1 307
订阅者
+124 小时
-27 天
-1330 天
帖子存档
1 307
Hawa ndio Watanzania waliochukuliwa mateka na Hamas. Ni Clemence Felix Mtenga and Joshua Loitu Mollel. Tarehe 7 October Hamas walivamia maeneo ya miji na vijiji huko Israel na kuuwa watu 1400 na kuchukua wengine 260 kama mateka wakiwemo hawa Watanzania waliokuwa masomoni nchini Israel. Mpaka sasa Hamas imeachia mateka wanne tu..Taarifa katika Ukurusa wa Twitter wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Israel imesema Watanzania hao wanashikilia na Hamas huko Gaza.
Tuwaombee wenzetu huko waliko warudi salama..!
1 307
Joshua Loitu Mollel, kijana kutoka Morogoro, Tanzania, aliianzisha safari yake kwenda Israel tarehe 18/9/2023, kuendeleza ndoto yake ya kujifunza Kilimo katika Shamba la Nachal Oz Holdings, Chuo cha IBIM. Alifika Israel salama na kuungana na jamii ya Nahal Oz, iliyopo karibu na mpaka wa Gaza, ili kujifunza kilimo, kwa manufaa ya Taifa la Tanzania.
Hata hivyo; tangu tarehe 07/10/2023 lilipotokea shambulio la kwanza la Hamas, Joshua hapatikani hewani wala kwa njia yoyote ile. Jiihada za familia kupitia ubalozi wa Tanzania nchini Israel za kumtafuta hazijazaa matunda.
Familia na wapendwa wa Joshua wanahuzunika sana kutopatikana kwake na wanahofia usalama wake. Hawajui nini hasa kimempata ndugu yao na hivyo tunaomba kila mmoja wetu amuweke Joshua kwenye sala na dua na maombi.
Ikiwa una habari yoyote kuhusu mahali au hali ya Joshua, tafadhali wasiliana nasi kwa simu +255768648844 Jina: Loitu Mollel (baba mzazi wa Joshua) AU +97253-303-7359 Balozi Alex KALLUA. Tusimame pamoja, tukivuka mipaka ya mila, tamaduni, na imani, ili kuhakikisha Joshua na Watanzania wengine waliopo Israel wanarudi salama. #Joshualoitu #MgogoroWaIsraelNaGaza #TuombeNaJoshua
1 307
“Kiongozi wa dini amefungua kanisa bila kibali adhabu yake miaka mitatu (3) jela, mtu amefungua baa bila kibali adhabu yake ni kufungiwa hio baa mpaka atakapopata kibali” Mhe. Godbless Lema Mwenyekiti wa CHADEMA kanda ya kaskazini.
1 307
"Ukweli wa mtoto wa Hamissa Mobetto na Diamond wazazi wenyewe wanajua, walishaenda mpaka kwenye ustawi wakaenda kupima DNA na ukweli ulionyesha kwamba mtoto sio wa Diamond"- Juma Lokole
1 307
Mtangazaji maarufu nchini Jamhuri ya Czech, Kamil Bartoshek @kazma_kazmitch alifanya balaa baada ya kusababisha mvua ya pesa Kwa Mashabiki zake kwa kumwaga kiasi cha Pesa Dola Milioni 1 sawa na Pesa za Tanzania Bilioni 2.5 kwa kutumia Helikopta kwenye umati mkubwa wa watu kama zawadi kwa walioshiriki katika shindano aliloandaa.
Bartoshek aliwaalika washiriki wote kukusanyika kwenye Uwanja mkubwa na kisha kumwaga pesa hizo Kwa Kutumia Helicopter ambapo kila mmoja akawa anazigombea
Unadhani Msanii Gani Bongo anaweza kufanya Kitu kama Hichi 🤔
1 307
WASIFU WA LENGAI OLE SABAYA
Lengai Ole Sabaya amezaliwa Tarehe 26/12/1986 mkoani Arusha. Amesoma Shahada ya Sayansi katika Elimu Chuo Kikuu cha Mtakatifu John Dodoma (St. John University).
Ole Sabaya aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana CCM (UVCCM) Mkoa wa Arusha na pia aliwahi kushika wadhifa wa Udiwani katika kata ya Sambasha Wilaya ya Arumeru mwaka 2015.
Ole Sabaya aliteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro tarehe 28 Julai 2018 ya aliyekuwa Rais wa Tanzania awamu ya tano, Hayati John Pombe Magufuli.
Sabaya alitenguliwa nafasi hiyo ya ukuu wa Wilaya ya Hai tarehe 13 Mei 2021 na Rais Samia Suluhu Hassan ili kupisha uchunguzi wa makosa yaliyokuwa yakimkabili ikiwemo unyang’anyi wa kutumia silaha na Baadae aliachiwa huru Baada ya kukutwa Hana Hatia.
