamoja na ongezeko kubwa la misaada ya kibinadamu kuruhusiwa kuingia Gaza.
Mnamo mwaka 1977, ndege iliyokuwa imebeba idadi kubwa ya raia wa Israel ilitekwa nyara kwa sharti kama hili la kuachiwa kwa wafungwa wa Kipalestina. Israel ilikataa kata kata na ikafanya uokoaji katika mkasa unaotambuliwa kama Entebe 77 ulitokea nchini Uganda.
Leo hii Israel wanakubali kuwaachia huru wafungwa wa Kipalestina kwa masharti yale yale ya mwaka 1977.
Nini maoni yako?! Unadhani nani aliyefanikiwa?! Je, ni serikali ya Israel, au Wanamgambo wa Hamas?!
1 307
KOREA KASKAZINI WAFANIKIWA KUFIKISHA SATELLITE YA UCHUNGUZI KATIKA ORBIT
Mara baada ya kushindwa kwa mara kadhaa sasa hatimaye Korea Kaskazini wamefanikiwa kupeleka na kuweka satellite yao kwenye orbit ya dunia yetu .
Imeelezwa kuwa satellite hiyo itakuwa na aina ya matumizi ya kiuchunguzi katika nchi za Japan na Korea Kusini kwa ujumla wao kati yao na Marekani ambao wamekuwa wakifanya harakati mbalimbali za kijeshi karibu na mipaka ya Korea Kaskazini .
Malligyong-1 ndio jina la satellite hiyo ambalo limebatizwa na viongozi wa sarikali ya Korea ya Kaskazini na kwamujibu wa vyombo vya habari vya Korea Kaskazini vimesema kuwa kuna satellite nyingi zitarushwa baada ya mafanikio ya satellite hii ya kwanza
Korea Kaskazini walitumia rocket yao ya Chollima - 1 kufikisha satellite yao kwenye orbit ya dunia yetu , kumbuka kwa mara hii hawakujaribu kutumia kombora la masafa marefu kukamilisha jambo hili ila waliamua tu kutumia rocket kwa kukamilisha jambo lao kubwa .
Nadhani bado tunapata maswali mengi kuhusu kufanikiwa kwa Korea Kaskazini , Je ni nani aliyeko nyuma yake ambapo watu wengi wamekuwa wakisema kuwa pengine safari ya Kim Jong Un baada ya kufeli kurusha satellite yao kwenye orbit hapo awali pengine safari yakr kuelekea Urusi imekuwa na matunda haya ambayo tunayaona kwa sasa .
Marekani wamesema kuwa Korea Kaskazini kurusha satellite yake hiyo ni kwenda tofauti na Umoja wa mataifa wanavyotaka , kiufupi wamevunja sheria za umoja wa mataifa juu ya kanuni za usalama wa dunia .
💯💯💯💯💯💯💯💯💯💯💯💯💯💯💯💯
Kwa asilimia 95 Urusi amehusika katika jambo hili na niliwahi kusema kuwa safari ya Kim Jong Un Urusi ni ya kwenda kuhakikisha wanasayansi wake wanapata uelewa mzuri kabisa katika kutengeneza chombo ambacho kitakuwa na nguvu ya kuhakikisha satellite yao haishindwi kwa mara hii
Naweza kusema kuwa uwepo wa satellite ya Korea Kaskazini ya chunguzi za taarifa za siri nadhani kutakwenda kuongeza tensions kubwa sana baina ya nchi hizo Marekani , Japan , Korea na Milliam
Ni wazi kuwa ni nchi mbili peke yake ndizo zenye tekinolojia ya kwao wenyewe ya masuala ya anga za mbali katika uundaji wa vifaa kama rocket na vyenginevyo kwahiyo ni wazi kabisa baadhi ya nchi zinaendelea kutumia tekinolojia za nchi mbili ambazo ni Marekani na Urusi
Kwahiyo natapa uhakika kuwa kwa aina ya rocket ambayo wameitumia Korea Kaskazini muundo wake ni wazi kabisa ni moja wapo ya miundo ya nchi ya Urusi kwahiyo ni wazi kabisa kuwa Korea kaskazini walipata usaidizi wa Urusi katika safari ya Kim kule Urusi
1 307
Hilo Sio duka Bali Ni Jezi Ambazo Mchezaji Wa Zamani Aa Liverpool MARTIN SKERTAL Alibadilishana Na Wachezaji Wenzake Uwanjani Pindi Alipokua Ana Piga Noli.
1 307
#HABARI Martine John (40) Mkazi wa Geita Mjini amejinyonga hadi kufa baada ya kumjeruhi mke wake kwa kumkata na panga sehemu mbalimbali za mwili wake na kudhani kuwa amefariki huku chanzo cha tukio hilo likitajwa kuwa ni wivu wa mapenzi.
Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Novemba 22/ 2023 katika mtaa wa 14 Kambarage Halmashauri ya mji wa Geita Mkoani Geita
Mama mzazi wa mwanamke aliyejeruhiwa sio mara ya kwanza kwa wawili hao kugombana na wamekuwa wakipatanishwa mara kadhaa
"Walishawahi kugombana akaja nyumbani Mkwilima nikawasuluhisha wakarudi nyumbani sasa jana ndo napigiwa simu mtoto wako kachomwa kisu na mkwe wako amejinyonga" amesema Anastazia Paul Mama mzazi wa Majeruhi
Kaimu kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Geita ACP Adam Maro amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema chanzo cha tukio hilo ni wivu wa kimapenzi baada ya mwanaume huyo kukagua simu ya Mke wake. Dawa Za Asili Tanzania Kutoka Shinyanga
