E-PLUS MEDIA
الذهاب إلى القناة على Telegram
1 307
المشتركون
+124 ساعات
-27 أيام
-1330 أيام
أرشيف المشاركات
1 307
Ratiba ya mazishi ya ndugu @ole_mushi
Ibada ya kuaga mwili itafanyika kanisa la St.Peters Oysterbay leo saa 5 kamili asubuhi hadi saa 7 mchana.
Baada ya hapo mwili utapelekwa airport ukisindikizwa na ndugu wa karibu pamoja na mke wake.
Mwili utawasili KIA saa moja na nusu jioni na utapokelewa na wanafamilia waliopo Moshi na baadhi ya waliotoka Dar.
Mwili utaenda kulala nyumbani kwao Uru, Kitandu karibu na shule ya msingi Chombo Uru.
Kesho tar.7 2024 maziko yatafanyika hapohapo nyumbani kwao Uru Kitandu. Kwa watu wote wanaotoka DSM kama unahitaji kusafiri kwenda Moshi wasiliana na ndugu Deo Mushi kwa nambari 0719 780 033.
1 307
SABAYA ATANGAZA KUWASAMEHE WOTE WALIOMKOSEA
"Kama kuna mtu nimemkosea mbele za Mungu anisamehe, na mimi mbele za Mungu anayeishi kama kuna mtu yeyote anadhani alinikosea, iwe shahidi, iwe kutengeneza kesi kunisingizia uongo, leo kwa kibali cha Mungu nimemsamehe. Nimenyanyua mikono, sitapigana, na mtu atakayeendeleza vita, naiacha vita hiyo apigane na Mungu." - Lengai Ole Sabaya
1 307
Watu wasiojulikana, wameiba majeneza mawili na mabati 10 katika Msikiti wa Marhaba ulioko Bakarani mjini Mombasa Nchini Kenya.
Kwa mujibu wa Mzee wa mtaa huo, Mohamed Hamid amesema waligundua kutoweka kwa majeneza hayo mawili yaliyotengenezwa kwa chuma, wakati walipotaka kubebea maiti zilizofikishwa msikitini kuswaliwa.
Amesema, kufuatia tukio hilo wanapanga kufanya maombi maalum ‘albadiri’, ili kulaani waliohusika na wizi huo wanaosema sio wa kawaida uliofanyika katika Msikiti huo uitwao Masjid Mar-haba.
Hata hivyo, taarifa ya Polisi wa Kituo cha Kisauni Mombasa imeeleza kuwa maafisa wake wanaendelea na uchunguzi ili kuwabaini wahalifu hao na kuwachukulia hatua.
1 307
MFAHAMU ALIYETUNGA WIMBO WA TAIFA WA TANZANIA🇹🇿
Wimbo wa taifa wa Tanzania "Mungu ibariki Afrika" ulibuniwa na mtunzi kutoka Afrika Kusini Enoch Sontonga.
Wimbo huu asili yake ni wimbo Nkosi Sikelel’i Afrika aliotunga mwaka 1897.
Tafsiri ya jina hilo kwa kiswahili ni Mungu ibariki Afrika.
Ni wimbo maarufu zaidi Afrika ukitumika pia katika harakati za ukombozi kwa Baadhi ya nchi za Afrika.
Maneno ya wimbo huo pia yanatumika kwenye nyimbo za taifa kwa nchi za Afrika Kusini,Zambia na Zimbabwe
Sontonga alizaliwa mwaka 1873 na kufariki 18/04/1905.
SHARE
1 307
JESHI la Polisi mkoani Arusha, linamshikilia hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Loliondo mkoani humo kwa tuhuma za kumlawiti kijana mwenye umri wa miaka 29 ambaye ni mwendesha bodaboda baada ya kumlewesha pombe.
Pamoja na hakimu huyo kushikiliwa, Jeshi hilo pia linamshikilia mwathirika wa tukio hilo kutokana na sheria inayosema kuwa mwanaume anayeruhusu kuingiliwa na mwanaume mwenzake naye atakuwa ametenda kosa.
Akisimulia shuhuda “Ilipofika majira ya usiku kaka wa kijana aliyelawitiwa (jina limehifadhiwa) alifika nyumbani kwa mgodo wake na kuwakuta wakiwa bila nguo, ndipo alipompigia simu hakimu mwenzake na mtuhumiwa”
“Alipokuja huyo hakimu wakapiga simu polisi na polisi walikuja kuwachukua wote wawili na hadi sasa wanashikiliwa kituoni”
1 307
🇵🇹😍 🎙 " Sidhani kama nitaolewa na Cristiano Ronaldo lakini cha muhimu kwamba mimi na yeye tunapendana sana na hilo kwangu linatosha" 🤔
🗣 Georgina Rodriguez Mpemzi wa Ronaldo.
1 307
#TANZIA
Mwigizaji wa filamu za Hollywood (Marekani 🇺🇸), Carl Weathers ambaye alitamba filamu nyingi ikiwamo "Predator" amefariki Dunia.
"Carl Weathers will always be a legend. An extraordinary athlete, a fantastic actor, and a great person. We couldn’t have made Predator without him. And we certainly wouldn’t have had such a wonderful time making it. Every minute with him - on set and off - was pure joy. He was the type of friend who pushes you to be your best just to keep up with him. I’ll miss him, and my thoughts are with his family" - Arnold Schwarzenegger (Commando).
Tafsiri isiyo rasmi 👇
Carl Weathers daima atakuwa hadithi.Mwanariadha "wa ajabu, muigizaji mzuri na mtu mzuri.Hatungeweza kumfanya Predator bila yeye.Na hakika hatungekuwa na wakati mzuri sana wa kuifanya.Kila dakika pamoja naye - wakati wa kuweka na kuondoka - ilikuwa furaha tupu.Alikuwa ni aina ya rafiki anayekusukuma kuwa bora kwako ili tu kuendelea naye.Nitamkosa, na mawazo yangu yako kwa familia yake."
"Even though I did not complete my role as the Predator in the film, Carl Weathers has been always a great friend since 1978 until the end. May his good soul RiP." - Jean Claude Van Damme, Mwigizaji wa filamu ambaye alitakiwa kuigiza kama "Predator" lakini wakashindwana na Muongozaji Mkuu (Director).
Tafsiri isiyo rasmi 👇
"Ingawa sikukamilisha jukumu langu kama Predator katika filamu, Carl Weathers amekuwa rafiki mkubwa tangu 1978 hadi mwisho.May his good soul RiP."
Tunatoa pole kwa Ndugu, Jamaa na Marafiki bila kusahau Mashabiki wake na filamu kwa ujumla.
1 307
⚠️ "Mwanamke asiye na makal!o asimdharau mwanaume wake bilionea" - Raymond Nduga mwanaume wa nchini Kenya aibuka kumdhihaki ex wake kwa jina la Dorris ikiwa ni miezi kadhaa baada ya clip kusambaa akimshambulia kwa makofi
Mahusiano ya wawili hao kwa muda mrefu yalidaiwa kujaa sumu kali kutoka kwa mwanaume huyo anayejiita mwanasheria ambapo, September mwaka jana clip ilisambaa Raymond akionekana kumpiga ex wake huyo kwa kurudiarudia, watu walimshauri Dorris kuwa aondoke katika mahusiano yaliyoonekana sio salama kwake, Dorris alidaiwa kutosikiliza ushauri
Pia baba wa Dorris alitajwa kutopenda mahusiano ya mwanae na jamaa huyo kwa kuona mwanae hayupo katika mikono salama, hivyo kumtaka mwanae arudi nyumbani ambapo Dorris alidaiwa kukaidi kwa kutomsikiliza baba yake akabaki na jamaa lakini kwasasa inaelezwa Doris amerudi kwa wazazi wake hivyo Raymond kuwa na kibarua cha kumshushia maneno makali mitandaoni ikiwemo kumuita nya*i asiye na makalio
Raymond pia amepost mdada mwingine aliyejazia mapaja anayetajwa kuwa mpenzi wake mwingine na baada ya hapo akapost picha nyingine na maneno yasiyo mazuri kwa Dorris
Pia kuna muda Raymond alionekana kupost maneno ya dharau na kumtag ndugu wa Dorris akimwambia kwa mechi za kitandani nipo vizuri sana hivyo ndugu yako(Dorris) hawezi kuniacha
Kuna muda pia ilidaiwa Raymond ndio alikuwa anapost maneno katika akaunt ya Dorris ili ionekane Dorris anampenda sana Raymond
Jamaa huyo anajiita bilionea, anatajwankusomea sheria na pia aliwahi kugombea moja ya nafasi za kiungozi kupitia siasa(ugavana) akakosa
#saynotodomesticviolence
1 307
"Mwanamke unampigia video call usiku anapokea akiwa kitandani na mwanaume mwingine huyu ni mwanamke? Alikuwa tayari ameshapanga kuniacha alikuwa ananiuliza maswali ya ajabu ajabu ambayo niliona kabisa hapa kuna dalili ya kuachwa"- Mr Nana aliyekuwa mpenzi wa Dida Shaibu
1 307
⚠️😳 Akihojiwa na Diva kwenye Lavidavi, Wasafi FM, Sophia amesema yeye hutumia laki 8 kununua nywele tu na kwa mwaka hujikuta akitumia shilingi milioni 5.4 kununua nywele ambazo ni za uongo hata hivyo(false hair)
1 307
**Baadhi ya Nchi za Africa ambazo Raia wake wanazungumza zaidi lugha zao wenyewe kuliko lugha za kigeni**
1. Ethiopia 🇪🇹 (Amharic)
2. Tanzania 🇹🇿 (Swahili)
3. Somalia 🇸🇴 (Somali)
4. Kenya 🇰🇪 (Swahili)
5. Eritrea🇪🇷 (Tigrenia)
6. Zambia 🇿🇲 (Bemba, Nyanja)
7. Madagascar🇲🇬 (Malagasy)
8. Malawi 🇲🇼 (Chewa)
9. Botswana 🇧🇼 (Setswana)
10. South Africa 🇿🇦 (isiZulu,isiXhosa)
11. Lesotho 🇱🇸 (Sesotho)
#AfricaYetu....
