E-PLUS MEDIA
الذهاب إلى القناة على Telegram
1 307
المشتركون
+124 ساعات
-27 أيام
-1330 أيام
أرشيف المشاركات
1 307
Wasanii wa muziki kutoka Tanzania Mbosso na Billnass wametozwa faini ya Shilingi milioni tatu (3) kila mmoja na kufungiwa kutokujishughulisha na kazi za sanaa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kwa muda wa miezi mitatu kuanzia Novemba 4, 2023 kisa kushirikishwa kwenye wimbo wa "Ameyatimba" ya Whozu ambao maudhui yake yametafsiriwa kuwa yamekiuka kanuni za maadili.
Kwa upande wake Whozu ametakiwa kushusha mara moja video ya wimbo wake wa "Ameyatimba" kwenye mitandao yote "Digitali platform" huku Baraza hilo la Sanaa Taifa (BASATA) likimtoza faini ya Shilingi milioni tatu (3) na kifungo cha miezi sita (6) bila kujishughulisha na kazi za Sanaa kuanzia Novemba 4, 2023.
BASATA imesema Whozu alichapisha video ya wimbo huo Novemba 2, 2023 akiwashirikisha Wasanii wenzake Mbosso na Billass, na kwamba wimbo huo una maudhui yanayokiuka kanuni za maadili kutokana na kuwepo ishara ya vitendo vinavyoashiria matusi kinyume na Kanuni ya 25(6) (j) pamoja na vitendo ya unyanyasaji, ukatili na udhalilisha wa utu wa Mwanamke kinyume na Kanuni ya 25(6)-(f).
“Msanii huyu ameshaonywa mara mbili na kutozwa faini mara moja huko nyuma kwa kukiuka taratibu za kuzingatia maadili katika kazi za sanaa lakini bado ameendelea kupuuza”
“Baraza limeshatoa na kuzindua mwongozo wa maadili katika kazi za sanaa ambao unapatikana katika tovuti yetu www.basata.go.tz, hivyo ni jukumu la kila Msanii na mdau wa sanaa kuzingatia maadili katika kazi za sanaa” imesema taarifa ya BASATA.
Ukihitaji matangazo ya biashara yako au Promotion ya nyimbo zako, filamu, mitandao yako ya kijamii (facebook na YouTube), njoo inbox 📥
Toa maoni yako
1 307
Hadi raha😊!! Baada ya Sonia kuendelea kufanya vizuri kwenye masomo yake levo ya Chuo Kikuu nchini Netherlands. Huku Tanzania mtoto wa pili wa kiume wa Monalissa nae amefanya sherehe ya kuhitimu kidato cha nne katika shule ya Sekondari Tusiime.
1 307
"Nilikuwa na mpango wa kufungua Media lakini nimetapeliwa hela. Nimetapeliwa Bilioni saba za Kitanzania kwahiyo mchongo wangu wa kufungua Media ukaishia hapo"- Harmonize
1 307
Baadhi ya Wananchi wamefurahishwa na kitendo cha Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba kutotajwa katika Ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwenye kipengele chochote kama amehusika na upotevu hata wa Tsh 1 licha ya wengi kuwa wanamtuhumu.
1 307
Jenifer Kyaka (Odama) ni miongoni mwa wanawake shupavu waliopata tuzo za WISAC hapo jana (BEST FEMALE PRODUCER). Hongera Odama🙏 juhudi zako hazijaanza leo.
1 307
Mtangazaji: Hivi Nani anaekuhamasisha Yaani unaemuiga katika maisha yako ?
Saido Mané : Mtume Muhammad ( Amani ya Mungu iwe juu yake )
Follow ukurasa wetu wa Instagram 👇
https://instagram.com/e_plus_media?igshid=MzNlNGNkZWQ4Mg==
1 307
🚨OFFICIAL: Kuanzia Mwaka 2024, UEFA itaandaa Ballon d’Or ikishirikiana na France Football.
Kwa maana hiyo Tuzo ya Mchezaji bora wa Mwaka wa UEFA (UEFA Best Player of the Year award) haitakuwepo
.
Cristiano Ronaldo na Lionel Messi ndio wachezaji waliotwaa mara nyingi zaidi tuzo ya UEFA Best Player Of The Year. 👏
1 307
KAMA SIO MESSI,NANI ALISTAHILI?
Mkono wa Bernie Snr
Sherehe ilifana sana haswa baada ya Rema kufanya show nzuri iliyonogesha zaidi utamu wa sherehe hizo za ugawaji tuzo. Kama ilivyo ada mastaa kibao walihudhuria sherehe hiyo, tofauti na vipindi vingne kipindi hiki mshindi wa tuzo alijulikana wiki moja kabla.Ilikua ni kama kutimiza ratiba tu kwani kila mtu alijua fika kuwa mshindi wa hiyo tuzo ni nani.
Kimya kilitawala ghafla alikuwa ni David Beckham aliyeunja ukimya kwa kumtangaza Leonel Messi kama mshindi wa Ballon Do'r, ijapokua watu walijua ni nani atashinda lakini hiyo haikutosha kuwaaminisha mpaka pale alipotangazwa rasmi.
Erling Halland alionekana mwenye sura ya unyonge,sura iliyoashiria dhuluma juu yake na upendeleo kwa Leonel Messi.Kichwani alikuwa anajiuliza maswali kuwa kwanini kila siku Messi? Yaani hata pale mtu mwingine anapofanya jambo kubwa na zuri akiwa kwenye timu yake ya Taifa au Klabu basi huwa anangaliwa Messi pekee,Sura ya Haaland ilionesha maneno anayojisemea moyoni.
Mwishoni sura yake ilionesha kumpa majibu kuwa huenda huwa wanaangalia ukubwa wa jina na sio mchango wa mtu husika kwenye timu zake (Ya Taifa na Klabu) kwa msimu husika. Siku moja Mwandishi mmoja wa Habari za michezo alizungumza na Kiungo Fundi, Kelvin de Bruyne Maarufu kama KDB na mazunguzo yalikuwa kama hivi.
Mwandishi: Ni nani alistahili kupewa tuzo ya Ballon Do'r msimu huu?
KDB: Erling anastahili,kwa sababu amefunga magoli mengi msimu huu na amechangia mafanikio ya Manchester City ya msimu huu kwa kiasi kubwa.
Mwandishi: (Akadakia sekunde chache baada ya KDB kumaliza kuongea) Lakini Messi ana kombe la dunia
KDB: Unakumbuka Iniesta alishinda kombe la Dunia mwaka 2010 lakini hakupewa Ballon Do'r?
Mwandishi: Ndiyo, lakini Messi alifunga magoli mengi sana msimu ule.
KDB: Uko sahihi na ndio maana nasema Haaland ndiye anayestahili kwani kafunga Magoli mengi zaidi ya Messi msimu uliopita.Siwezi kushiriki kwenye hii rushwa ndio maana sijaenda kwenye kipazasauti.
Mwaka 2010 wakati Iniesta anachukua World Cup na Spain yake huo msimu Messi alifunga goli 60 huku akiwa na kiwango bora mno , Leo alichukua tuzo kwa kigezo cha magoli yake.
Kipindi hiki Messi anachukua World Cup na Halland amefunga goli 54 huku akiwa na kiwango bora sana Lakini tuzo bado imeenda kwa Leo Messi.Natamani kuona Leo Messi anastaafu soka labda tutaona tena haki ikitendeka.
