1 307
订阅者
+124 小时
-27 天
-1330 天
帖子存档
1 307
Kiongozi wa Chama cha Upinzani nchini DRC, Corneille Nangaa anayeishi uhamishoni nchini Kenya ametangaza kuundwa kwa muungano wa kisiasa na kijeshi na waasi wa M23 pamoja na makundi mengine yenye silaha.
Hatua hiyo, imepelekea Serikali ya Congo kuionya Kenya kutokana na athari zinazoweza kujitokeza kwa kumruhusu Nangaa, ambaye alikuwa mwenyekiti wa tume ya uchaguzi ya Congo katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2018, kuishi nchini humo.
Katika matamshi yake, Kiongozi huyo wa upinzani alitoa wito wa muungano wa vikosi vyote vya kijeshi, kisiasa na kijamii ili kuijenga upya Serikali na kurejesha amani katika taifa hilo lililokumbwa na mapigano ya mara kwa mara hasa maeneo ya mashariki.
Nangaa alisema vikundi tisa vikijumuisha M23, tayari vimeungana naye kupitia muungano wake wa Congo River Alliance akisema unalenga kuleta moja na utulivu wa kitaifa ili kuondoa udhaifu wa Serikali ya Congo katika muda wa miongo mitatu na kushindwa kwake kudumisha usalama nchini kote.
1 307
Ni tukio lililoacha simanzi kwa familia, jamaa na mashabiki wa Mwanamuziki na mpiga Gitaa mkongwe wa Nchini DRC Dennis Lokassa maarufu kama Lokassa ya Mbongo ambaye siku ya kuzikwa kwake ikawadia jijini Kinshasa ikiwa ni miezi 10 tangu afariki.
Mazishi hayo yaliyotawaliwa na ukimya yalikuwa tofauti na mazishi ya awali ya Wanamuziki wenzake waliotangulia mbele za haki, huku Wanafamilia walijumuika na maafisa wa muungano wa muziki wa Kongo na baadhi ya wafanyakazi wenzake wa zamani.
Kiongozi wa muungano huo, Adios Alemba ambaye aliungana na Maitre John kuwasilisha ujumbe wa rambirambi kutoka kwa wasanii wenzake nchini DRC na kwingineko alisema kuutokuwepo kwa uhakika wa tarehe ya mazishi yake, tangu mwili wake uliposafirishwa kwa ndege kutoka Marekani hadi Kinshasa mwezi Aprili 2023 ambako alifariki, ndiyo sababu kuu ya wengi kutofika.
Ratiba ya maziko yake ilitolewa siku ya Jumatano Desemba 13, ikionesha Mwili wa Lokassa utazikwa Ijumaa Desemba 15, 2023 na hivyo muda kutoluwa rafiki kwa wapendwa walio mbali hasa nje ya nchi kuweza kufanikisha safari kuhudhuria maziko.
Eneo alilozikwa Lokassa ni lile ambalo lipo nje kidogo ya jiji la Kinshasa ambapo baadhi ya Wanamuziki wengine mashuhuri kama vile Tabu Ley, Ndombe Opetum, La Poetre Lutumba Simaro, Tshala Muana, La General Defao Matumona na Mzee King Kester Emeneya walizikwa hapo.
Tangu kuondoka kwa Tabu Ley Afrisa International mwishoni mwa 1977, Lokassa alikuwa akiishi Abidjan, Ivory Coast na miji mingine ya Afrika Magharibi na pia aliweka makazi Ufaransa mwanzoni mwa miaka ya 1980 na baadaye kuhamia Marekani mwishoni mwa miaka ya 1990.
Baadhi ya nyimbo maarufu alizowahi kutunga Lokassa ni pamoja na Marie Jose, Bonne Annee, Monica, Sophia na Adiza kwa sehemu kubwa akimshirikisha katika uimbaji Mkongwe Shimita el Diedo na kundi la Soukous Stars.
1 307
Bilionea MNigeria Femi Otedola alipoulizwa kwenye interview, ya Simu na Mtangazaji wa Radio, "Sir ni kitu gani unachokumbuka kilichokufanya uwe na furaha maishani?"
Femi alijibu:
"Nimepitia hatua nne za furaha katika maisha yangu na mwishowe nilielewa maana ya furaha ya kweli."
Hatua ya Kwanza ilikuwa ni kutafuta Mali na kulimbikiza. Lakini katika hatua hii sikupata furaha niliyoihitaji.
Nikaingia hatua ya pili ya kujinunulia vitu vya thamani. Lakini niligundua kuwa vitu vyote hivi vinakupa furaha ya muda tu ambayo haidumu.
Nikaingia hatua ya tatu ya kufanya miradi mikubwa. Ni katika hatua hii nilikuwa ninasambaza 95% ya Diesel Nigeria yote na Africa Kwa ujumla. Pia nilikuwa mmiliki mkubwa wa Vessel Africa na Asia. Lakini pia hapa sikupata furaha niliyokuwa nimeifikiria.
Hatua ya nne ilikuwa ni kipindi ambacho Rafiki aliniomba kununua Wheelchairs Kwa ajili ya watoto walemavu. Walikuwa kama watoto 200 hivi.
Baada ya kuombwa na rafiki yangu nilinunua Wheelchairs 200 mara moja.
Lakini pia aliniomba niambatane naye ili nikawakabidhi watoto zile wheelchairs. Nilijiandaa nikaambatana naye.
Nikawagawia zile wheel chairs Kwa mikono yangu mwenyewe. Niliona furaha ikitawala kwenye nyuso za hawa watoto. Nikawaona wamekaa kwenye wheelchairs, wakizunguka na kufurahia.
Ilikuwa ni kama wako Picnic wakisherehekea ushindi wa bahati nasibu.
NiIihisi furaha ya kweli ndani yangu. Nilipotaka kuondoka mtoto mmoja alinishika miguu yangu. Nilijaribu kujinasua taratibu lakini alinikazia macho akinitazama usoni.
Niliinama chini nikamuuliza, kuna kitu kingine unahitaji?
Jibu alilolitoa mtoto huyu sio tu kwamba lilinipa furaha bali pia lilinifanya nibadili kabisa mtazamo wangu juu ya maisha. Mtoto huyu alisema:
*"Ninakuangalia ili niikumbuke Sura yako, siku nikikukuta mbinguni niweze kukutambua na kukushukuru tena."*
Je Wewe mwenzangu, utakumbukwa Kwa lipi utakapoondoka kwenye hiyo Kampuni, Ofisi, Biashara, Kazini au mahali unapoishi?
Je kuna Mtu atatamani kuuona uso wako tena siku za usoni?.
1 307
Hii ni timu ya wanawake ya PSG 😋
Nadhani Sasa umeanza kupata Jibu kwanini Kylian Mbape hataki kuondoka PSG 🤣🤣🤣🤣
1 307
KUTOKA MITANDAONI
Kwa habari zaidi SUBSCRIBE kupitia YOUTUBE channel yetu kwa ku bonyeza hapa chini.👇.kwenye link
https://youtube.com/@E-PlusMediaTv?si=JjehK80_nkzrHGNK
1 307
FULL VIDEO NA MATUKIO MAZIMA UTAYAPATA KWA KU BONYEZA HAPA KWENYE INSTAGRAM LINK:-https://instagram.com/e_plus_media?utm_medium=copy_link
FACEBOOK PAGE FOLLOW:-https://www.facebook.com/eplusmediatv/
1 307
UNADHANI KATI YA LADY JAY DEE NA RAY C NANI MKALI ZAIDI KWENYE MZIKI KATI YAO..
1 307
⚠️ Baada ya mkwaruzano uliobuka baina ya wakongwe hao wa Bongofleva, mashabiki kila mmoja anasema lake kuhusu vipaji vyao, lakini kwa mtazamo wako wewe kati ya Jidee na Ray C nani unaona ana kipaji zaidi cha muziki kumzidi mwenzie?
1 307
WAZAZI MSIBANIE VIPAJI VYA WATOTO WENU VINA MANUFAA, LEO HII MIMI SANDRAH NAVAA CHENI YA DHAHABU; MAMA DANGOTE
"Wazazi wenzangu nawasihi sana kama mtoto wako ana kipaji chochote naomba muendeleze, na kama mimi ningekuwa nasikiliza maneno ya watu leo hii mwanangu Naseeb kwa sasa anafahamika kama Diamond Platnumz kipaji chake kingepotea bure. Kwakuwa nilikuwa naambiwa nawafundisha uhuni juu ya kuwa alikuwa anapenda sana mziki na mimi ndio nilikuwa namba moja kumpeleka sehemu yoyote wanayosaka vipaji"
"Nilikuwa sijali hata tukikesha mpaka asubuhi ilimradi mwanangu apate nafasi nae aimbe tu basi hapo roho yangu kwatu, sasa naombeni wamama wenzangu kuimba sio uhuni ni kazi kama kazi nyingine, waacheni watoto wafanye au waonyeshe vipaji vyao vina manufaa kwao na kwetu wazazi.......haya mimi ningewasikiliza je? leo hii Sandrah navaa cheni ya dhahabu, ni jambo la kumshukuru Mungu🤲, Asante sana mwanangu Naseeb"-ameandika Mama Dangote
1 307
"Sina Twitter nitakujibu hapa, wewe ukijiangalia kwenye kioo tu ni depression tosha, umuue nani kwa depression sasa kwa lipi hasa? Kutwa kutembea na michupa ya pombe kwenye gari hivi huwezi kuwa sawa bila kunywa hiyo mipombe kila siku? kama hujui basi nakujuza you are alcoholic you need Jesus! Acceptance and Rehab. Kuzomea mapito ya wenzio haitakujenga, chuki zako wewe kwangu ni za miaka na miaka, labda watoto wa juzi hawajui"
"Najua huamini kama nimesimama tena ndio maana una wenge, nilikuachia nafasi miaka nikataabika, ungefanya basi ya maana ufike levo za kina Tiwa Savage lakini wapi, anyway tuongee kiutu uzima wewe ni mkongwe nadhani ulitakiwa usiwakebehi watu wenye depression unatakiwa uwe makini na mambo uyaandikayo kwenye platforms zako maana watu wanajinyonga kila siku sababu ya msongo wa mawazo ( mental health is real)"
Familia nyingi tu zinateseka, so kashfa haikufanyi wewe uwe bora kuliko wengine maana kila mtu ana mapito yake kwenye hii dunia, ingekuwa mtu ana uwezo wa kuchagua pito basi nina uhakika anayeteseka na kansa leo pale ocean road angechagua gonjwa lingine. Nadhani kwanza wewe mwenyewe labda hujui ngoja nikujuze, kwa experience yangu niliyoipata pombe ina addiction mbaya mnoo na ina madhara makubwa tu"
"Ukiendekeza kunywa kama ufanyavyo mbeleni unaweza jisababishia matatizo makubwa tu, tafuta msaada wa kisaikolojia eidha uende Rehab maana zipo nyingi za wenye uraibu wa pombe. Unajua kuna umri ukifika alafu vitu fulani hujaweza kufanikisha mtu anaweza vurugwa akajikuta anaongea hovyo hovyo tu ilimradi kujiburudisha angali ndani ya moyo ana mengi yanamsibu, ama ukajikuta unalewa tu hovyoo huwezi lala bila pombe"
"Naomba nikushuhudie leo naona Ukuu wa Mungu kwenye maisha yangu sababu nilikubaliana na hali nikakubali kuwa nina tatizo na nikakubali kupata msaada wa kisaikolojia. Leo hii natembea huku nang'ara maana Mungu wangu kaniheshimisha, kwahiyo hujachelewa dada, maisha bila mipombe inawezekana, maisha bila madawa inawezekana ni kuamua tu bidada"- Ujumbe wa Ray C kwa Lady Jaydee
1 307
KARIBU SOMALILAND
nchi ambayo inaaminika kua na viwango vya juu vya watu wasiojua kusoma na kuandika na uchumi ulioharibiwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe!!
Dola moja ya Marekani ni sawa na shilingi 9,000 za Somaliland - sarafu hiyo imeshuka thamani hadi watu wanatangatanga sokoni wakiwa na vijiti vya pesa za karatasi kwenye mifuko yao.
Kuhusu wabadilishaji fedha ambao wanaendesha maisha yao kwa kubadilisha dola za Marekani na euro kwa shilingi mitaani, mikokoteni mara nyingi hutumiwa kuhamisha bili kutoka mtaa mmoja hadi mwingine.
Katika nchi hii kusafirisha pesa ni ngumu kuliko shughuli yeyote ile.
1 307
Na hivi ndivyo dimba la Amaan lililopo Zanzibar linavyooneka nyakati za usiku. Ikumbukwe hapa ndipo michuano ya kombe Mapinduzi itakapotimua vumbi mwanzoni mwa mwezi January mwakani, 2024.
Picha za Kumbukumbu nzuri la kuvutia zitapigwa hapa.
1 307
Serikali imesema katika kipindi cha Januari Mosi hadi Desemba 13, mwaka huu jumla ya ajali 1,641 zimetokea barabarani na kusababisha vifo vya watu 1,550 huku wanaume wakiwa 1,189, ambao ni sawa na asilimia 76.7.
Aidha, katika majeruhi 2,562 wa ajali hizo, wanaume waliojeruhiwa ni 1,721 sawa na asilimia 67 huku idadi ya majeruhi wanawake wakiwa 841, ambao ni sawa na asilimia 33.
Akibainisha taarifa hizo mbele ya waandishi wa Habari, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni amesema madereva 1,226 walifikishwa mahakamani na madereva 2,596 walifungiwa leseni kutokana na makosa mbalimbali.
1 307
@roma_zimbabwe ame share chat zake na msanii mwenzake @madeeali ambazo zikimuonesha kuwa ame block namba ya msanii mwenzake Madee na hii ni baada ya Madee kumtafuta Roma baada ya kufungiwa na baraza la sanaa Basata
