ar
Feedback

لا تقع ضحية للمخادعين! تيليمتريو يكتشف ويُميّز هذه القنوات 👉 إذا كنت تريد رؤية العلامة، اشترك

E-PLUS MEDIA

E-PLUS MEDIA

الذهاب إلى القناة على Telegram

Get the latest news,videos,and more everyday.

إظهار المزيد
1 307
المشتركون
+124 ساعات
-27 أيام
-1330 أيام
أرشيف المشاركات
Akiwa na miaka 5 Alifiwa na Baba yake... Akiwa na miaka 16 aliamua kuacha shule. Akiwa na miaka 17 tayari alikua kapoteza ajira 4. Akiwa na miaka 18 aliamua kuoa. Akiwa na miaka 19, alifanikiwa kuwa Baba. Akiwa na miaka 20, Mke aliamua kuondoka na mtoto. Alishindwa hata katika jaribio la kumpata mwanae, na kuamua kumshawishi mkewe kurejea nyumbani. Akiwa na miaka kati ya 18-22, alikua msimazi wa njia za reli lakini alishindwa akafukuzwa. Baadae alijiunga na Jeshi lakini akafukuzwa pia. Akatuma maombi shule ya sheria ila hakupata nafasi. Akawa muuzaji wa Bima lakini alishindwa pia. Hatimaye akapata ajira kama mpishi na mwosha vyombo wa mgahawa mdogo. Akiwa na miaka 65 alistaafu ajira yake ya kupika na kuosha vyombo katika mgahawa, Baada ya kustaafu alipata mafao yake kutoka serikalini dola 105$, kama Tsh 262,500. Alidhani serikali imemuona kama hajiwezi kabisa. Akafanya jaribio la kujiua, akiamini hakuna thamani ya kuishi tena na kwamba ameshashindwa sana. Hakufanikiwa hata katik jaribio lake hilo. Akaamua kukaa chini ya mti na kuandika matarajio yake, Ila aliona ayaandike yale aliyoyakamilisha tayari. Akagundua kuna mambo mengi hakuyafanya bado. Akagundua lipo jambo moja ambalo anaweza kulifanya vizuri zaidi kuliko mtu yeyote yule anayemfahamu. Na ilikua ni namna gani ya kupika. Akaamua kuchukua dola 87$ kama Tsh 217,500 kutoka kwenye Hundi yake ya pensheni na kununua kuku. Akawakaanga kwa kuwachanganya na viungo anuai akapata mchanganyiko wa aina yake (unaovutia). Akaamua kupita mlango kwa mlango kuwauza kwa majirani zake huko Kentucky. Mchanganyiko ule ukapendwa sana na akaamua kuanzisha mgahawa wake uitwao Kentucky Fried Chicken (KFC)... ...uliokua ukitengeneza mchanganyiko wa kuku alioubuni. Hatimaye biashara yake ikakua na akafungua migahawa mingi ya KFC nchini Marekani. Mchanganyiko ule ukazidi kupendwa na kutanua wigo wa biashara yake. Huyu si mwingine ni Colonel Harland Sanders mwanzilishi wa migahawa ya KFC duniani. Licha ya kustaafu akiwa "fukara wa kutupwa" katika umri wa miaka 65, lakini hadi wakati anafariki (1980)... ...akiwa na umri wa miaka 90 alikua katika orodha ya mabilionea wakubwa nchini Marekani. Kwa sasa migahawa ya KFC imeenea kote duniani katika nchi 123, Tanzania ikiwemo. Na ni mgahawa wa pili mkubwa ulioenea zaidi duniani baada ya migahawa ya McDonald's. Mwaka 2013 migahawa ya KFC ulifanya mauzo ya dola Bilioni 23 sawa na Tsh Trilioni 50. Kumbuka muasisi alikua FUKARA hadi uzee wake (miaka 65) na akadhani ameshindwa maisha. Akajaribu kujiua. Lakini baada ya kutafakari akaona bado ana nafasi ya kujaribu tena. Akajaribu japo katika umri wa uzee, na hatimaye Mungu akamfanikisha. Akawa BILIONEA MKUBWA sana nchini Marekani. Je wewe umekata tamaa ya maisha? Ulitamani kusoma lakini ukashindwa kwa kukosa ada? Umesoma lakini umekosa ajira? Miaka inapita na unaona wenzio wanaajiriwa wewe uko tu nyumbani? Je Umejaribu biashara lakini kila wakati unapata tu hasara? Unahisi kukata tamaa? Unahisi Mungu amekuacha? Usikate tamaa. Mungu hajakuacha. Jipange tena na uanze upya. Haujakawia bado.... Kitu kikubwa ni "Mtazamo" ( Attitude). Usikate tamaa .... Haijalishi mambo ni magumu kiasi gani. Una kila kitu cha kukufanya Ufanikiwe. Amua kubadili mtazamo ili kubadili Stori ya maisha yako. Inawezekana, anza sasa.! Kama umejifunza vitu tafadhali SHARE makala hii na rafiki/ndugu/jamaa wengi kadri uwezavyo... ...kwa maana hiyo ndio njia pekee ambayo mimi na wewe tunaweza itumia kugusa maisha ya wengi na sote tukatimiza malengo yetu kwa kasi. Cc: Joel Nanauka

photo content

Lissu akakubali na akafanya kazi yake kwa weledi wa hali ya juu. Mh. Lissu akasaidia pia kushinda kesi za wananchi wanyonge 366 katika kipindi cha miezi minne tu. Hawa ni wananchi waliokuwa wakiishi pembezoni mwa migodi kabla ya kuswekwa ndani kwa kosa la kuvamia migodi hiyo. Lissu aliwatetea bure wananchi hawa mafukara na baada ya ushindi wa kesi hizo akatamka-"Uwekezaji umegeuka kuwa unyama Tanzania". Lissu akaonekana ni mtu asiye na uzalendo na taifa lake kwa kuwasema vibaya wawekezaji ambao serikali ilikuwaikidai walikuwa wakiliingizia taifa mapato makubwa. Hata hivyo, kwa wananchi hao wanyonge, Lissu alionekana ni Mfalme. Baadae Mh. Mbowe akampigia Lissu na kumuomba asaidie kutafuta wanasheria wengine waingie CHADEMA kama yeye. Lissu akamshangaza Mh. Mbowe kwani bila kupepesa macho wala kutikisa maskio, Lissu akasema yeye ni mwanachama wa NCCR MAGEUZI! Mh. Mbowe alistaajabu sana kwani aliamini Lissu ni mwanachama wa CHADEMA. Hivyo, Lissu akamwambia Mh. Mbowe "kama unataka nijiunge nanyi basi najiunga" ndivyo Lissu alivyojiunga CHADEMA. Lissu aliendelea na jitihada zake kuwasaidia wananchi waliokuwa wakinyanyasika migodini huku akiacha wateja wenye fedha nyingi Dar Es Salaam. Kwa Lissu, hakuna kitu kinamuuma moyoni mwake kama akiona mnyonge ana haki lakini anaonewa. Lissu kamwe hawezi kukaa kimya kuona hali hiyo ikiendelea. Jitihada hizi zikamfanya Lissu azidi kukorofishana na serikali mara kwa mara. Serikali ikamwita ni mchochezi anaechochea wananchi kuwachukia wawekezaji wa Barrick ambao serikali ilikuwa ikidai ni wawekezaji wazuri waliokuwa wakiliingizia taifa pato kubwa. Lissu amekuwa mstari wa mbele kwenye harakati za kutetea sekta ya madini nchini. Kwa miongo zaidi ya miwili amekuwa akipambana na wawekezaji wazungu waliokuwa wakikingiwa kifua na serikali ya awamu ya tatu na ya nne na kuonekana yeye si mzalendo. Alikuwa ni mmoja wa waliopinga hadharani na kwenye maandiko yake, sheria ya madini ya mwaka 1998 na ya 2010 kwa hoja kwamba zinawatajirisha wawekezaji wazungu na kutuachia watanzania mashimo tu na umaskini mkubwa wakati Mungu aliibariki nchi hii kwa kuipa madini mengi. Hoja hizi zilikuwa zikikejeliwa na wabunge wa CCM ambao walikuwa wakiipitisha miswada hii kutokana na wingi wao bungeni. Aidha, Lissu alipinga vikali kupitishwa na bunge sheria zote za madini kwa hati ya dharura mwaka 2015 na 2017. Licha ya jitihada hizi kubwa za kuwapigania wananchi wanyonge na maskini huku wengi akiwatetea mahakamani bure na kupambana vikali na wawekezaji wa makampuni ya madini ambayo yeye miaka yote amekuwa akiyaita ni ya wezi wanaotuibia madini yetu na kunyanyasa wananchi migodini, Lissu anaonekana kwenye macho ya baadhi ya watu kwamba si mzalendo bali ni "kibaraka anaetumiwa na wazungu asieitakia mema nchi yetu". Tundu Lissu kwa Sasa anaongoza vuguvugu la kuiondoa CCM madarakani.

RPC Mahita, kwa wajihi, ni mweupe sana lakini swali hilo lilimbadilisha na kuwa mwekunduuuu. Ghafla bin vuu maafande wakamkimbilia Lissu kutaka kumkwida kwa "kosa" la kutukana meza kuu. Bahati nzuri, Kanali Shija akawa na busara na akawazuia na kuwaambia "Huyo kijana Lissu yupo sahihi kwani hicho ndicho alichosema Baba wa Taifa." Huo ndio ukawa mwisho wa mkutano. Baada ya songombingo na tafrani hiyo ya kipekee siku hiyo, maafande wote wa Itende JKT wakaanza kumuogopa sana Lissu wakiamini yeye ni mtu wa Usalama wa Taifa na akawa hapangiwi tena kazi bali akawa anakula shushi hadi kumaliza muda wake! Kutokana na kufaulu vizuri kidato cha sita, Lissu alijiunga na kitivo cha sheria mwaka 1991 UDSM. Huko aliendelea na harakati zake za kupigania haki za wanafunzi na akajiunga na NCCR MAGEUZI. Miaka hiyo, chama hicho kilichokuwa chini ya mmoja ya viongozi waliowahi pendwa mno nchini, Mh. Augustin Mrema, ndicho kilikuwa chama kikuu cha upinzani nchini. Baadae mwaka 1995, Lissu akaenda kusomea shahada ya uzamili chuo cha Warwick UK. Alipofika huko akaomba ruhusa aje kugombea ubunge Singida mashariki. Hata hivyo, kutokana na maandalizi duni, kura hazikutosha hivyo akarejea masomoni. Lissu alipomaliza masomo yake 1997 alirejea na kufanya kazi ya sheria Arusha. Baadae akaoa na kuhamia Dar Es Salaam. Akawa mmoja wa wanasheria wa chama cha wanasheria wa mazingira (LEAT) pamoja na Dr. Rugemeleza Nshalla na Alex Shauri. Lissu akaanza kujipambanua kama Mtanzania anaepigania haki za wanyonge na maliasili za nchi yake bila woga wowote. Ujasiri wake mkubwa wa kwanza kupigania maliasili za taifa lake ulikuwa mwishoni mwa miaka ya 90. Serikali ya awamu ya tatu ilikuwa imempa raia wa Ireland aitwae Reginald Nolan hekta 20, 000 kuchimba mabwawa ya kambakoche kwenye delta ya Rufiji katika maeneo ya watu yenye vijiji nane waliokuwa wakiishi na wakilima humo. Lissu aliwahurumia sana wananchi hao wanyonge. Hivyo, aliratibu kampeni iliyoendeshwa na LEAT kimataifa kuupinga mradi huo kwa kutumia njia mbalimbali ikiwemo mitandao ya kimataifa. Hii ilikuwa ni kazi ngumu mno na yenye vitisho vingi. Ilikuwa si ajabu asubuhi kukuta chini ya mlango wa ofisi ya LEAT Mavuno house barua ya vitisho. Lissu hakujali wala kuogopa. Kutokana na juhudi kubwa ya Lissu, hatimaye "European Investment bank", iliyokuwa tayari kutoa mkopo kwa Nolan ambao ungedhaminiwa na serikali ya awamu ya tatu, ikakubaliana na hoja kuntu za Lissu na kugoma kutoa fedha hizo. Hivyo, mradi huo ukasambaratika. Huu ulikuwa ushindi mkubwa kwa Lissu na alipongezwa mno na wanavijiji hao wanyonge waliomuona shujaa. Lissu akapata umaarufu na kualikwa kwenye kipindi cha "Hamza Kasongo hour" Octoba 1998 na mzalendo mmoja akawa amempa nyaraka za Baraza la Mawaziri ambazo zilisema mradi huo ni wa hovyo na ulipitishwa kinyemela! Mwezi Septemba 2000 alikwenda USA kama mtafiti kwa miaka mitatu kwenye kampuni ya World Resource Institute huku akirudi mara kwa mara nchini kuendelea na kazi za LEAT. Mwaka 2001 yeye na wenzake wa LEAT walifanya Press conference maelezo na kudai wana ushahidi wa video kuhusu mauaji ya Bulyankulu. Yeye akarudi US lakini wenzake wakakamatwa. Akasikia imeelezwa ametoroka na atafutwa na Interpol. Akarudi na akakamatwa. Akasachiwa nyumbani kwake na kupelekwa Central. Akafanya ujanja na kuingia na simu na usiku kucha akawa anawasiliana na magazeti ya US na Canada. Hiyo ikamsaidia kuondokana na msala huo. Je Lissu aliingiaje CHADEMA? Lissu alijiunga CHADEMA mwaka 2004. Mwaka 2003, Lissu alikwenda Tarime kwenye masuala ya madini. Akakutana na Mh. Chacha Wangwe akiwa Diwani wa Tarime akiwa na kesi kumi za jinai. Mh. Wangwe akamwambia Lissu kuwa wanataka kumfunga. Lissu akamwambia aondoe hofu hawataweza. Mh. Mbowe akampigia simu Mh. Lissu kumuomba amtetee Mh. Wangwe kwenye hizo kesi zilizokuwa zikifunguliwa kila uchao.

HISTORIA FUPI YA TUNDU ANTIPHAS LISSU. Lissu alizaliwa tarehe 20 Januari 1968 na alisoma shule ya msingi Mahambe, Singida. Katika miaka yake yote saba shuleni hapo, Lissu hakukubali hata mara moja kuamka alfajiri saa 11 kuwahi namba na daima aligomea kulima mashamba ya walimu, kuwachotea maji na kazi za namna hiyo kwani kwake aliona haziko sahihi. Hii ilipelekea awe anatandikwa bakora mara kwa mara. Shuleni hapo, bakora na mwili wa Lissu vilikuwa ni kama uji na mgonjwa. Hata hivyo, kilichomsaidia ni akili yake. He was a very, very brilliant pupil (mwanafunzi). Lissu alifaulu mtihani wa darasa la saba na kwenda shule ya sekondari ya Ilboru, Arusha. Shuleni hapo, yeye ndie aliyekuwa mwanafunzi mdogo kuliko wote. Licha ya udogo wake, alikuwa mwiba mkali kwa prefects na walimu. Akiwa kidatu cha tatu wenzake walimtaka awe prefect (kiongozi wa wanafunzi) lakini alikataa kwani alizoea kuwaita "manyoka" kwa tabia yao ya kupenda kupeleka taarifa za wanafunzi kwa walimu. Lissu alifaulu vizuri na kuingia kidato cha tano shule ya sekondari ya Galanosi, Tanga. Akiwa Galanosi, akapewa Uenyekiti wa Kamati ya Taaluma. Hata hivyo, akakorofishana vibaya mno na mwalimu wa taaluma na kuvuliwa cheo hicho. Akiwa kidato cha sita mwaka 1988, kulikuwa na disko la graduation. Kidato cha sita wakaruhusiwa kwenda kucheza na Korogwe girls lakini kidato cha nne wakakataliwa na wakaambiwa wataletewa taarabu shuleni hapo. Lissu aliona huo ni uonevu na daima shuleni hapo alichukia mno mwanafunzi mwenzake kuonewa hata kama ni wa madarasa ya chini. Hivyo, akaandika Waraka "TAARAB FOR WHOSE INTEREST". Lissu hakuandika jina lake kwenye Waraka huo. Akaubandika kwenye ubao wa matangazo usiku. Walimu walipouona walichukia sana na wakachunguza na kuhisi mwanafunzi pekee aliyepinda shuleni hapo mwenye ubavu wa kuandika vitu kama vile ni Lissu tu hivyo wakamkamata. Walimu wakamwita Lissu mchochezi na hivyo akapewa suspension. Hata hivyo, baadae akarudishwa shuleni na kisha akafanya mtihani wa kidato cha sita. Mwaka 1989 akaenda Mafinga JKT kisha Itende JKT kwa mwaka mmoja. Wakati huo, vuguvugu la vyama vingi lilikua limepamba moto nchini huku CCM ikiwa haitaki kabisa kusikia mambo ya vyama vingi. Katiba ya CCM ilikuwa inautambua Mkoa wa Majeshi hivyo ilituma viongozi wake kutembelea kambi zote na kuulezea msimamo wa CCM kutotaka kuskia takataka inayoitwa vyama vingi. RPC Omary Mahita (Rukwa) na Kanali wa Andrew Shija wakitokea Mkoa huo wa Majeshi wakapangiwa kwenda Itende JKT kuwaelezea servicemen msimamo wa chama. Walipofika wakaitisha mkutano mkubwa na ukumbi ukawa umefurika. Katika mkutano huo, Mahita na Shija wakaeleza kwamba "Sisi haya mambo ya vyama vingi hayatuhusu. Haya ni mambo ya wazungu huko Ulaya mashariki hivyo tusiyashabikie". Kitu ambacho viongozi hao hawakukijua ni kwamba miongoni mwa servicemen hao alikuwepo kijana mmoja very brilliant mwenye uelewa mkubwa wa mambo mengi yanayoendelea duniani asiye na simile kuongea kilichomo akilini mwake. Lissu alikuwa amesikiliza hotuba ya Baba wa Taifa alipoongea na Baraza Kuu la Umoja wa vijana wa CCM Mwanza wiki chache kabla ya mkutano huo wa akina RPC Mahita. Mwalimu alikuwa amesema -"Wanaodhani mageuzi hayatuhusu bali yanazihusu nchi za Ulaya mashariki pekee ni wajinga kwani Tanzania sio kisiwa". Muda wa maswali ulipofika huku wengi wakiamini hakuna atakaekuwa na ubavu wa kuuliza swali, Lissu bila kuogopa na kwa ujasiri wa hali ya juu ambao haukuwahi kuonekana hapo Itende JKT, akanyoosha mkono. Servicemen wenzake waliokuwa wakijua misimamo yake isiyoyumba walijitahidi kumshusha mkono bila mafanikio. Huku akitumia lugha kali bila kumun'gunya maneno kama kawaida yake, Lissu aliwauliza viongozi hao -"Je, mjinga ni Baba wa Taifa aliyesema mageuzi ya vyama vingi yanatuhusu au ni nyie mnaosema hayatuhusu?"

photo content

Martin Luther king Jr aliwahii kuitwa gaidi kisa anapambania haki za watu weusi Marekani Malcolm x aliwahii kuitwa gaidi kisa anapambania haki za watu weusi Marekani Marcus Mosey Garvey aliwahii kuitwa gaidi kisa kuwambia wamarekani weusi ni muda wao wa kuwa na viwanda na nguvu kiuchumi pia kuwekeza kwenye elimu kwao na watoto zao Mandela aliwahii kuitwa gaidi kisa anapambana dhidii ya makaburu (wazungu) Mwalimu Nyerere aliwahii kuitwa gaidi kisa anapambania uhuru wa Tanganyika Mahatma Gandhi aliwahii kuitwa gaidi kisa anapambania uhuru wa India Mau mau waliitwa magaidi kisa wanapigania uhuru wa Kenya Duniani kote ukipigania haki yako au haki za watu wa jamii iliyokuzunguka utaitwa gaidi Especially uwe unapigania haki yako dhidii ya wazungu, Hawachelewi watakupaa majina mengi mabaya sana Ili jamii ikuchukie, neno gaidi linatumika Ili kudhulumu haki za watu wengi duniani, linatumika Ili liweze kukandamiza sauti za watu wengi duniani, linatumika Ili liweze kuharibu maisha ya watu wengi duniani, Wanayopigania wapalestina Leo hii ndio hayo hayo waliopigania, ANC, Mau mau, Malcolm x, Martin Luther king, Marcus Mosey Garvey , Mahatma Gandhi na mwalimu Nyerere pia waliitwa magaidi kwa kupigania haki zao Wakati tunaambiwa ugaidi tuwe tunafanya utafitii pia Muhsini Kwigwa Mr Kigoma

photo content

Uzuri wa Wema Sepetu wa 2010-2015 wadaiwa kurejea tena baada ya kuwa na Whozu.
Uzuri wa Wema Sepetu wa 2010-2015 wadaiwa kurejea tena baada ya kuwa na Whozu.

Croptop la Diamond Platnumz laacha gumzo
Croptop la Diamond Platnumz laacha gumzo

photo content
+4

FULL VIDEO NA MATUKIO MAZIMA UTAYAPATA KWA KU BONYEZA HAPA KWENYE INSTAGRAM LINK:-https://instagram.com/e_plus_media?utm_medi
+9
FULL VIDEO NA MATUKIO MAZIMA UTAYAPATA KWA KU BONYEZA HAPA KWENYE INSTAGRAM LINK:-https://instagram.com/e_plus_media?utm_medium=copy_link FACEBOOK PAGE FOLLOW:-https://www.facebook.com/eplusmediatv/

SIWEZI KUVAA NUSU UTUPU WALA KUJICHUBUA, NI AIBU NA FEDHEHA KWANGU; PASSY "Kitu ambacho sikipendi kwa mabinti wengi wa sasa h
SIWEZI KUVAA NUSU UTUPU WALA KUJICHUBUA, NI AIBU NA FEDHEHA KWANGU; PASSY "Kitu ambacho sikipendi kwa mabinti wengi wa sasa hivi ni jinsi wanavyojidhalilisha mitandaoni bila kujali kesho yao. Unakuta mwanamke anaenda kujidhalilisha kwenye mitandao ya kijamii bila kujua kuna madhara mbeleni, kwa mfano, mimi leo nikisema nivae cheni nizianike nje kiunoni alafu niache kitovu nje, manyonyo na maungio ya siri ambayo yanatakiwa yasitiriwe na mavazi hicho ni kitu kibaya sana "Unaweza ukaona ni sahihi kwa sasa hivi lakini tuna watoto watakuja watavikuta, hivi vitu sasa hivi vinaishi, ni bora miaka ya zamani hakukuwa na mitandao ya kijamii. Kibaya utakachokifanya sasa hivi unaweza ukahisi uko sahihi, lakini ukae ukijua kwamba kitaishi milele, watoto wako na wajukuu wako watakikuta "Mimi siwezi kuvaa nusu utupu wala kujichubua, nimeachana na marafiki zangu ambao walianza kuleta stori za kutaka kujichubua kwasababu ni mambo ya aibu na fedheha mtu kuikataa ngozi yake."- Black Passy, Mwigizaji na Mchekeshaji wa Kibongo

Waraka mpya uliotiwa saini na Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis,umesema mafundisho ya Kikatoliki na uanachama
Waraka mpya uliotiwa saini na Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis,umesema mafundisho ya Kikatoliki na uanachama wa Freemason hayawezi kutangamana au hayapatani . • Barua hiyo iliyotolewa na ofisi ya mafundisho ya Vatikani ilinukuu tamko lililotolewa miaka arobaini iliyopita, likisema kwamba wakatoliki waliojiunga na chama cha freemason hawaruhusiwi kushiriki katika ekaristi takatifu.

Winga Anwar El Ghazi raia wa Uholanzi ameichukulia hatua za kisheria iliyokuwa klabu yake ya Mainz kwa kumsitishia mkataba is
Winga Anwar El Ghazi raia wa Uholanzi ameichukulia hatua za kisheria iliyokuwa klabu yake ya Mainz kwa kumsitishia mkataba isivyo halali. Itakumbukwa mnamo Novemba 2, 2023 miamba hiyo ya Ujerumani ilisitisha mkataba na nyota huyo kutokana na machapisho yake kwenye mitandao ya kijamii kuhusu vita vya Israel na Hamas na kupinga taarifa ya klabu hiyo kuhusu anajutia uamuzi wake.

Andaa ugali Naja na mboga Ila Mimi sitokula nshakula huku tafrijani bae
Andaa ugali Naja na mboga Ila Mimi sitokula nshakula huku tafrijani bae

Selena Gomez,msanii wa Marekani ametangaza wazi kuwa anavutiwa na Msanii,Rema kutoka Nigeria. Gomez alisema alikuwa shabiki w
Selena Gomez,msanii wa Marekani ametangaza wazi kuwa anavutiwa na Msanii,Rema kutoka Nigeria. Gomez alisema alikuwa shabiki wa Msanii huyo hata kabla hawajashirikiana kwenye "remix" ya wimbo wa "Calm Down" kwani alianza kuupenda wimbo wa "Runaway na "Rave Lorde" kabla ya kuwasiliana naye kwaajili ya "remix" ya "Calm Down" .Selena,mwenye umri wa miaka (32) akiwa kwenye mahojiano asema alikubali kufanya kazi na Msanii huyo kwa sababu anapenda tabia yake,akisisitiza kwamba "anataka tu kumtunza." “Nilipokutana naye,kwa kweli nilivutiwa sana na mwenendo wake,jinsi anavyokuwa mnyenyekevu na mwenye shukrani kwa kila dakika" "Na,sikuweza kuchagua mtu mwingine ambaye anastahili mafanikio haya yote ulimwenguni.Yeye ni mkarimu sana Sijui,nataka tu kumtunza." ~amesema Selena.

NDOTO YA KILA MWANAUME
NDOTO YA KILA MWANAUME