1 307
订阅者
+124 小时
-27 天
-1330 天
帖子存档
1 307
"Sio kwamba wanaume hawapendi kuhudumia wapenzi au wake zao, tatizo hali ya maisha imekuwa ngumu siwezi kulaumu. Siku hizi mambo yamebadilika kwenye mapenzi, wanawake ndio wanawalea wanaume"- Kungwi Mama Love
1 307
WAKILI AJITOLEA KUMSAIDIA MAMA ALIYEHUKUMIWA MIAKA 22 JELA BAADA YA KUKUTWA NA NYAMA YA SWALA.
Wakili Peter Kibatala amejitokeza kutaka kumsaidia mama aliyehukumiwa kifungo cha miaka 22 jela kwa kosa la kukutwa na nyama ya swala.
Hivi karibuni, Maria ngoda Mkazi wa mtaa wa Zizi la Ng'ombe Mkoa wa Iringa alihukumiwa kifungo cha miaka 22 jela na Hakimu Mkazi Said Mkasiwa wa mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Iringa baada ya kumkuta na hatia ya kukutwa na ndoo yenye vipande 12 vya nyama ya swala.
Nyama hiyo ya swala yenye vipande 12 ndani ilikuwa na thamani ya Tsh. laki tisa.
1 307
HALI YA KIAFYA YA TESA WA HUBA YAZUA MASWALI, APUKUTIKA GHAFLA.
Hali ya kiafya ya Mwigizaji Mkongwe wa Bongomovie nchini, Mwanamama Grace Mapunda maarufu kama Tesa kama anavyofahamika kwenye Tamthilia ya Huba imeendelea kuwashangaza wapenzi wa Tamthilia hiyo baada ya kuonekana amekonda ghafla huku uso wake ukipoteza nuru na mashamsham kama alivyokuwa awali.
Watu wa karibu wa msanii huyo wanasema ni kweli afya yake inaonekana kuwa siyo nzuri na hata wanapokuwa location kwa ajili ya ku-shoot amekuwa ni mtu wa kulala, hawezi kusimama kwa muda mrefu, hana tena mashamsham na wanasema anasumbuliwa zaidi na ugonjwa wa kisukari.
Na ikawe kheri Afya yake🙏.
1 307
MWIGULU NCHEMBA NDIO "MR CLEAN" WA KIZAZI CHETU.
Uongozi hupimwa kwa mambo mengi sana lakini kipimo cha juu zaidi kwa mujibu wa Carol S. Pearson, Mwandishi nguli wa masuala ya uongozi ni kipimo kitokanacho na uhalali wa kimaadili. Kwake yeye maadili ni nguzo mama katika kupima uwezo wa kiuongozi wa mtu yeyote katika utumishi wa Umma.
Bunge lipo katika vikao vinavyojadili taarifa tatu muhimu za kiukaguzi. Kwanza taarifa ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG, taarifa ya Kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali PAC, sambamba na kamati tatu za Bunge za Hesabu za Serikali za Mitaa LAAC, PAC na PIC. Kitu kimoja kimevuta na kinavutia macho ya wachambuzi wengi wa masuala ya uchumi na siasa na hiki ni moja wapo.
"HAKUNA MAHALA MWIGULU KATIKA TAARIFA ZOTE TATU ANATAJWA KUHUSIKA NA UPOTEVU HATA WA SENTI MOJA YA UMMA"
Taarifa za CAG ni moja ya taarifa muhimu sana katika kutengeneza uhalali wa kimaadili katika utumishi wa Umma wa ngazi ya juu kama Uwaziri, na kwavyovyote vile taarifa hii inapokupa uhalali au usafi kumaanisha kwamba imekupa utakaso na usafi maana maana ndio kipimo cha juu kabisa cha ukaguzi na uwajibikaji katika fedha za Umma. Hizi taarifa zote tatu za CAG kupita bila kumtaja popote si tu zinampa Mwigulu Nchemba positive impressions katika siasa zake, lakini zaidi zinampa ubatizo halali wa kuitwa jina jipya la "Mr Clean".
Mwigulu anasifika kwa uzalendo wake, kuwahurumia wanyonge na kusukuma maendeleo na kwa miaka yote hiyo ndiyo imekuwa sifa inayomtofautisha na wanasiasa wengi sana nchini. Kwa watu wenye kufuatilia masuala ya siasa ni mara chache sana ripoti hizi zimekuwa zikipita bila kuwataja baadhi ya mawaziri kuhusika na upotevu au ubadhilifu wa fedha za Umma, kikombe ambacho mwigulu naona amekiepuka na kujipa uhalali wa kuitwa "Mr Clean".
SWALI kuu kwa sasa ni Je! Mwigulu Nchemba ndio Mr Clean wa kizazi chetu kufuatia kupata uhalali wa usafi na taarifa zote za kikaguzi?
1 307
MARK ZUCKERBERG AVUNJIKA GOTI
Mmiliki Meta (Instagram, Facebook & WhatsApp), Mark Zuckerberg amekutana na shuruba ya kuvunjika goti wakati akifanya mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na pambano la ushindani la mchezo wa MMA.
Mark ambaye kwa siku za hivi karibuni ameonekana akijihusisha zaidi na mchezo huo ameshare picha akiwa hospitali na kueleza kuwa tayari ameshafanyiwa upasuaji wa jeraha hilo.
1 307
Klabu ya Yanga imetangaza kifo cha baba mzazi wa Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo, Andre Mtine aitwaye Tom Mtine.
"Kwa niaba ya Wanachama, mashabiki na wapenzi wa Yanga, uongozi unatoa pole kwa Mtendaji Mkuu wetu, Andre Mtine na familia yake, ndugu jamaa na marafiki kwa msiba huo mzito na klabu iko pamoja naye katika kipindi hiki cha majonzi," imeeleza taarifa ya Yanga.
1 307
Walimu Wakuu wawili wa Shule za Msingi Mlimani na Tunduma TC zilizopo Halmashauri ya Mji Tunduma Mkoani Songwe ambao walivuliwa vyeo kutokana na video iliyosambaa mitandaoni ikionesha Wanafunzi wakicheza wimbo wa Msanii Zuchu wa Honey, wamerejeshwa kwenye nafasi zao.
Spika wa Bunge laJamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt, Tulia Ackson akiwa Bungeni jana Novemba 6, 2023 aliishauri Serikali kuwarejesha kazini Walimu hao, na Waziri wa Elimu Prof. Adolf Mkenda akatoa maagizo warejeshwe.
1 307
''Kufikia saa saba mchana leo(jana), Baba yangu amefanyiwa upasuaji mara 7 hata hivyo ili kuokoa maisha yake na kuongeza uwezekano wake kupona, ilibidi mguu wake mmoja ukatwe.”
Mchekeshaji nguli raia wa Nigeria Mr IBU amelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi baada ya kufanyiwa upasuaji mara 7 na kukatwa mguu wake.
Mr IBU alianza kuugua tangu mwezi Oktoba na ameonekana katika video moja akiwa amelazwa hospitalini, akiomba msaada wa kifedha.
Ugua pole Mr IBU. Je ni filamu gani unaikubali kutoka kwake?
Cc: bbcswahili
1 307
#HABARI Serikali imewataka wamiliki wote wa majengo wenye changamoto za ulipaji kodi ya majengo kupitia ununuzi wa umeme ikiwa ni pamoja na uwepo wa mita zaidi ya moja katika jengo, wafike katika Ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) iliyokaribu nao kwa ajili ya kufanya maboresho ya taarifa zao.
Rai hiyo imetolewa bungeni jijini Dodoma na Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), wakati akijibu swali la Mbunge wa Nyamagana, Mhe. Stanslaus Shing'oma Mabula, aliyetaka kujua mpango wa Serikali wa kutenganisha malipo ya majengo kwa nyumba yenye zaidi ya mita moja ya umeme.
“Serikali imeendelea kuboresha ukusanyaji wa mapato kupitia mfumo wa luku kwa nyumba zenye mita zaidi ya moja kwa kuhakikisha inalipiwa mita moja pekee”, alieleza Dkt. Nchemba.
Dkt. Nchemba alisema kuwa inapobainika majengo mawili au zaidi yanatumia mita moja, Serikali imekuwa ikifanya maboresho ya ukusanyaji wa mapato kwa kutoza kiasi kinachopaswa kulipwa kwa kila jengo kwa mita iliyopo, lengo la hatua hiyo ni kuhakikisha msingi wa utozaji wa kodi ya majengo unazingatiwa.
1 307
NI USEMI UPI UMEKUKAMATA?:
1. "Kuzaliwa masikini siyo kosa lako,ila kufa masikini ni ujinga wako." ~ Bill Gate
2. "Kushindwa kupanga ni kupanga kushindwa." ~ Felix Bundala
3. "Heri kufa na mawazo yanayoishi, kuliko kuishi na Mawazo yaliyokufa." ~ Che Guevara
4. "Vita inamalizwa kwa vita na ili tuachane na matumizi ya bunduki inabidi itumike bunduki." ~ Mao ze Dong
5. "Sitamani kumjua babu yangu alikuwa nani, ninachotaka kumfahamu mjukuu wake atakuwa na tabia gani." ~ Martin Luther King
6. "Usimuulize mtu yoyote anayenijua mimi maana utamjua yeye kupitia mimi." Joe Lescot
7. "Muonekano siku zote hutengeneza uwezekano." ~ Lucky Crackent
8. "Hatuwapendi wanawake kwa sababu ni wazuri, ila tunawaona wazuri kwa sababu tunawapenda." ~ Luck Crackent
9. "Watu ni wengi ila binadamu ni wachache." ~ Fidel Castro
10. "Usiishi kwa sababu unaishi, tafuta sababu ya wewe kuishi." ~ Jay Ozil Cazorla Wilshere
11. "Hakuna mkate mgumu mbele ya chai." ~ Bob Sydou
12. "Kichwa kikubwa bila Akili ni Adhabu kwa miguu." ~ Thabiti Kube..
1 307
Waziri Mkuu wa Palestina Mohammad Shtayyeh jana alionekana akilia kwa uchungu kwenye Baraza la Mawaziri wakati akielezea hadithi ya mama mmoja ambaye watoto wake walizikwa chini ya kifusi huko Gaza.
Bw.Shtayyeh (65) alipata shida kuongea wakati akieleza jinsi watoto wanavyojiandika majina kwenye miili yao ili maiti zao ziweze kutambulika.
Waziri Mkuu huyo alijawa na hisia, na kunyamaza kwa muda kabla hajaendelea kuongea na kusema ”rehema iwe juu ya roho za mashahidi na aibu kwa wahalifu.”
Mgogoro kati ya Israel ina Hamas sasa umeingia katika wiki yake ya tano baada ya waasi wa Hamas kufanya shambulio la ghafla mnamo Oktoba 7.
Wizara ya Afya iliyopo Gaza imetangaza kuwa hada sasa watu zaidi ya 10,000 wameuawa, wengi wao wakiwa ni wanawake na watoto.
Wakati huohuo, Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu amesema kuwa nchi yake itakuwa na jukumu la jumla la usalama huko Gaza kwa muda usiojulikana.
1 307
Kulikuwa na maandamano makubwa ya kuunga mkono Palestina huko Washington D.C. jana. Makumi kwa maelfu waliandamana kutoka Freedom Plaza hadi Ikulu ya White House kulaani mauaji ya kimbari ya Israel dhidi ya Wapalestina huko Gaza
1 307
KWANINI GAZA YOTE, KWANINI SASA?
Mgogoro wa Israel na Palestina umedumu kwa zaidi ya miaka 70 sasa.
Mara zote umekuwa ukisababisha machafuko makubwa yanayogharimu maisha ya watu, mamia kwa maelfu.
Safari hii kama safari nyingine huko nyuma, hali imechafuka tena, na maelfu ya watu wanaendelea kuuawa.
Bila shaka utakuwa umesikia sababu kadhaa za asili ya mgogoro huu; dini, siasa nk.
Lakini tofauti na mara zote machafuko yanapotokea, safari hii kuna sababu nyingine imeongezeka ambayo ni ya kiuchumi.
Kuna kitu kinaitwa mfereji wa Suez, yaani ni kama mto wa kutengeneza, unaounganisha bahari mbili za Sham na Mediterranea.
Bahari hizi ndiyo kiungo kikuyu kati ya bara la Ulaya na Mashariki ya Kati.
Mfereji huu ulijengwa na wakoloni wa kiingereza kati ya 1859 hadi 1869 ili kurahisisha usafiri wa majini kutoka Asia kwenda Ulaya.
Mwaka 1956 baada ya uhuru, Misri ikautafisha mfereji huu na kuufanya kuwa mali ya Misri.
Mfereji huu ni muhimu sana katika uchumi wa dunia kwa ujumla kwani unachangia asilimia 12 ya pato la dunia.
Asilimia 10 ya mafuta yanayosafirishwa duniani yanapita kwenye mfereji huu.
Mwaka 2022, Misri iliingiza kiasi cha Dola bilioni 22 kama ushuru wa kuitumia mfereji huu.
Kutokana na ongezeko kubwa la mahitaji, mfereji huu kwa sasa unaonekana mdogo.
Kwanza hauruhusu meli mbili kupishana njiani, ni hadi moja ifike upande wa pili ndiyo nyingine ije, na safari moja inachukua hadi saa sita.
Kiuchumi hii inagharimu muda na pesa. Mbaya zaidi mwaka 2021.meli moja ilipata hitilafu na kuziba njia.
Ikasababisha meli nyingine zilizunguke bara la Afrika (angalia ramani ya pili) ili kutoka upande mmoja kwenda mwingine.
Siku moja tu ya kadhia kama hii husabanisha hasara ya zaidi ya dola bilioni 9.6.
Wizara ya ulinzi ya Marekani, Pentagon, ilisema kadhia ile ilileta madhara makubwa sana kwenye jeshi la nchi hiyo.
Kutokana na hilo, mataifa makubwa ya Marekani, Uingereza na Ufaransa yameamua kujenga mfereji mwingine unaoitwa Ben Gurion kupitia nchi ya Israel.
Lakini mfereji huu ili utokee bahari ya Sham, inabidi upite Gaza.
Kwa hiyo Israel na washirika wake wanataka kuichukua Gaza moja kwa moja ili wapate kutekeleza mpango huu.
1 307
HASARA YA VITA! Chaguo hili la picha laonyesha mamia ya magari yaliyochomeka yakiwa yamerundikwa nje ya mji wa Netivot, Israel ya kusini. Ni baadhi ya magari yaliyoharibiwa kwenye shambulio la kushtusha ambalo lilitekelezwa na wanamgambo wa Hamas nchini Israel mnamo Oktoba 7.
