1 307
订阅者
+124 小时
-27 天
-1330 天
帖子存档
1 307
🚨 Benjamin Mendy (29) anaipeleka Man City kwenye mahakama ya ajira akiwadai £10M (Tshs Bilioni 31) kama malimbikizo ya mshahara wake wa miaka miwili.
Klabu hiyo iliacha kumlipa mishahara yake alipokamatwa kutokana na tuhuma za ubakaji.
Kwasasa Mendy anakipiga katika klabu ya Lorient ya nchini kwao Ufaransa 🇫🇷
(Chanzo: BBC Sport)
1 307
FIFA italazimika kuilipa Barcelona 🇪🇸 fidia ya euro 20,548 (Tshs Milioni 56+) kila siku ambayo Gavi atakuwa nje ya uwanja tangu alipoumia akiwa kwenye majukumu ya kimataifa.
Malipo yataanza siku 28 baada ya mchezaji huyo kupata jeraha na yanaweza kudumu kwa muda usiozidi mwaka mmoja.
Kwa mujibu wa sheria za FIFA, vilabu vitapokea fidia iwapo mchezaji ataumia akiwa kwenye majukumu ya timu ya taifa na kukaa nje ya uwanja kwa zaidi ya siku 28. Barcelona, kwa hivyo, itaanza kulipwa mnamo Desemba 16.
Gavi anatarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa miezi 7-9 akiuguza majeraha yake.
Katika kipindi hicho Barca, wanaweza kuvuna kiasi cha €4,315,080 sawa na Tshs Bilioni 11.83
1 307
Kijana mmoja wa Jijini Arusha maarufu kwa jina la Ally Dangote ambaye kwenye siku za karibuni amekuwa akisakwa hadi picha zake kubandikwa kwenye mitaa mbalimbali kutokana na tuhuma za kuchoma Watu 15 visu, kuua Watatu huku akiwa anavalia hijabu ili kujificha, amefariki dunia leo baada ya kudaiwa kujirusha kutoka kwenye gari la Polisi wakati akiwapeleka Polisi kwenda kuwafichua Wahalifu wenzake.
Mamia ya Watu walifurika leo nje ya chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Mount Meru Arusha wakitaka kushuhudia kama ni kweli Kijana huyo amefariki kwani amekua tishio kwa Wakazi wengi hasa kutokana na mfululizo wa matukio yake ya kutisha ikiwemo kuwabaka Wanawake.
“Sijaamini kama amekufa ndio maana nimeshikilia jiwe tunaweza kufanya mzaha ukakuta tu kazimia..... nimejihadhari na jiwe” amenukuliwa akiongea Mwanamke mmoja aliyejitambulisha kama Mama Chuda ( picha ya pili ). #MillardAyoUPDATES.
1 307
Rasalynn Carter amefariki dunia nyumbani kwake na familia imethibitisha huku familia ikieleza kuwa amefariki katika makazi yao Geogia.
Ijumaa mwishoni mwa wiki taarifa ziliambaa kuzidiwa kwa mama huyo ambaye amekuwa akiugua tangu Februari mwaka huu, hivyo kuwekwa chini ya uangalizi nyumbani kwake.
Julai mwaka huu Rosalyn aliadhimisha miaka 77 ya ndoa yake na mumewe, Carter.
“Alikuwa mwakamke ambaye akinisaidia na kunitia moyo kila nilipohitaji kwa kipindi chaote cha uhai wake nilijua kwamba ainipenda na alikuwa akijali,” amesema Carter.
1 307
"Watu wengi wanatamani mimi na Femi tuwe wapenzi kweli, karibia watu wote wanaoiangalia Tamthilia ya Juakali wanatamani siku moja iwe hivyo na hata wengine wanaamini kama tayari sisi ni mtu na mpenziwe"
"Ukweli ni kwamba mimi nina mahusiano yangu na yeye ana mahusiano yake na tunapokuwa nje ya kazi kila mtu anayaheshimu mahusiano ya mwenzake, japokuwa kama wakisema nimchague mrembo mmoja wa kuwa nae kwenye mahusiano kutokea kwenye Tamthilia ya Juakali moja kwa moja nitaenda kwa Femi kwasababu namuelewa kiasi"- Isarito, Luka wa Juakali
1 307
SINGLE MOTHER
"Tulikutana Gongo la Mboto na baba mtoto huyu alikuwa anafanya kazi kampuni ya Hygen walikuwa wanajenga nyumba za wanajeshi sasa hizo nyumba zimekwisha, aliondoka hapa Tanzania baada ya kibali chake kuisha, wakati anaondoka nilikuwa na imani kuwa hata mimi atanikumbuka lakini mpaka sasa hivi hakuna mawasiliano wala jambo lolote linaloendelea, huyu mtoto saizi ana miaka miwili na miezi mitatu, kipindi napata ujauzito mpaka najifungua alikuwa ananitunza vizuri tu ila alipoondoka tu ndiyo sina mawasiliano naye " Safina Mohamed
Una mshauri nini huyu dada Safina kwa hili.
1 307
Siku kadhaa zilizopita Msanii Snoop Dogg aliushangaza ulimwengu wa mitandao ya kijamii kwa muda, baada ya kutangaza kuwa ameachana na uvutaji (wengi wakiamini ameacha uvutaji wa bangi), jioni ya leo Snoop amerudi kivingine tena!.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram ameachia video za Tangazo na kampuni ya majiko yasiyotoa moshi #solostove na kuinadi kampuni hiyo tofauti na watu wengi walivyokuwa wamepokea awali.
Hii inakua mara ya pili kwa msanii huyo kutangaza kuachana uvutaji na kisha anarudi na tangazo. Kifupi Anko Snoop ametupiga chenga ya mwili!😀.
Je, ni msanii gani hapa bongo mwenye sifa za kupindua pindua mambo kama mtaalamu Anko Snoop?😀 Mtaje kwenye comment 👇
1 307
PICHA: Mwanamke aliyejitambulisha kwa jina la Mama Chuda akiwa ameshika jiwe kubwa nje ya chumba cha kuhifadhia maiti Hospitali ya Mount Meru Jijini Arusha ili kujihami iwapo Kijana aitwae Ally Dangote ataamka kutoka ndani ya chumba hicho.
“Sijaamini kama amekufa ndio maana nimeshikilia jiwe tunaweza kufanya mzaha ukakuta tu kazimia, nimejihadhari na jiwe” ———amenukuliwa akiongea Mama Chuda.
Marehemu Ally Dangote alikua akituhumiwa kwa wizi, ubakaji na mauaji huku akidiwa kufanya hayo yote akiwa anajiziba sura kwa kutumia vazi la hijabu ambapo hadi anafariki inadaiwa alikua amechoma visu Watu 15 na kuua Watu watatu Jijini Arusha.
Kaimu Kamanda wa Polisi Arusha Salvas Makweli ameithibitishia AyoTV leo na kusema kuwa kifo cha Ally kilitokana na kujirusha kwenye gari la Polisi kwenye safari ya kwenda kuwaonesha Polisi makazi ya Wahalifu wenzake. #MillardAyoUPDATES
1 307
Msanii @isarito_tmt amewaomba mashabiki kuacha Tabia ya kumfananishana Marehemu Kanumba kwa sababu sio sawa ni Bora kumshindanishana waliopo
1 307
HISPANIA: Nyota wa Muziki wa Pop na Raia wa #Colombia, #Shakira amefikia makubaliano na Waendesha Mashtaka wa kumaliza Shauri la kukwepa Kodi kwa kulipa Euro Milioni 7.5 (Tsh. Bilioni 20.4) kabla kesi ya msingi haijaanza kisikilizwa
Awali, Shakira alitakiwa achague kulipa kiwango hicho ili mambo yaishe au Shauri liende Mahakamani na akishindwa kesi kuna kifungo cha Miaka 8 jela na Faini ya Euro 23.8m (Tsh. Bilioni 65), akachagua Mahakamani kabla ya kubadili mawazo baadaye
Shauri la Msingi lilikuwa kukwepa Kodi ya Euro Milioni 14.5 (Tsh. Bilioni 39.4) lililowasilishwa Mahakama ya Barcelona
1 307
MC GARAB NA MKE WAKE WAADHIMISHA MIAKA 7 YA NDOA YAO
Ikumbukwe pia wamejaliwa kupata watoto watano
Mungu azidi kuwabariki ❤️❤️
1 307
Kwa sasa stori kubwa mjini Twitter (X) ni Kampeni ya kushinikiza mamlaka husika kumshawishi Mshambuliaji wa Bodø/Glimt, Amahl William D'vaz Pellegrino aje kuitumikia timu ya taifa ya Tanzania.
Mshambuliaji huyo mzaliwa wa jijini Drammen nchini Norway na wazazi wenye asili ya Tanzania amekuwa tegemeo kunako klabu hiyo ya Norway ambapi tangu amejiunga nao mwaka 2021 amecheza michezo 69 na kufanikiwa kufunga mabao 54.
Licha ya Amhl kuwa na umri wa miaka 33 kwa sasa wanaharakati hao mjini X wanaamini kuwa umri ni namba tu na kijana anastahili kuja kuipa nguvu timu ya taifa lake la asili ikiwa zimesalia siku chache kabla ya fainali za kombe la mataifa ya Afrika na wakati huu ambapo mamlaka zinajitahidi kuhakikisha wale wote wenye chembechembe za taifa la Tanzania wanakuja kuongeda nguvu kwenye timu ya taifa ya Tanzania.
Kampeni hii imeonekana kuungwa mkono na watu wa kutoka nyanja mbalimbali kama vile waandishi wa habari ,wanasiasa na wengineo ambao wanaamini ongezeko la wachezaji wanaocheza maeneo mbalimbali duniani wataongeza na kuleta mafanikio kwa timu ya taifa.
1 307
ODAMA, JOHARI NA GERTRUDE MWITA WANG'ARA NA TUZO ZA ZIKOMO.
Wasanii Johari Chagula, Jenifer Kyaka "Odama" na Getrude Mwita "Kibibi" wamejishindia tuzo usiku wa kuamkia jana nchini Zambia (Zikomo Awards 2023)
Getrude Mwita "Kibibi" ameshinda tuzo kipendele cha Msanii bora wa mwaka wa kike Afrika Mashariki.
Jenifer Kyaka "Odama" yeye ameondoka na Tuzo ya Tamthilia bora ya mwaka Afrika huku Tamthilia yake ya (Fungu langu) ikichukua Tuzo hiyo.
Lakini pia Johari yeye ameibuka na Tuzo ya Msanii bora wa kike wa mwaka.
Wasanii hao wametua nchini Tanzania siku ya jana na wote kwa pamoja wameonyesha kuzifurahia tuzo hizo kila mmoja kwa nafasi yake.
1 307
WE MTOTO UTAKUJA KUNITOA ROHO MIE ; HAJJI MANARA
"Zai weee utakuja kunitoa roho shomvi mie, mwenzako mimi dhaifu na hizi rangi za Peponi. Au umetumwa na makolo nini?"- Hajji Manara kwa Zaiylissa
Wawili hao wanadaiwa kuwa wapenzi kwa muda wa wiki mbili sasa.
