E-PLUS MEDIA
الذهاب إلى القناة على Telegram
1 307
المشتركون
+124 ساعات
-27 أيام
-1330 أيام
أرشيف المشاركات
1 307
"Ukitaka uishi muda mrefu na rafiki yako basi usimkopeshe pesa wala msiishi pamoja, ukifanya hivyo vitu viwili lazima mtakosana tu"- Bhoke
1 307
Mange Kimambi atia neno kuhusu Zuchu kutangaza kuachana na Diamond Platnumz.
"We nae ebu tuache, umuache Diamond alafu utaishije kwenye hii dunia? Huna ujanja huo, yani wewe kuachana na Diamond ni siku Diamond atoke hadharani na demu mwingine, ila hata umfumanie na mama yako mzazi haumuachi huyo. Jamani king'ang'a hana issue huyo, mpeni wiki tu kanajirudisha tena kwa machozi"
"Uondoke kwa Diamond ukakonde kama mwenzio Zari? manyimbo yako we na bwana ako yamebuma sababu ya Dah ya Nandy sasa mnatafuta sababu. Eti uondoke kwa Dai? huoni mastaa wenzio wanavyohangaika kulea vimarioo? Hakuna Mwanaume bongo, we si unaona vitoto vizuri kama haviendi chooni kina Paula ila wamekosa wanaume wa maana wameishia kwa kina Marioo, sasa wewe mwenzangu kijuso si utaishia kwa Hamorapa?"- Mange Kimambi baada ya kushtuka usingizini na kukuta Zuchu kaachana na Diamond" - Mange Kimambi.
Ikumbukwe kwamba sakata lilianzia pale Diamond Platnumz alipoonekana kwenye video akiwa Zari wakiwa wameshikana mikono kisha Mume wa Zari akafuta Picha zote akiwa na Zari kwenye ukurasa wake wa Instagram baadaye akaonekana akiwa na Dada mmoja kwenye Gari kwa lengo la kulipiza kisasi. Na muda mfupi uliopita Zuchu nae katangaza kuachana na Diamond Platnumz
1 307
Pichani ni mwanaume mrefu zaidi duniani, Sultan Kosen raia wa Turkey 🇹🇷 mwenye umri wa miaka 41 akiwa na Mwanamke mfupi zaidi duniani, Jyoti Amge raia wa India🇮🇳 mwenye umri wa miaka 30.
Sultan Kosen🇹🇷 ana urefu wa futi 8.3, huku Jyoti Amge🇮🇳 yeye akiwa na urefu wa futi 2 tu.
1 307
"Wafanyabiashara wana option mbili tu, waache kuuza sukari serikali itatafuta option nyingine na wenye viwanda wana option mbili tu wafuate utaratibu wa serikali, hawawezi waache hii kazi na tumewapelekea waraka wa kubadilisha mfumo wa usambazaji haiwezekani mfano Kagera Sugar anamsambazaji mmoja Mwanza na anahudumia mikoa 11 serikali haiwezi kuruhusu, tumewaprotect vya kutosha, mwezi wa sita kwenye Bunge la bajeti napeleka mabadiliko ya sheria kwa ajili ya ku-liberalize biashara ya sukari watacompete na kampuni za kutoka nje, hawa watu tumewaprotect kwa zaidi ya miaka 20 sasa inatosha kama kukua wameshakua," - @bashehussein Waziri wa Kilimo
1 307
Mtoto wa Harmonize, Zulekha anatumia kiasi hicho cha fedha (pichani) kama ilivyowekwa wazi kwenye ujumbe mfupi (sms) wa Mama yake mzazi kwenda kwa Baba Mtu.
1 307
KUTOKA YANGA SC
Wananchi, Afisa habari wetu Ally Kamwe alipata changamoto dakika chache kabla ya mchezo wetu kuisha na kukimbizwa hospitali ya Aga Khan kupata matibabu.
Hivi sasa anaendelea vizuri na yuko salama salmin.
Ally Kamwe Msemaji Wa Yanga
1 307
⚠️ Jamaa huyo kwa jina la Obinna Udenwe kutoka Nigeria ameibuka kueleza tukio lililomshangaza....
"Ngoja nikusimulie kisa cha kushtua lakini cha kusikitisha. Baada ya kusoma haya, utaelewa zaidi ni [uhar-bifu] gani mbaya wa dini zimetusababishia.
Desemba 2023, ndugu wa kiume wa mmoja wa wafanyakazi wangu alianguka kutoka kwenye mti mrefu. Ulikuwa mti mrefu sana, ule tunaouita akputu. Alikuwa amepanda kupogoa/kupunguza matawi mti kwa ajili ya mtu ili alipwe Naira 1,000 (Tsh.1,580).
Baada ya kuanguka akaumia vibaya kwa kuvunjika uti wa mgongo, alihitaji upasuaji. Madaktari walisema hataweza kutembea tena Kwahiyo, upasuaji huo ulikuwa wa kumwezesha tu kukaa wima kwenye kiti cha magurudumu, vinginevyo angelala chali tu, milele. 😌
Mfanyakazi wangu ni fundi ujenzi, alitumia akiba yake yote, kununua dawa na kulipia vipimo vya gharama kubwa kwa ajili ya ndugu yake
Kufikia mwisho wa Januari 2024, nilitaka kujua kwa nini upasuaji haujafanyika, mfanyakazi wangu alisema upasuaji huo utagharimu Naira 1.5 milion (Tsh.2,375,500)
Baada ya kuona jinsi mfanyakazi wangu alivyokuwa akipata tabu akitumia muda wake mwingi hospitalini tangu tarehe 22 Desemba 2023, nilimpa mkopo wa Naira 1.5 milioni. Akiwa na pesa hizo, alirejea hospitalini kuanza mchakato wa upasuaji wa ndugu yake
Wiki mbili baada ya kumpa pesa, mwishoni mwa Januari, niliuliza juu ya ndugu yake, nikidhani kuwa utaratibu umefanywa, nilipata habari ya kushangaza.
Mfanyakazi wangu aliingiza pesa kwenye akaunti ya hospitali, lakini upasuaji haukufanywa. Siku baada ya siku, alienda hospitalini na madaktari waliendelea kuahirisha upasuaji. Alikasirika huku akiwafokea madaktari. Walimwambia kwa nini
Kuweka wazi ni kwamba, ndugu yake, aliyeanguka kutoka kwenye mti ni mfuasi wa imani ya kanisa la Mashahidi Wa Jehovah. Kila siku waumini wa dhehebu hilo walikuja kumwona kijana huyo hospitalini, wakiwa na chakula ikiwemo matunda na mboga mboga za majani zilizopikwa
Waumini wenzie walikataa madaktari kufanya upasuaji kwa kuwa angehitaji kuongezwa damu. Kijana husika aliwaambia madaktari kwamba atakubali kufanyiwa upasuaji huo ikiwa tu hataongezewa damu ya mtu mwingine
Madaktari walikataa wakasema upasuaji husika sio rahisi ni tata na hakuna mtu ambaye angemfanyia upasuaji bila kuongezewa damu
Kwahiyo, ndio maana waumini wa dhehebu lake walikuwa wanaleta matunda na mboga mboga mboga za majani zilizopikwa. Waliamini kwamba akila mboga na matunda ya kutosha angekuwa na damu nyingi sana ambayo madaktari wangeweza kumfanyia upasuaji huo bila yeye kupoteza damu hata kidogo ili asiongezewe damu ya mtu mwingine
Lakini madaktari waliweka wazi kwamba bila kujali kiwango cha damu alichokuwa nacho kabla ya upasuaji bado wangehitaji kuwa na damu nyingine ya ziada karibu kwa ajili ya upasuaji huo wa uti wa mgongo
Mfanyakazi wangu ambaye ni Mkatoliki na yeye alishtuka kwa kuelewa kinachoendelea kuwa imani ya dini ya ndugu yake hairuhusu mgonjwa kuongezewa damu hata kwa matibabu
Mfanyakazi wangu akaenda kwa ndugu yake na kumuuliza kuhusu suala la kufanyiwa upasuaji na kuongezewa damu ambapo mgonjwa alisema ameamua asifanyiwe upasuaji atabaki tu na hali yake ya kupooza kulala chali maisha yake yote
Baada ya hapo mfanyakazi wangu akamkabidhi rasmi ndugu yake kwa waumini wenzie wa Mashahidi Wa Jehovah na kumwacha hospitalini.
Jana ilikuwa wiki mbili tangu akabidhiwe kwa waumini wenzio wa kanisani, bado amekataa kubadili mawazo yake kuhusu kufanyiwa upasuaji uliohitaji kuongezewa damu. Kanisa limemtelekeza hospitalini, kwahiyo kaka yake akarudi hospitalini akapewa ruhusa ya kumchukua kumpeleka nyumbani.
Kwasasa yupo nyumbani, amelalia mgongo na atabaki hivyo hadi Mungu wa Mashahidi Wa Jehovah atakapomponya bila upasuaji.
Inasikitisha! 😌"
1 307
⚠️😳Malia Obama(25) aamua kuliweka pembeni jina lake la ukoo "Obama" baada ya kuingia katika kiwanda cha filamu kama mwandishi na muongozaji ili jina hilo maarufu lisiwe mzigo kwake kikazi ikiwemo kuonekana anabebwa
Kuanzia sasa atatambulika kama Malia Ann jina la Ann ni jina lake la kati
Malia ambaye ni mhitimu wa chuo kikuu cha Harvard, juzi kati filamu yake ya kwanza kutengeneza ambayo ni fupi "The Heart" ni moja ya kazi zilizochaguliwa kuoneshwa katika tamasha maarufu la Sundance Film Festival ambapo tayari pia baadhi ya kazi zake amefanya na Prime Video na HBO huku kampuni husika zikimsifia kwa upekee na juhudi zake kikazi
Malia ni mtoto wa kwanza wa Barack Obama aliyekuwa Rais wa Marekani, wazazi wake baada ya kuondoka ikulu na wao walianzisha kampuni ya kuzalisha filamu, series, documentaries 2018 huku mara kadhaa Obama na mke wake wakionekana wazi kuwa watu wanaoipenda sanaa hasa filamu, muziki na uandishi wa vitabu
1 307
⚠️😳 Kwa hasira na mshtuko Shakib mume wa Zari afuta picha na videos zote alizokuwa na Zari katika insta yake, ni baada ya clip mpya kuonekana Zari akiwa kashikana mikono na Diamond Platnumz wakitembea kwa mbwembwe
1 307
“Mimi ninakula mara Mbili tu kwa Siku. Sio
Kwamba ninataka Kupunguza Uzito hapana, ninataka kinga yangu ya mwili iwe bora zaidi, nisiugue mara kwa mara. Kwa Mfano leo nimekunywa chai kavu asubuhi, mchana nikanywa maji halafu nitakula tena Usiku” Professor Janabi
