E-PLUS MEDIA
الذهاب إلى القناة على Telegram
1 307
المشتركون
+124 ساعات
-27 أيام
-1330 أيام
أرشيف المشاركات
1 307
MAANDAMANO MAKUBWA NCHINI ISRAEL | BENJAMIN NETANYAHU KUNG'OLEWA MADARAKANI.
Wakati vita kati ya Israel na Palestina ikizidi kupamba moto huku mamia ya raia wasio na hatia wakingoja miujiza ya Mungu kusitisha vita hiyo, hali si shwari kwa Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu ambaye anaonekana amekalia kuti kavu kutokana na kufanyika kwa mashambulio ya Hamas dhidi ya nchi hiyo mapema Oktoba mwaka huu.
Huko nchini Israel kwenye miji mbalimbali, maelfu ya raia wa nchi hiyo wanashiriki kwenye maandamano dhidi ya serikali yao wakidai;- kwanza, ndugu zao walioshikiliwa mateka na Hamas warudishwe salama. Pili, serikali yao isikilize madai ya Wapalestina. Vinginevyo ni kuwaweka hatarini jamaa zao walio ukanda wa Gaza. Lakini kubwa zaidi wakimtaka Waziri mkuu wa nchi hiyo, Benjamin Netanyahu ajiuzulu.
Maandamano hayo ambayo yalienda sambamba na kura ya maoni, ambapo ilionyesha zaidi ya robo tatu ya Waisrael hawamtaki Nenyahau kuendelea kuongoza taifa hilo. Ghadhabu ya umma ikiongezeka dhidi ya viongozi wao wa kisiasa na kiusalama, huku vuta nikuvute ikiendelea baina ya umati wa watu unaoonekana kusukuma vizingiti vya Polisi kuzunguka makazi ya Netanyahu huko Jerusalem wakati huo Maafisa wa Jeshi la Polisi wakiwazuia waandamanaji hao.
Matokeo ya kura ya maoni iliyopigwa hapo jana yanaonyesha kuwa 76% ya Waisrael wanamtaka Netanyahu ambaye sasa anashikilia rekodi ya awamu ya sita kama Waziri Mkuu ajiuzulu. Na 64% kati ya hao wanasema kwamba nchi hiyo inapaswa kufanya uchaguzi mara tu baada ya vita kusitishwa.
Swali kuhusu nani aliyehusika dhidi ya shambulio hilo?! 44% ya Waisral wanamlaumu Netanyahu, wakati 33% wanalaumu Mkuu wa Jeshi na Maafisa Wakuu wa IDF. Na 5% wanamlaumu Waziri wa Ulinzi. Hii ni kulingana na kura ya maoni iliyopigwa mapema hapo jana.
Vita hii ya Israel na Hamas inagharimu maisha ya raia wa pande zote mbili, Palestina na Israel kwani vifo ni zaidi ya watu 1,405 na majeruhi 543 kwa upande wa Israel. Na kwa upande wa Palestina, vifo ni watu 9,227 huku majeruhi wakiwa watu 32,519 na wengi wa waathitiwa wa vita hii ji watoto na kinamama. Lakini kuna asilimia kubwa ya ndugu na jamaa wengi wa Waisrael waliopo ukanda wa Gaza ambao huenda ni miongoni mwa waliopoteza maisha, kujeruhiwa huku wengine wakiwa hawajulikani walipo.
Picha kwa msaada wa Reuters
#FreePalestine
#GazaWar
#IsraelvsPalestine
Na Hilal Kanal
Dar, Tz
1 307
🇵🇸⚔️🇮🇱☠️Majina ya wanajeshi wanne wa IDF walioanguka wakati wa mapigano na Hamas kaskazini mwa Ukanda wa Gaza yaliruhusiwa kuchapishwa.
• Meja Yehuda Natan Cohen, mwenye umri wa miaka 25, kutoka Mishmod Machola, kamanda wa kampuni katika doria ya Givati.
- Sajenti Gilad Nehemia Nitzan, mwenye umri wa miaka 21, kutoka Shilo, mpiganaji katika doria ya Givati.
- Sajenti Yondav Raz Levinstein, umri wa miaka 23, kutoka Eilat, mpiganaji katika doria ya Givati.
- Meja Lior Arzi, mwenye umri wa miaka 25, kutoka Givat Haim Ihud, pambana na daktari wa dharura katika kitengo cha Sheldag
1 307
Msanii wa Muziki kutoka Tanzania Barakah the Prince amesisitiza kuhusiana na kumchukia alikiba tena siyo kumchukia tu hata ampendi, hivyo katika maelezo yake msanii huyo amesema kuwa
"Nkweli bado anamchukia sana @officialalikiba na hilo hawezi kuJificha Mpaka leo hii maana ndo ukweli wake,Kwa sababu kuna vitu personal vinavyofanya amchukie KingKiba,Pia amesisitiza kuwa sio lazma ampende Alikiba" amesema Baraka The prince
Ikumbukwe tu siyo mala ya kwanza msanii huyo kuweka wazi kuhusiana na kumchukia alikiba, ila awali alishawahi kuzungumza hivyo kwenye Media lakini hakuweza kuweka sababu nini zilizomfanya amchukie kiasi hicho lakini wenda wawili hao watakuwa wamegombana kwani kila akihojiwaa anasema vitu ni personal
Je unakipi cha kumshauri Baraka the prince kuhusiana na kumchukia alikiba ...Dondosha maoni
#updates
1 307
SUB MARINE YENYE NUCLEAR YAWASILI MASHARIKI YA KATI
Marekani ameshafikisha nyambizi yake ambay imebeba makombora ya masafa marefu na yale ya cruise missile ambapo pia imebebeshwa vichwa vya nuclear tayari katika viunga vya bahari karibu na Israel .
Mpaka sasa bado haijafahamika kama kazi kubwa ya upelekwaji wa nyambizi hiyo itakuwa ni nini haswa kama ni kwa ajili ya vita dhidi ya Hamas na Israel au kuna kazi nyengineyo nyengine .
Bunge la Congress limetenga kiasi cha 14.7 B pesa za kimarekani kwa kuipatia Israel ili kutumika katika yale yanayoendelea kati yake na Israel na kwa yeyote yule atakayetaka kujihusisha na vita inayoendelea huko
Katika kiasi hicho kilichotajwa cha msaada huko Israel kitajumuisha mpaka ndege ambazo zinabeba silaha za kimakakati kama B52 na B2 na bila ya kusahahu Air super power kama F35 na nyenginezo
❌❌❌❌❌❌❌❌❌❌❌❌❌❌❌❌
Nadhani kuna mtu atapelekwa anapohitaji yeye mwenyewe kwenda , dhana zinazidi kusogezwa katika mahala husika haswa
Nchi ya Iran inafahamu kuwa dozi hii ni kwa ajili yake sasa basi akiendelea tu
Mimi yangu macho na mnatakiwa muelewe sina upande wowote ule ila nawaonea huruma sana baadhi ya nchi kwakuwa zitakwenda kukutana na vitu vizito kabisa
1 307
Vita mpya huko Nchini (Instagram) ni Lukamba na aliyekuwa Mke wake Lucy. Vita hii imeanza baada ya Lucy kumshambulia Lukamba, sasa hivi ni zamu ya Lukamba kujibu mapigo 😂
1 307
KUTOKA MITANDAONI
Jiunge ukurasa wetu wa what's up hapa kwenye link.👇
https://whatsapp.com/channel/0029VaD9yM1D8SE3Brlapz1l
1 307
Pichani ni Sonia Monalissa, anayedaiwa kupikwa katika malezi bora na wazazi wake na akapikika.
1 307
NDOA/DINI VILIMNYIMA UHURU QUEEN MTALAKA WA DR. MWAKA, MAMBO NI SAFI BAADA YA KURUDI KWENYE DINI YAKE NA KUWA NJE YA NDOA.
Ukiingia kwenye ukurasa wa Instagram wa Queen Masanja ambaye awali alikuwa akijitambulisha kama Queen Mwaka, utagundua kwamba sasa hivi ana furaha, ana maisha mazuri na anaishi kwa uhuru huku akionekana kufanya kazi usiku na mchana.
Havai tena Hijab na Baibui, mara nyingi anajirekodi akicheza nyimbo za dini ya Kikristo na ni mwenye furaha kubwa, mara kadhaa amekuwa akiwajibu watu wanaomuuliza kuhusu kurudi kwenye dini yake ya Kikristo na majibu yake amekuwa akiwajibu kwamba anafata kile kitu moyo wake unapenda.
Queen alikuwa ni Mkristo lakini baada ya kuolewa na Dr. Mwaka alibadili dini na kuwa Muislam. Hata hivyo kwenye komenti Waislamu wengi wamekuwa wakimtaka arejee kwenye Uislamu aache kutapatapa huku na kule huku wengine wakisema hilo ni kama funzo kwa wanaume wanaotaka kuoa kwamba ni bora kuoa mwanamke wa dini yako ambaye hata mkiachana mkiwa tayari mmezaa watoto, watoto wajue dini moja ya kwenda kuliko kutapatapa wasijue waende kwa mama au baba.
1 307
⚠️ Baada ya Diamond Platnumz kushinda tuzo za MTV Europe Music Awards (MTV EMA) 2023 katika kipengele cha msanii bora kutoka Afrika kwa kuwabwaga kina Burna Boy, Asake(Nigeria), Libianca (Cameroon) na TylerICU (Dj wa Afrika Kusini) , sasa ndie msanii wa Afrika anayeshikilia rekodi ya kuwa na tuzo nyinginza MTV EMA
1 307
SPIKA TULIA ACKSON AINGILIA KATI WAALIMU KUSHUSHWA VYEO KISA WIMBO WA ZUCHU
Spika wa Bunge la Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Tulia Ackson,Leo Novemba 06,2023 Bungeni Jijini Dodoma amehoji kama utaratibu umefuatwa kuwasimamisha kazi walimu wawili wa shule ya Tunduma baada ya kupiga wimbo wa msanii Zuchu ujilikanao kama 'HONEY' shuleni na kuwachezesha wanafunzi.
Aidha Spika Tulia amesema kama utaratibu haukufuatwa, walimu hao wanapaswa kurejeshwa kazini na kuendelea na shughuli zao.
1 307
Bi.Christina Ozturk mwenye umri wa miaka 26 kutoka nchini Russia ambaye kwasasa ana watoto 22 amesema kuwa bado anapambana na ana muomba Mwenyezi Mungu amfanyie wepesi kwasababu lengo lake ni kupata watoto 100 akiwa duniani kutokana na kuwa anapenda sana watoto.
1 307
Hizi picha zitunzwe sana ili tuweze kuwaelezea wajukuu zetu wasije dhani timu nzima ya Simba walicheza na @aziz.ki.10 peke yake 🤣🤣🙌
1 307
Kikosi cha Timu ya Taifa “Taifa Stars” kitakachoingia kambini kwa michezo ya kufuzu Kombe la Dunia vs Niger na Morocco @TaifaStars_
1 307
Nyota wa Klabu ya KMC FC,Ibrahim Mao ameitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Somalia kwa ajili ya michezo miwili ya kufuzu kombe la dunia dhidi ya Algeria na Uganda mapema mwezi huu.
Another one kutoka Jumba la ladha na hekaheka za #LigiKuu
