1 307
订阅者
+124 小时
-27 天
-1330 天
帖子存档
1 307
SAA YA RONALDO 🇵🇹 INAWEZA KUSAJILI WACHEZAJI SIMBA/YANGA.
Mshambuliaji wa Klabu ya Al Nassr 🇸🇦,Cristiano Ronaldo 🇵🇹 hapo jana alihudhuria tukio la Masumbwi akiwa amevaa saa aina ya Hublot Spirit of Big Bang "KING GOLD RAINBOW" ambayo kwa Ulaya inauzwa dola za Kimarekani $100,000 ambazo ni zaidi ya shilingi Milioni 251.4 za Kitanzania.
Kwa wachezaji wa ndani wa Tanzania,kupitia thamani ya saa hiyo Ronaldo 🇵🇹 anaweza kulipa ada ya kusajili wachezaji watatu mpaka watano.
KITU CHAKO CHA THAMANI ZAIDI ULICHOWAHI KUVAA MWILINI KINAUZWAJE 👇🏿
1 307
#ForSure kutoka mtandao wa X ametudondoshea sifa za watu wa kimya. Je, unakubaliana kiasi gani na sifa hizi alizozitaja?
Dondosha kwenye comment sifa nyingine unazozijua za watu wa kimya.
1 307
Nikamkuta Casino la Wadachi na Walatino
Akigonga mvinyo, wa hashipapi, hashipinyo
Pechie chipinyo na pamba za mandarino
Macho yalinitoka mithiri ya zingonginyo
Hivi hapa Prof. Jaya hakutupanga kweli?
1 307
VYAMA LAZIMA VIBADILIKE
“Vyama vya Siasa haviwezi kuzungumzia usawa wa kijinsia kama vyenyewe havitaki kubadilika na vinakumbatia mfumo dume. Kabla ya kuibadili nchi, sisi wenyewe wanasiasa ni lazima tubadilike kwa kuhakikisha usawa wa kijinsia ndani ya Vyama vyetu” alisisitiza Ado Shaibu Katibu Mkuu ACT WAZALENSO
1 307
Wanandoa 61 wamepeleka maombi ya talaka kwa ajili kuvunja ndoa zao katika Baraza la Kata ya Kivavi Halmashauri ya Mji wa Makambako mkoani Njombe kwa kipindi cha mwezi mmoja na wiki mbili kuanzia November hadi December 20 mwaka huu.
AyoTV imezungumza na Mwenyekiti wa Baraza hilo Muhimba Payovela aliyethibitisha kupokea migogoro mingi ya Wanandoa kuliko ya ardhi huku akieleza kuwa sababu kubwa ya Wanandoa wengi kudaiana talaka ni kutoaminiana na wengine kuendekeza tamaa.
“Ndoa 61 kila mmoja anataka kuvunja ndoa yake hakuna anayekuja kusema anataka kusuluhisha bali kila mmoja anasema sitaki tena ndoa” ——— Payovela
Baadhi ya Wananchi wa Mji wa Makambako wamesema maombi ya talaka kwa Wanandoa yanachangiwa na wengi wao kutoridhika na walichonacho na baadhi ya Wanawake kutaka usawa ndani ya ndoa zao huku wengine wakitaka kuzivunja kutokana na vitendo vya ukatili wanavyofanyiwa.
1 307
Matokeo ya utafiti yanaonyesha kwamba ikiwa utalala kwa muda mrefu zaidi wakati wa wikendi, basi unapunguza hatari ya kupata shambulio la moyo
Kwa mujibu wa Fox News, watu ambao walilala kwa angalau saa moja zaidi wakati wa wikendi kuliko siku za kawaida walionyesha viwango vya chini vya magonjwa ya moyo - hasa, kiharusi, maradhi ya moyo wa koroni na maumivu ya kifua yanayotokana na ukosefu wa mtiririko wa damu, ikilinganishwa na wale ambao hawalali kufidia muda wa kulala.
Hatari ya kupata magonjwa hayo ilionekana kupungua zaidi kwa wale ambao hulala chini ya saa sita kwa siku za kawaida na hulala kwa angalau masaa mawili zaidi wakati wa wikendi.
________
M-tag rafiki yako anaependa kulala sana wikendi, mwambie kuna ujumbe wake huku😁
1 307
Hata hivyo Mungu mkubwa, Ray C alijitambua na kuachana na madawa ya kulevya, kwa sasa nimepata tetesi kuwa yupo Nchini Ufaransa ameolewa huko, kama ni kweli basi habari hizi ni njema, na mimi na watanzania wenzangu wote, tunamtakia kila kheri katika ndoa yake huko alipo...
NA VIPI KUHUSU WIMBO WAKE WA UKO WAPI...
JE NI KWELI ALIMUIMBIA MPENZI WAKE???
Nitaorodhesha majibu yote ya swali hilo, kulingana na kile ambacho kilinaswa na wadakuzi, miaka hiyo ya 2002,
Mimi sijawahi kukaa chini na kisha kupiga Stori na Ray C, Lakini ni miongoni mwa watu ambao walishawahi kudhuru katika moja ya Club, ambayo Ray C alikuwa akipiga Shoo, kushuhudia kwangu Shoo ya Ray C, haiwezi kuwa sababu ya mimi kusema namjua Ray C, isipokuwa nitabaki katika kundi lile lile lenye kumtambua Ray C Kama Msanii...
Miaka ya 2002 wadakuzi wa mambo ya mjini, waliingia ndani ndani ya maisha ya Ray C, kisha kumulika tochi upande wa mahusiano yake, wakatujia na habari kuwa Ray C yupo mapenzini na Freshi Jumbe mkuu....
Freshi Jumbe mkuu ni nani???
Alikuwa ni mwanamuziki na mtayarishaji wa muziki Nchini Tanzania, pia Freshi Jumbe mkuu alikuwa ni mtunzi wa nyimbo mbalimbali, Freshi Jumbe alikuwa na kipaji, na aliweza kufanya kila aina ya Muziki, kuanzia Dansi R&B pamoja na Hip Hop, kabila lake ni Mzigua na ni Mzaliwa wa Tanga, Jina Lake la utani alikuwa akiitwa Kungugu Kitanda Milima, madogo wa miaka ya 2000 ni vigumu kumtambua huyu Mwamba, kwanini??? Aliondoka Tanzania wakiwa bado hata hawajajua kujiogesha wenyewe,
Basi wadakuzi wa mambo ya mjini,
Walisema Ray C alikufa na kuoza kwenye penzi la Mshikaji, ingawaje mahusiano yao yalikuwa ni ya siri, na hata magazeti yaliishia kuandika tetesi tu ya mahusiano hayo,
Kumbuka kwamba penzi hilo lilianza kabla ya Ray C kuimba muziki,
Wakati huo akiwa bado ni mtangazaji,
Lakini akiwa katika harakati za kuingia kwenye muziki,
Ni nyakati hizo hizo Freshi Jumbe mkuu naye, akahamisha makazi nje ya Nchi,
Wadakuzi walisema Freshi Jumbe baada ya kuondoka Nchini Tanzania, breki ya kwanza ilikuwa China, kabla ya baadaye kwenda kuweka kambi Tokyo Nchini Japani, ambapo ndipo alipo mpaka sasa,
Huku nyuma Ray C akaanza kusikika kama Msanii na si mtangazaji tena, katika kutunga tunga Ray C akatunga wimbo wa Uko wapi??? Hili ni swali ambalo Ray C anauliza,
Katika huu wimbo Ray C Kuna mstari anasema,
Tafadhali niambie
Hata kwa barua pepe
Au simu ya mkononi
Roho yangu itulie
Roho yangu itulie
Wadakuzi wa mambo ya mjini waliunganisha matukio kuanzia katika mistari ya wimbo huo, mpaka kwenye video ya wimbo huo, ndipo wakabaini wimbo huo Ray C amemtungia Mpenzi wake, tukio la kwanza ni kitendo cha Ray C kusafiri mpaka China, ambapo ndipo Mshikaji alipoenda baada ya kuondoka Nchini, huko alikwenda kwa ajili ya kuchukua video ya wimbo huo, matukio mengine ni haya,
Video mwanzo mpaka mwisho hakuna sehemu ambayo Ray C ameangalia juu mawinguni kwa dakika hata mbili, video inapoanza Ray C baada ya kutoa sauti ya kulalama alipeleka uso wake juu, na kuyafumbia macho yake katika hali ya kihisia, (naomba mjue kutofautisha hisia) na kama hiyo haitoshi sehemu kubwa ya video Ray C anaonekana akiwa katika sehemu yenye mikusanyiko ya watu...
Maana yake nini hapo??? Ni kuonesha kuna mtu anamtafuta katikati ya mikusanyiko hiyo, Oya sikieni, wakati wimbo huu unatoka, kuna moja ya gazeti la udaku (jina limenitoka kidogo) liliandika (Mapenzi yanamfanya Ray C kutunga wimbo)
Ni kweli Ray C kwa mdomo wake amesema wimbo huo amemtungia Marehemu baba yake,
Lakini naomba niwaambieni kitu kimoja kuwa, hakuna mwenye kupenda kuonekana kashindwa,
Kama wimbo huo ungepelekea Ray C kukutana na mlengwa, na mpaka sasa angekuwa anaishi na mlengwa huyo, ingekuwa rahisi yeye kukiri wimbo ulikuwa kwa ajili ya mlengwa, lakini kwa sababu hajafanikisha kumpata mlengwa, ndiyo maana majibu yake ni kuwa wimbo ni wa marehemu baba yake, siyo mbaya tukamuamini ili maisha mengine yaendelee,
Asanteni sana wote naomba kuhitimisha,
Mwisho
Imeandikwa na @ustadh musto
1 307
NGOJENI NIWAFAFANULIE KUHUSU RAY C.......
NA WIMBO WAKE WA UKO WAPI,
SEHEMU YA MWISHO,
Ray C ni nani???
Jina lake halisi ni Rehema Chalamila,
Ni mwenyeji wa Mkoani Iringa,
Kuhusu mwaka wa kuzaliwa kwake, wapo wanaosema alizaliwa mwaka 82, na wengine wanasema 83, binafsi siwezi kuliongelea hili la kuzaliwa kwake, kwanini??? Kwasababu bado sijajua niwaamini watu gani, kati ya hao wa mwaka 82 au wa 83,
Aina ya Muziki wa Ray C ni Taarab, dansi, Bongo bhangra Katika kazi yake ya Muziki Ray C, amefanya kazi na wasanii wengi akiwemo, Ay, Dknob,
Chid Benz, Mh Temba, Squeezer, na Nako 2 Nako, na wengineo, Pia Ray C alishawahi kucheza kama Video Vixen kwenye wimbo uitwao Regina, wa Akili The Brain, katika wimbo huo Akili pia alimshirikisha Steve 2k,
Lakini naomba niseme tu Kabla ya kuingia katika ulingo wa Bongo Fleva, Ray C aliwahi kufanya kazi kama mtangazaji wa redio ya East Africa kabla ya kwenda redio ya Clouds FM zote za jijini Dar es Salaam,
Ray C naye ni miongoni mwa wasanii, ambao wamepita katika mikono ya aliyewahi kuwa, mkurugenzi wa vipindi wa Clouds FM, Marehemu Ruge Mutahaba, na Ruge ndiye aliyesimamia nusu ya gharama, wakati wa kushutiwa kwa video ya wimbo wa Na wewe milele, video hii ilichukuliwa huko visiwani Zanzibar,
Wimbo wa kwanza wa Ray C unaitwa Sikuhitaji, katika kiitikio cha wimbo huo, Ray C anasema hivi......
Nimekuvumilia sana
Nimeteseka mimi sana
Nimechoka nenda zako
Wala sikuhitaji tena
Nimekuvumilia sana
Nimeteseka mimi sana
Nimechoka nenda zako
Wala sikuhitaji tena
Katika Verse ya kwanza Ray C anasikika akisema....
Mwanaume gani huna hata huruma
Kazi yako wewe kunisemasema
Mapenzi yako yamekwenda wapi
Aah aah sikutaki
Sasa sasa basi
Achana nami ondoka zako
Sikuhitaji sikutaki
Baada ya hapo anarudia tena kiitikio,
Kisha anakuja na Verse ya pili yenye maneno ya namna hii.....
Nasema kutoka moyoni mwangu
Nimechoka na tabia zako
Bora niachane nawe
Aah aah nimechoka
Natafuta mwingine wa kunionyesha mapenzi ya dhati
Dhaa dhaa dhaati
Dhaaidhaa dhaati
Umahiri wake wa kukata viuno,
Ulimfanya abatizwe jina la kiuno bila mfupa, kila mtanzania mwenye pumzi na apendaye Bongo Fleva, alimpenda Ray C, Either kwa sauti yake au kwa namna anavyotikisa kiuno chake, ukitoa wimbo wa Sikuhitaji pia Ray C alitoa nyimbo nyingine kama zifuatazo, Mapenzi Yangu, Na wewe Milele,
Ulinikataa na nyingine nyingi zilizompa umaarufu na hata kupelekea kuutingisha muziki wa Bongo Flava, katika upande wa Tuzo Ray C,
Mwaka 2004 alishinda Tuzo ya Tanzania Music Awards katika kipengele cha Msanii bora wa kike,
Mwaka huo huo wa 2004, katika Tuzo za Kisima Music Awards, Ray C alishinda kwenye kipengele cha Msanii bora wa kike kutoka Uganda & Tanzania,
Mwaka 2007 katika Tuzo za Tanzania Music Awards, Ray C aliibuka tena na ushindi, katika kipengele cha msanii bora wa kike....... katika Tuzo ambazo Ray C alishiriki, ni Channel O Music Awards, alishiriki mwaka 2005, katika kipengele cha Msanii bora wa Afrika mashariki,
Mwaka 2006 mpaka 2008 Ray C alishiriki Tuzo za Pearl of Africa Music Awards, katika miaka yote hiyo Ray C alishiriki katika kipengele cha Msanii bora wa kike kutoka Tanzania, bado kuna Tuzo nyingi na nyingi, ambazo Ray C alishiriki, nyingine sitozitaja hapa, lakini pia naomba mjue kutofautisha, kushiriki na kushinda, neno ameshiriki msiliingize katika maabara ya ushindi, sijui tumeelewana???
Ray C alikuja kupotea kwenye gemu,
Baada ya kujiingiza katika matumizi ya madawa ya kulevya, nadhani hili ni la juzi juzi na wengi wenu mnalijua, Mwaka wa 2012, Rais wa Tanzania kwa wakati huo, Jakaya Kikwete, alitoa msaada mkubwa wa fedha kwa ajili ya matibabu ya Ray C, na baada ya huduma mwimbaji huyu alikwenda kumshukuru Mheshimiwa huyo kwa msaada wake. Lakini ilipofika Mwaka wa 2016 ikaripotiwa tena kwamba Ray C amerudia tabia yake ya kutumia dawa za kulevya, hali ambayo ilimkera sana mzee Kikwete.
1 307
𝗔𝗟𝗜𝗞𝗜𝗕𝗔 𝗔𝗭𝗨𝗡𝗚𝗨𝗠𝗭𝗜𝗔 𝗕𝗜𝗙𝗨 𝗟𝗔𝗞𝗘 𝗡𝗔 𝗗𝗜𝗔𝗠𝗢𝗡𝗗 𝗞𝗪𝗘𝗡𝗬𝗘 𝗜𝗡𝗧𝗘𝗥𝗩𝗜𝗘𝗪
Kunikosea kwa Diamond nilihakikisha mwenyewe kutokana mimi mwenyewe ndo nilifanya nyimbo yake ya Lala Salama kwenye album yake na akanifuta, Nikahisi amenikosea sanaa maana nilichoimba mimi akawa ameimba yeye..
Full Interview nimekuekea hapa👇👇
KUTOKA MITANDAONI
Kwa habari zaidi SUBSCRIBE kupitia YOUTUBE channel yetu kwa ku bonyeza hapa chini.👇.kwenye link
https://youtube.com/@E-PlusMediaTv?si=JjehK80_nkzrHGNK
1 307
FULL VIDEO NA MATUKIO MAZIMA UTAYAPATA KWA KU BONYEZA HAPA KWENYE INSTAGRAM LINK:-https://instagram.com/e_plus_media?utm_medium=copy_link
FACEBOOK PAGE FOLLOW:-https://www.facebook.com/eplusmediatv/
1 307
Refarii mkongwe wa kimataifa wa Gambia 🇬🇲 Bacary Gassama ametangaza kustaafu kuchezesha soka baada ya kudumu kwenye tasnia hiyo kwa mafanikio makubwa.
Gassama amechezesha michuano mbalimbali ikiwemo Kombe la Dunia, AFCON, CAFCL na CAFCC ikiwemo fainali ya mwaka 2017.
Hapo pichani ni mwamba akizozana na Mohamed Salah kwenye michuano iliyopita ya AFCON wakati wa mechi kati ya wenyeji Cameroon 🇨🇲 vs Egypt 🇪🇬 na alimwambia Salah "Basi nikupe filimbi uchezeshe wewe" 😆.
🤪Peponi atapasikia tuuu huyu mwamba nakumbuka aliwaonea mno 1 Do Agosto mwaka 2019 nusu fainali ya CAF Champions League pale Stade de Rades mjini Tunis dhidi ya Esperance Sportive de Tunis walifunga mabao mawili akasema offside Kisha akatoa penalty ya mchongo dakika ya 90+5. #AfricanFootball
Credit ✍️ @enockbwigane
#mpekeo_mtandala
1 307
Wanaume wameshauriwa kushiriki kuwasaidia wake zao katika mchakato wa kujifungua kwa kuwa uwepo wao unasaidia kupunguza kwa asilimia kubwa maumivu ya uchungu pamoja na vifo.
Akizungumza na Swahili Times, Daktari kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala, Dkt. Raphael Ung'eng'e amesema pindi wanapopeana faraja, humsaidia mjamzito kupunguza uchungu na hata akijifungua asilimia kubwa huwa salama.
“Ndo maana sasa hivi ukiangalia hospitali nyingi zinatia mkazo kuwa na mwambata wakati wa kujifungua na walitamani sana mwambata huyu awe mwanaume.
Kumpata mwambata especially mwanaume au mumeo au yule ambaye ndiye baba wa mtoto inasaidia kupunguza vifo vya mama na mtoto kwa asilimia kubwa sana, lakini pia inasaidia kumpunguzia mama kiwango kikubwa cha mateso. Kwahiyo wanaume tusiogope kuwa mwambata kwa wake zetu,” ameeleza.
1 307
Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Fransisko ametangaza eneo la Mafinga mkoani Iringa kuwa Jimbo Jipya Katoliki na kumteua Padri Vincent Mwagala wa Jimbo Katoliki la Iringa kuwa askofu wa kwanza wa jimbo hilo jipya.
Kwa mujibu wa taarifa ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) iliyosainiwa na katibu wake mkuu, Padri Charles Kitima, leo Desemba 22, 2023,
uteuzi huo unaanza leo huku jimbo hilo likipewa jina katika lugha ya kilatini ‘Mafingens’. Askofu Mteule Mwagala amezaliwa Desemba 11, 1973 huko Makungu Wilaya ya Mufindi,
Jimbo Katoliki la Iringa. Baada ya masomo ya upadri, alipewa daraja takatifu la upadri Julai 11, 2007 jimboni Iringa na kuhudumu katika nafasi tofauti za utume nchini Italia na jimboni Iringa.
Source Mwananchi
1 307
MAJI YA SHINGO YALIFIKIA PENZI LA HAJJI MANARA.
Ni kama penzi la Hajji Manara na Zaiylisa limeanza kuteteleka kutokana na yanayoendelea mtandaoni. Mapema jana charts zao zilidukuliwa ambapo Hajji Manara alikuwa anajikomba-komba kwa Zaiylisa asisikilize maneno ya watu wala asiyumbushwe na wanaowatakia mabaya waachane.
Ukiachana na charts hizo, watu wengi wanasema Hajji Manara anatumia nguvu nyingi kuonyesha kwamba wanapendana kuliko hata uhalisia wenyewe na hata kwenye video zao nyingi, Zaiylisa amekuwa akionyesha sura mfifio ambayo inaonyesha kwamba analazimishwa kujibebisha kwa Manara na amechoka; wanasema walimwengu.
Licha ya watu mbalimbali kumpa ushauri apunguze Show Off mtandaoni, ndio kwaaanza Hajji anazidi kutamba ambapo amesema yeye na mwandani wake huyo ndio wanatamba mjini kwa sasa.
1 307
Mwigizaji staa wa filamu ya Fast Furious, Vin Diesel anakabiliwa na kesi ya unyanyasaji wa kijinsia alioufanya wakati wa uandaaji wa filamu hiyo ya Fast & Furious mwaka 2010 huko Georgia nchini Marekani.
Kesi hiyo imefunguliwa Los Angeles na aliyekuwa msaidizi wake Asta Jonasson siku ya Alhamisi, Disemba 21, ambapo anadai kuwa mwaka 2010 katika hoteli ya St. Regis, Atlanta mwigizaji huyo wa filamu ya Fast & Furious alimvuta Jonasson kwenye kitanda kwa nguvu, na kuanza kumpapasa kifuani na miguu, piga busu na kisha kujichua.
Jonasson amesema kipindi hicho aliajiriwa na One Race Films, kampuni ya utayarishaji, kuwa msaidizi wa Diesel wakati filamu ya ‘Fast 5’ ikifanyika.
Hata hivyo Jonasson amedai alikaa kimya kwa muda mrefu kwa kuhofia nguvu ya Diesel huko Hollywood, lakini pia hali yake ya uhamiaji kama mmiliki wa green card kwa maana siyo raia wa Marekani bali ni mkazi wa kudumu tu.
1 307
Anaandika Dj wa msanii Diamond Platnumz @Romyjons
"DEPRESSION,ANXIETY ,HOFU,WASIWASI VINAZIDI KUONGEZEKA KWA ASILIMIA KUBWA SANA HASA KWA VIJANA!!! NAOMBENI TUMUOMBE MUNGU ATUONDOLEE HIZO HALI IN SHA ALLAH KUNA KITU HAKIPO SAWA TUSALINI JAMANI"
Nini maoni yako?
1 307
"Sipendezwi na kitendo cha mashabiki kunishindanisha na Wasanii wakubwa walionitangulia wakiwemo Diamond Platnumz, Costa Titch. Hii inaniharibia kwa sababu bado nahitaji msaada na sapoti kubwa kutoka kwa kaka zangu hivyo wanaponishindanisha wananiharibia kwa sababu wananitengenezea chuki baina yangu na wasanii wakubwa" - Chino, Lsanii wa muziki Tanzania.
Toa maoni yako
