1 307
订阅者
+124 小时
-27 天
-1330 天
帖子存档
1 307
#HABARI Polisi huko katika wilaya ya Ntungamo nchini Uganda, wanamshikilia mzee mmoja mwenye umri wa miaka 110 kwa tuhuma za kumuua mkewe mwenye umri wa miaka 109 kwa kosa la kumnyima unyumba.
Kwa mujibu wa msemaji wa polisi wa mkoa wa Rwizi Samson Kasasira, Mzee Dominic Babiiha anatuhumiwa kumuua mkewe Costansio Bakasisa akitumia mundu majira ya saa 1 asubuhi jumamosi huko nyumbani kwao eneo la Kahunga.
Taarifa Zaidi zinatanabaisha kwamba wazee hao ambao ni wakulima wamekua wakiishi vyuumba tofauti tangu walipooana.
Polisi wamesema mkewe alikataa kumpa tendo la ndoa sababu alikua akijisikia vibaya, ambapo licha ya hayo bibi huyo aliendelea kulazimishwa tendo hilo ambapo aliamu kwenda kulala chumba cha wajukuu zake.
Mzee huyo aliamua kuchukua mundu na kumuamuru atoke nje ya chumba, ambapo aliingia kwenye chumba hicho na kumshambulia na mundu mfululizo huku wajukuu wakikimbia nje kuomba msaada.
1 307
Baba yake ana ndoto ya kuwa Rais wa jamhuri ya muungano wa TANZANIA 🇹🇿..Mtaje kama wamjua mimi nasoma comments 👇🙇🙈
1 307
Huyu ndiye rubani aliyerusha ndege iliyobeba mwili wa Rais Magufuli. Anaitwa Anna Tusajigwe Mwakasege. Ni binti wa pili wa baba Christopher na mama Diana Mwakasege.
Anna alipata maono ya kuwa rubani akiwa darasa la 3 tu. Baba yake akampeleka uwanja wa ndege angalau kuona ndege "live" badala tu ya kuziona angani tu. Alipofika darasa la 5 baba yake alitembeza uwanja mdogo wa ndege Arusha ambapo alipata nafasi ya kuongea na marubani kuhusu ndoto yake, nao wakampa ushauri masomo ya kusoma ili aweze kuifikia ndoto hiyo.
Alijifunza urubani Afrika kusini, na siku anarusha ndege kwa mara ya kwanza baba yake hakulala usiku huo (hii ni story ya wakati mwingine).
Lakini kwa sasa Anna ni miongoni mwa marubani wa shirika la ndege ATCL. Kabla ya kujiunga na ATCL alifanya kazi mashirika mengine makubwa ya ndwge kama SAA na kupata uzoefu wa kuendesha ndege kubwa kama Boeing 747, Boeing 777 na Airbus A340.
Hongera Anna kwa kuaminiwa kuendesha ndege iliyobeba mwili wa Rais. Umeweka alama kubwa kwa taifa hili, ambayo haitafutika kirahisi. Mara zote tutakapokumbuka kifo cha JPM tutakumbuka kuwa wewe na rubani mwenzio msaidizi (First officer) ndio mlipata neema ya kubeba mwili wake.
Najua si kazi rahisi kuendesha ndege ukiwa na majonzi ya kumpoteza Rais wako lakini umeaminiwa na umeweza. Tunakuombea kwa safari ya Zanzibar na baadae Mwanza na Chato. Wewe pamoja na team yako yote (cabin crew). Hakika wanawake mnaweza. #TheFutureIsFemale #GenderEmpowerment
MALISA GJ
1 307
#TotalEnergiesCAFCL | leo Simba Sc chini ya mwalimu Abdelhak Benchikha watakuwa na kibarua dhidi ya Wydad Kutoka pale Morocco.
Mchezo huu utapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam saa 10:00 jioni,Macho na akili za wapenzi wa Simba kwenye mchezo huu ni Kuhakikisha wanapata matokeo chanya ambayo yatawasogeza mahali katika kundi ambalo mpaka sasa wana alama 2 tu baada ya michezo mitatu.
Huu ni mchezo wa tatu kwa Benchikha kama kocha mkuu kwenye michuano hii ambapo amecheza michezo miwili ugenini na amefanikiwa kuokota alama moja pekee kati ya alama sita.
Anarudi nyumbani kwenye lile eneo la kujidai kwa Simba,Jukumu kuu ni moja tu kuhakikisha Mnyama anaondoka na alama tatu ili kuisogeza timu kwenye hatua ya mtoano.
Katika michezo mitatu iliyopita Wydad kashinda mbili na Simba kashinda mchezo mmoja tu baina yao,Hawajawahi kutoka sare hawa vitambaa huwa havitoshi wakikutana.
Kila la kheri Simba Sc
UNASUBIRI NINI CHAT NA MAFANS KIBAO LINK:-https://t.me/joinchat/QZcUBeMotA8wMmNk
1 307
KUTOKA MITANDAONI
Kwa habari zaidi SUBSCRIBE kupitia YOUTUBE channel yetu kwa ku bonyeza hapa chini.👇.kwenye link
https://youtube.com/@E-PlusMediaTv?si=JjehK80_nkzrHGNK
1 307
Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshiriki hafla ya utoaji tuzo za Rais kwa Wazalishaji bora usiku huu December 17,2023 Jijini Dar es salaam ambapo moja ya mambo aliyoyasema kwenye hotuba yake ni kwamba hadi kufikia miezi ya katikati mwakani 2024 malalamiko kuhusu umeme yatakuwa yamepungua kwakuwa vinu viwili vitawashwa katika Bwawa la Nyerere na kuongeza umeme kwenye gridi ya Taifa hivyo Nchi itakuwa na umeme wa kutosha.
“Itakapofika January mwakani tunaanza kuwasha kinu cha kwanza cha umeme pale kwenye Bwawa la Nyerere, jumla vinu vyote viko tisa, cha kwanza kitawaka January, cha pili hatutozidi April tutakuwa tumewasha kinu cha pili na vile viwili tukiwasha tutakuwa na umeme wa kutosha sana”
“Kwahiyo pamoja na jitihada nyingine za gesi, solar na mambo mengine lakini kwenye umeme wa maji ambao tunautegemea, nadhani katikati ya mwakani na ni malalamiko mengi (ya umeme) yatakuwa yamepungua, tutawasha vinu viwili tutaongeza kwenye gridi ya Taifa umeme mkubwa”
1 307
Nilikuwa napiga stori na Mwandishi kutoka Ukraine, nikamuuliza kwanini ni ghafla sana Shakhtar Donestk wameacha kumtumia Novatus Dismas kwenye kikosi cha kwanza? punde baada ya mabadiliko kwenye benchi la Ufundi ndipo Mtanzania amepoteza nafasi kwenye kikosi chao?
Mwandishi akaniambia sitaki kuamini kama ni issue ya uwezo ila kitendo cha Novatus kwenda hapo kwa mkopo akitokea Zulte naamini kuna hofu ya Shakhtar kuendelea kumtumia kwakuwa wanahisi wanaiweka relini biashara ya timu nyingine, Ulaya vitu vinaenda tofauti watu wanawaza pesa kwanza.
Football ya Ulaya ina vitu vingi sana ila cha kuchukua ni kuwa huwa ni Pure Business Mod Shakhtar wamejitambulisha kama Feeder Club wakiuza wachezaji si chini ya wanne kwa msimu, ukija kupiga hesabu za kawaida ni labda Novatus auzwe kwao jumla hapo inawezekana akaanza kuutwanga kwakuwa wao wana uhakika.
Wapo hatua za mtoano kwenye Europa League, huenda atapata nafasi Kijana.
[@jr_farhanjr]
LINK:-https://t.me/joinchat/QZcUBeMotA8wMmNk
1 307
"Nimeikuta timu haina mshikamano kwa wachezaji ila nimeshakaa nao na kulimaliza hilo, nina kikosi imara kwa hapo nyuma kilikosa vitu kadhaa ili kifanye vizuri naimani mechi zinazofuata tutafanya kitu bora kwa ajili ya Mashabiki wetu".
- Faouzi Benzarti, Kocha Mkuu wa Wydad AC Via LE Matin Médias.
UNASUBIRI NINI CHAT NA MAFANS KIBAO WANAOSUPPORT MPIRA KUHUSU MPIRA KWA KUJIUNGA HAPA KWENYE LINK:-https://t.me/joinchat/QZcUBeMotA8wMmNk
1 307
“Waliokuwa wakiwajeruhi wapinzani ni watu walioguswa na kazi nzuri ya Rais Magufuli, si Magufuli, hivyo kusema Rais Samia aombe msamaha kwa makosa yaliyotokea huko nyuma haiwezekani” Alfred Luvanda
Katika mahojiano yake na @chiefodembatz StarTV
1 307
Kama utakuwa umesahau au hufahamu basi Joseph Kibwetere aliwahi kuishangaza Afrika na Dunia kiujumla, yeye ni raia wa Uganda na alikuwa ni Mwalimu wa shule ya msingi.
Mara kadhaa alijiingiza katika harakati za siasa lakini akashindwa kuwashawishi Wananchi na kuuteka umma kwa sera zenye mashiko, hivyo akatafakari njia
nyingine ya kutoka akaona DINI itamlipa.
Kupitia kona hiyo gari la kibwetere likawaka, huko akawapumbaza watu kwa kujiita 'Nabii na Mtume'.
Akawateka kwa maneno matamu na yenye ushawishi huku akitumia vibaya vifungu vya maandiko MATAKATIFU.
Kwa msisitizo na sura isiyo na shaka aliwaahidi Waumini wake kuwapeleka peponi, lakini mwisho wao ukawa mbaya kwani aliwauwa kwa kumwaga Petroli na kuwachoma moto akiwaaminisha kwamba mwisho wa dunia umefika.
Tukio hili ni baya kuwahi kutokea Barani Afrika, kwani aliwapa watu imani iliyojaa udanganyifu na kuacha majonzi makubwa huku yeye ikidaiwa kuwa alijificha na baadaye kutoroka.
Mzee wetu Jakaya Mrisho Kikwete aliwahi kunena kuwa "akili za kuambiwa changanya na za kwako."
1 307
Khaled Mohammed Khaled .
Maarufu Kama Dj Khaled huyu ni mzaliwa wa new Orleans sema wazaz ni waamiaji tu .
Kiasili ni mpalestina tokea Ramallah uko west bank.alianza kufahamika Kama muuandaa vipindi redion I miaka ya 90 .
Baadae akawa producer maarufu Sana .
1 307
🚨 Muonekano wa sasa wa Lionel Messi baada ya kuanza mazoezi ya kujenga mwili wake Gym🏋️♂️ 💪
1 307
AFYA YA MR. IBU YAZIDI KUZOROTA, AKATWA MGUU
Familia ya muigizaji mkongwe wa Nigeria, John Okafor almaarufu Mr Ibu imejitokeza kufafanua kuhusu uvumi kwamba msanii huyo amekatwa miguu yake yote.
Familia hiyo imefutilia uvumi huo ikiweka wazi kuwa ni mguu mmoja tu wa muigizaji huyo ambao ulikatwa mwezi uliopita.
"Tunapenda kutoa shukurani zetu za dhati kwa Wanigeria na umma kwa ujumla kwa mchango wenu mkubwa, wa kimwili, kiroho na zaidi ya yote kifedha kwa kumfanya baba yetu John Okafor (Ibu) asimame," familia imesema katika taarifa.
Katika taarifa hiyo iliyoshirikiwa kwenye akaunti rasmi ya Instagram ya muigizaji huyo, familia hiyo ilithibitisha kwamba hata hivyo kulikuwa na kukatwa kwa mara ya pili kwenye mguu huohuo ambao ulikatwa mwezi uliopita.
"Tunataka kurekebisha madai potofu yanayoenea kwenye mitandao ya kijamii kuhusu hali ya sasa ya afya ya baba yetu. Kwanza tungependa kusema kwamba baba yetu hakukatwa miguu yote miwili bali mmoja tu. Kukatwa kwa mara ya kwanza hakukusahihisha kabisa hali yake ya kiafya kwa hivyo daktari alilazimika kwenda mbele kumkata mguu huohuo ili kuhakikisha hatumpotezi,” iliongeza taarifa hiyo.
Ikifafanua kuhusu ugonjwa wa muigizaji huyo, familia hiyo imesema chanzo cha ugonjwa wa baba yao siyo ugonjwa wa kisukari lakini alikuwa na damu iliyoganda mara kwa mara kwenye mguu wake (mishipa yenye ugonjwa) na changamoto nyingine za kiafya zilizohatarisha maisha yake.
Familia ilibainisha kuwa haijampeleka muigizaji huyo mkongwe nje ya nchi kwa matibabu zaidi kwani daktari amemtangaza kuwa hafai kusafirishwa kwa ndege.
1 307
"Bi Tuks usipige picha na Tanasha siku nyingine, namshauri awe anapiga picha na Zuchu king'ang'a tu. Ila Bi Tukioano atufundishe na sisi kuedit picha jamani, doh yani huyu tunaemuona Kenya sio yule wa Instagram jamani"- Mange Kimambi
