1 307
订阅者
+124 小时
-27 天
-1330 天
帖子存档
1 307
"Ni aibu kuona vijana hawafanyi kazi, wanawaza pombe tu "- Waziri George Simbachawene
1 307
Nchi zenye bei ya chini kabisa ya Diesel kwa mwezi Juni 2024.
Top countries with cheapest diesel (June 2024)
1 307
Polisi wa Kenya walinda nje ya ubalozi wa Marekani nchini Haiti ulioko mjini Port-au-Prince. Wakati huo huo, majambazi wenye silaha wanaendelea kufanya uharibifu katika maeneo mengi ya Haiti.
1 307
+5
KUTOKA MITANDAONI
Zaidi follow ukurasa wetu wa instagram hapa kwenye link👇👇
https://www.instagram.com/e_plus_media?igsh=YW40cmNtdXV0OWZ2
1 307
Tazama Hapa Picha Ikimuonesha Msanii wa WCB Wasafi Zuchu Akilia Machozi ya Furaha Kwa Mara ya Kwaza Akisalimiana na Rais wa Tanzania Dr Magufuli.
Tazama Hapo Kisha Weka Comment Yako Hapa Tafadhali.
1 307
Mwanamke mmoja raia wa Nigeria amejikuta akimwaga machozi kwa uchungu baada ya kurejea nchini humo kutoka ughaibuni alipokuwa akifanya kazi na kubaini kaka yake alikuwa akimtapeli kwa kudhani alikuwa akimjengea nyumba kwa pesa alizokuwa akimtumia.
Mwanamke huyo ambaye amekuwa akimtumia kaka yake pesa kwa takribani miaka 15 alipatwa na mshtuko mkubwa baada ya kujua pesa alizokuwa akituma zimeelekezwa kwenye matumizi mengine na hakuna nyumba iliyojengwa.
Picha na video zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii zinamwonesha mwanamke huyo akijiviringisha kwenye tope huku akilia kwa uchungu kwa upotevu wa pesa zake.
Zaidi follow ukurasa wetu wa instagram hapa kwenye link👇👇
https://www.instagram.com/e_plus_media?igsh=YW40cmNtdXV0OWZ2
1 307
Nimejifunza kuwa ukijihusisha na wito wako tu utakuwa salama zaidi na mwenye mafanikio zaidi, pia Mimi nikiwa mtu ninayeamini kwenye malezi ya kiroho ninajua wazi kuwa mtu wangu wa Mungu ni sauti ya MUNGU kwangu na kwasababu anasema tusiwapige vita watumishi wa Mungu ndivyo Mimi ninafanya pia.
8. Wakati Bwana Yesu alipokuwa duniani katika mwili na hata wakati wa Mitume wa kwenye Biblia walikuwepo watumishi wa Mungu na hata viongozi wa kidini wengi tu na miongoni mwao wapo waliofanya makosa mbalimbali ila Bwana Yesu na Mitume wake hawakuwa busy kuwashambulia na kutaja majina yao kwenye mahubiri yao bali walizingatia kufundisha neno la kweli lenye kubadilisha maisha ya watu.
Mimi pia nimejifunza kuhubiri Injili ya kweli bila kujali nani anahubiri nini?.
9. Kama kwenye mahubiri yako au machapisho yako mtandaoni huwa unataja majina ya wahubiri na kuwasema kwa ubaya (haijalishi kama unachosema ni Cha ukweli au uongo) na unawaambia wasiende kwa mtumishi flani tena ukimtaja jina kabisa basi ujue unampigia kampeni huyo mtumishi wa Mungu na kwamba watu wengi zaidi wataenda kwake maana umewasaidia kujua juu ya uwepo wa huyo mtumishi au mhubiri.
Mimi nimechagua kutokufanya hivyo na kamwe sitojihusisha na biashara ya kutaja majina ya wahubiri kwa lengo la kuwachafua na kutaja mabaya yao ninapokuwa nahubiri.
10. Mwili wa Kristo umejaa wahubiri na wakristo wengi sana wenye mapungufu mno kwenye maeneo mbalimbali kama vile mafundisho, uombaji, tabia mbaya kama vile kudhulumu, matusi, uzinzi, ulevi n.k
Hivyo tunahitaji zaidi kuwafundisha watu wetu neno la Mungu ili wabadilike na sio kuangalia kwenye makanisa na huduma zingine ili kuzikosoa na kuwapiga vita (wahubiri wengi wanasahau kuwasaidia watu wao na badala yake wapo busy kushambulia makanisa mengine juu ya mabaya ambayo hata kwenye makanisa yao yapo).
Mimi nimechagua kutokuwa hivyo.
Sikuambii ufanye kama Mimi ila fanya kama Neno linavyosema na zaidi sana zingatia wito wako na kanisa lako achana na makanisa ya watu hasa yanayokukera utapata vidonda vya tumbo na BP kwasababu ya kupoteza muda mwingi ukiwaza mabaya dhidi ya huduma au mhubiri flani.
Ni Mimi nduguyo katika Kristo
Emmanuel D Chongela
1 307
Sababu kumi kwanini huwa siwapigi vita watumishi wa Mungu na sitokuja kumpiga vita mtumishi wa Mungu hata kamwa simwelewi au Kuna vitu sivikubali kwenye huduma yake.
1. Ni mtumishi wa Mungu na sio mtumishi wangu.
MUNGU ndiye anayewaita watu kwenye huduma (Calling) na kuwapa majukumu (assignment) ya kufanya kutokana na wito wao aliowaitia hivyo wanawajibika kwa Mungu na sio kwangu.
Mungu ndo anajua kama wanachokifanya ndicho alichowaambia kufanya au wametoka kwenye msitari, Mimi sikuwepo wakati wanaitwa wala sikuwepo wakati Mungu anawapaka mafuta kwaajili ya utumishi wao (I was not there when God anointed them) na pia Mungu hajanifanya kuwa kiranja mkuu kwenye mwili wa Kristo ili niwawajibishe watumishi wake na kamwe hakuna hiyo huduma kwenye mwili wa Kristo.
2. Watu wengi wanaowapinga watumishi wa Mungu wanafanya hivyo kwasababu ya wivu wao dhidi ya watumishi wa Mungu na chuki binafsi waliyonayo kutokana na kuona ukuaji katika huduma husika na si kwamba wanafanya hivyo kwasababu ya upendo (they are just doing it out of jealous and hatred rather than Love)
Hivyo siwezi kuwa miongoni mwa kundi hilo kwasababu Mungu amenipa kuwapenda watu wote bila kujali watu wengine wanasemaje kuwahusu.
3. Ninazingatia wito wangu binafsi na sio wito wa watu wengine, Kila mtu kwenye mwili wa Kristo amepewa wito wake na Kila mtu atawajibika mbele za Mungu kutokana na namna alivyotumia kile alichopewa.
Mimi ninazingatia wito wangu binafsi na kamwe sitopoteza muda wangu kujihusisha na wito wa mtu mwingine kwasababu Mungu hajaniitia kazi hiyo.
4. Kuna watu wa MUNGU ambao kwangu ni mababa kutokana na dimensions and levels zao katika ulimwengu wa roho na namna walivyotembea na MUNGU na zaidi sana Mungu bado anawatumia hata sasa hivyo sipo kwenye kiwango cha kupigana nao vita kwasababu Mungu hawezi kukubali waaibike au kuanguka kisa maneno yangu na harakati zangu za chuki dhidi yao na badala yake Mimi ndo nitapotea na kuwaacha wao kama nitajaribu kuwapiga vita (hauwezi kujitutumua kujaribu kumwangusha mtu aliyeujenga ufalme wa Mungu na anaujenga kuliko wewe ulivyofanya, hawa kwao huwa tunajifunza nasi kuwapiga vita).
5. Ikitokea Kuna Mtu wa Mungu simwelewi au simkubali either kutokana na mafundisho yake au mambo yanayofanyika kwenye huduma yake na Ibada zake au kauli zake na matendo yake mabaya au yenye chuki au pengine nimemsikia/kumwona akipiga vita huduma au watumishi wa Mungu ambao pengine ninawaheshimu kabisa, ninachokifanya Mimi huwa naacha mara moja kumfuatilia wala sitoenda kwenye Ibada yake au kusikiliza mafundisho yake na pia naweza hata kutokufuatilia mitandao yake ya kijamii kwasababu sitaki aendelee kunikwaza.
Sitompiga vita wala kuwaambia watu wasimsikilize ila Mimi binafsi sitomsikiliza na nimefanya hivyo kwa watumishi kadhaa ndani na nje ya nchi na imenifanya kutokuwa na chuki dhidi yao wala watu wanaowafuatilia.
6. Kuna nyakati nikiwa chuoni niliwahi kushuhudia vita dhidi ya huduma ambayo Mimi ni sehemu ya huduma hiyo (ni huduma ambapo tunaomba kwaajili ya chuo, vyuo, mwili wa Kristo na taifa la Tanzania (intercession) na pia tunajifunza na kufundishana kuhusu maombi na uhalisia wa Mkristo (Christian identity) nje ya misingi ya kiudhehebu na kidini kwasababu sisi tunahusisha wakristo kutoka madhehebu yote walio tayari kuomba), wapo watu walikuwa wakipambana kuiua huduma hii na kamwe hatukujaribu kupambana nao wala kuwachukia kwasababu tulijua ni utoto tu ndo ulikuwa unawasumbua na tunamshukuru MUNGU kwamba hawakufanikiwa.
Hii imenipa fundisho kubwa kuwa alichokianzisha MUNGU hakiwezi kuuliwa na mtu aliye nje na amejaa chuki zake na wivu wake na hivyo hata Mimi siwezi kujihusisha na kupambana dhidi ya kazi aliyoianzisha MUNGU.
7. Baba yangu wa kiroho pamoja na Baba yake wa kiroho Prophet Uebert Angel na Pastor Chris Oyakhilome huwa hawajihusishi na kuwapiga vita watumishi wa Mungu licha ya kwamba wao wenyewe wanapigwa sana vita na wamepigwa vita toka wanaanzisha huduma zao hivyo Mimi kama mtu ninayejifunza kwao nimechagua kuishi kama wao na kufanya kama wao nikizingatia wito wangu tu.
1 307
+9
KUTOKA MITANDAONI
Zaidi follow ukurasa wetu wa instagram hapa kwenye link👇👇
https://www.instagram.com/e_plus_media?igsh=YW40cmNtdXV0OWZ2
1 307
+9
KUTOKA MITANDAONI
Zaidi follow ukurasa wetu wa instagram hapa kwenye link👇👇
https://www.instagram.com/e_plus_media?igsh=YW40cmNtdXV0OWZ2
