1 307
订阅者
+124 小时
-27 天
-1330 天
帖子存档
1 307
Tarehe 2.12.2023 Mwanafunzi Glory Laurent wa Shule ya Msingi Karanga mjini Moshi, ambaye pia alikuwa Balozi wa Usalama Barabarani katika program yetu ya Junior Road Safety Ambasasador alifariki kwa Kugongwa na Bus la Shule baada ya kuanguka barabarani kutoka kwenye baiskeli aliyokuwa amepanda wakiekelea shuleni. Basikeli hiyo iliyumba baada ya kugongwa na bodaboda.
Jana tumeshiriki kumzika huko wilayani Rombo. Glory alikuwa mwanafunzi mwenye akili na aloyetegemewa na shule kufaulu katika mtihani wa Darasa la Saba. Ajali ni janga kubwa kwa watoto kati ya umri wa miaka 5 hadi vijana umri wa miaka 29. Pumzika kwa amani Glory, Mwenyezi Mungu akupokee kwenye nuru ya uso wake. Amina.
1 307
"Mimi ni mzuri ingawa maisha ndio magumu," ~Msanii Phina amesema yeye bado ni mzuri ila maisha ndio magumu tu!!
1 307
MAAFA HANANG | Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana (Mwenye shati la Kijani) akishiriki na wananchi, askari wa JWTZ na askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kutafuta miili ya iliyonasa katika tope lililotokana na mafuriko yaliyotokea wilayani Hanang kufuatia mvua kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia Disemba 3, 2023.
Kinana pia ametoa pole kwa baadhi ya majeruhi katika Hospitali ya wilaya hiyo (Tumaini) iliyopo Katesh, alipowatembelea waathirika wa mafuriko hayo katika baadhi ya vijiji vya wilaya hiyo.
#AzamTVUpdates
Imeandaliwa na Claud Mshana
1 307
KUTOKA MITANDAONI
Kwa habari zaidi SUBSCRIBE kupitia YOUTUBE channel yetu kwa ku bonyeza hapa chini.👇.kwenye link
https://youtube.com/@E-PlusMediaTv?si=JjehK80_nkzrHGNK
1 307
Miongoni mwa filamu zilizompa umaarufu Shahrukh Khan ni hii KOYLA ni movie yenye stori nzuri na song za hatar sana ilitoka mwaka 1997 humu ndani utamkuta Shahrukh Khan (Shanker) bibie Madhuri dixit (Gauri)Amrish Puri ,Johnny Lever na wengine, ndani ya movie hii unakumbuka kipande gani? ukumbuke Shahrukh Khan alilishwa kaa la moto na Amrish Puri akawa bubu hawezi kuongea!!
1 307
`🚨»| mapenzi hayajawahi kumuacha mtu salama.
"Kuna mwanamke niliwahi kumpenda ana akili sana lakini alikuja kunifanyia tendo ambalo nilikuja kuamini kwamba hakuna mwanamke yoyote mwenye akili.
Unajua kwanini nasema hamna akili? Nilimpenda, nilimwamini, nilikuwa na mkumbatia nilikuwa nafanya vitu ambavyo sijafundishwa kufanya, nafanya nilivyoona kwenye movie, naongeza ambavyo sijui nafanya nini lakini nilikuwa najua ana akili, najua ananipenda then nikimtumia meseji hajibu anajibu baadae hivyo tuishie hapo Love is crazy" -
🎙️ Chid Benz
Credit clouds fm
1 307
#TBC2UPDATES #2DIMBANI
Mtoto wa nyota wa mpira Phil Foden, Ronnie Foden maarufu kama "EL WEY" amesaini mkataba na Agency ya mitindo,ambalo ni dili nono akiwa katika umri mdogo.
El Wey, akaunti yake ya Instagram imefisha wafuasi milioni 3.8 kwa sasa na anatazamiwa kuingiza mpunga wa £10,000 sawa na TZS milioni 32 kwa kila project ya matangazo.
Mtoto @officialronniefoden_ amekuwa na umaarufu mkubwa kwenye mitandao ya kijamii tangu alipojiunga Uwanjani na baba yake [FODEN] kwenye sherehe za Man City baada ya klabu hiyo kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliopita wa mwaka 2022
Ronnie ameingia makubaliano na Propel Talent Group, kampuni inayosimamia maisha ya baadhi ya vipaji nchini Uingereza na tayari amepigia debe bidhaa mbalimbali za mitindo, huku mtoto huyo akiwa tayari amepigia picha kadhaa kwa ajili ya mradi huo mpya.
#TBC2YakijanjaZaidi
1 307
Kupitia Nisha kuna namna utagundua kwamba ndoa ina umuhimu mkubwa sana hasa kwa mastaa wetu wa Kibongo. Hajawahi kuwa na skendo mbaya lakini kabla hajaolewa kuna namna alikuwa mcharuko, ujibuji wake wa maswali kwenye interview na hata mara kadhaa tulimsikia akisema anatamani Ommy Dimpoz amuoe, tusimlaumu huenda alikuwa anajibusti ili aendelee kuongelewa.
Baada ya kuolewa na Mwanaume huyo pichani (kwenye picha ndogo) Nisha amebadilika kuanzia muonekano, na hata zile kashi-kashi za hapa na pale zimeisha kabisa, maisha yake ni ya siri sana. Alipoolewa na mwanaume huyo watu wengi walimbeza kwamba hajui kuchagua, sijui kafata pesa kwakuwa jamaa sio HB, lakini amewathibitishia watu kuwa kimfaacho mtu chake na ameamua kumzalia kabisa.
Nisha ni funzo kwa wasanii ambao umri wao umeenda lakini bado wanaendelea kudabuka kwa kujitoa fahamu.
1 307
BARUA KWA WANAFUNZI WENZANGU WA ZAMANI.
Wapendwa wanafunzi wenzangu,
Kwa unyenyekevu napenda kukuandikia barua hii kuwajulisha kuwa;
Baadhi yetu waliacha shule. Baadhi yetu walijiunga na vyuo vikuu. Baadhi yetu waliajiriwa. Baadhi yetu bado wanatafuta kazi. Baadhi yetu walisafiri nje ya nchi.
Baadhi yetu wamerudi kijijini. Baadhi yetu wako hospitalini. Baadhi yetu wamekufa. Baadhi yetu wapo gerezani. Baadhi yetu wameolewa na kuoa.
Baadhi yetu ni wajane. Baadhi yetu wapo single. Baadhi yetu walipata kichaa na wanatembea bila viatu barabarani.
Popote ulipo, ikiwa tutakutana katika ulimwengu huu, tafadhali uwe na huruma. Sio wote tunaishi maisha mazuri. Sio sote tulifanikiwa baada ya shule.
Haijalishi una shughuli nyingi kiasi gani, wakati mwingine tuangalie... Tupigie, tutume ujumbe.
Tutiane moyo,Tusaidiane,Kwa sababu tulianza safari pamoja, haimaanishi kwamba tulifika mahali pamoja.
Credit: Book_Joint
1 307
Kupitia Nisha kuna namna utagundua kwamba ndoa ina umuhimu mkubwa sana hasa kwa mastaa wetu wa Kibongo. Hajawahi kuwa na skendo mbaya lakini kabla hajaolewa kuna namna alikuwa mcharuko, ujibuji wake wa maswali kwenye interview na hata mara kadhaa tulimsikia akisema anatamani Ommy Dimpoz amuoe, tusimlaumu huenda alikuwa anajibusti ili aendelee kuongelewa.
Baada ya kuolewa na Mwanaume huyo pichani (kwenye picha ndogo) Nisha amebadilika kuanzia muonekano, na hata zile kashi-kashi za hapa na pale zimeisha kabisa, maisha yake ni ya siri sana. Alipoolewa na mwanaume huyo watu wengi walimbeza kwamba hajui kuchagua, sijui kafata pesa kwakuwa jamaa sio HB, lakini amewathibitishia watu kuwa kimfaacho mtu chake na ameamua kumzalia kabisa.
Nisha ni funzo kwa wasanii ambao umri wao umeenda lakini bado wanaendelea kudabuka kwa kujitoa fahamu.
1 307
Mapema leo Christina Shusho amepata Neema ya kutumbuiza katika kanisa maarufu Duniani la TB Joshua Ministies lililopo Lagos nchini Nigeria.
1 307
"Ukiwa mwema utasemwa
Ukiwa muovu utasemwa
Ukiwa mkimya utasemwa
Ukiwa msemaji utasemwa
Ukiwa hai utasemwa
Ukiwa maiti utasemwa
Sembuse mimi na wewe?"- Ommy Dimpoz
1 307
"Ili uwe masikini inabidi uwe haujafikia kiasi gani cha pesa au ukose nini?"- anauliza Idris Sultan
