E-PLUS MEDIA
الذهاب إلى القناة على Telegram
1 307
المشتركون
+124 ساعات
-27 أيام
-1330 أيام
أرشيف المشاركات
1 307
Mwigizaji Mkongwe kutoka Nigeria Ameachi amefariki dunia jioni ya leo. Siku chache zilizopita Mwigizaji huyo akiwa kitandani hoi bin taabani alisikika akiomba msaada wa kupandikizwa figo baada ya figo yake kufeli.
Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi Amen🙏
1 307
KUTOKA MITANDAONI
Follow ukurasa wetu wa Twitter👇
https://twitter.com/EplusMediaTv?t=OOCtdqDd1L27Uq8rLZ1UJg&s=09
1 307
Haji Manara amjibu Mr Pimbi kwa vitendo
"Mimi na Zainab tulioana Tarehe 24/01/2024 tuna miezi miwili ya ndoa na miezi mitatu mingine ya urafiki plus uchumba na mahusiano.
Haya kiko wapi? Ila Pls Pls msithubutu kumchinja huyu kiumbe, hawa kazi yao ni kutafuta kutrend tu, wala msimkate hiyo shingo, bad luck simjui ila nimeambiwa nae ni Muigizaji.
Asichokijua Mungu ndio mpangaji wa kila kitu no matter wapo Viumbe wa aina hii ambao wanadiriki kutoa hadi Viapo vya hatari, Msameheni yeye na wenzie na muombeeni Mungu aachane na maisha ya watu.
Nawaomba pia msiache kutuombea kheri maana hii nchi imejaa mahasidi kupitiliza hadi ndugu zake @stevenyerere2 wapo 😜" - Haji Manara, Msemaji wa klabu ya Yanga SC.
Toa maoni yako
1 307
"Mimi ni Mchungaji lakini nikiwa nyumbani namvalia bikini mume wangu ili asinichiti kwasababu ukimbania ataenda kuvitafuta huko nje na atavipata"- Mch. Rose Shaboka, Mchungaji.
Toa maoni yako
1 307
"Chanuo bado ni mke wangu, mama watoto wangu na yeye ananitambua kama mume wake, kugombana kupo ukizingatia sisi wote ni maarufu kwahiyo lazima matatizo yetu yawachanganye watu. Ila kwa sasa tuko sawa hayo mengine yaliyonikuta ni sehemu ya uanaume tu misukosuko ni lazima" - Madebe Lidai, Mwigizaji wa filamu Tanzania.
Toa maoni
1 307
MOSCOW, Russia: Rais wa Urusi Vladimir Putin amehutubia taifa leo Jumamosi Machi 23 saa kadhaa baada ya shambulio la kigaidi katika Ukumbi wa Jiji la Crocus mjini Moscow, ambapo watu 115 waliuawa.
Katika hotuba yake, Putin ametaja mambo mengi lakini hapa ni mambo 10 ya muhimu;
1. Kilichotokea katika Ukumbi wa Jiji la Crocus, ni shambulio la kigaidi la umwagaji damu na la kinyama
2. Mamia ya watu wenye amani na wasio na hatia wameuawa katika shambulio hilo la kigaidi katika Ukumbi wa Jiji la Crocus
3. Nina hakika kwamba madaktari watafanya kila linalowezekana na lisilowezekana kuokoa maisha ya wahasiriwa wa shambulio la kigaidi katika Jumba la Jiji la Crocus.
4. Vyombo vya uchunguzi vitafanya kila kitu kufafanua maelezo yote ya shambulio hilo
5. Ni dhahiri kwamba tunakabiliwa na mauaji makubwa ya raia yaliyopangwa
6. Wahalifu walienda kuua kwa kuwapiga risasi Warusi mahali pa wazi, kama Wanazi walivyofanya wakati mmoja.
7. Wahusika wote, waandaaji na wafadhili wa shambulio la kigaidi katika Ukumbi wa Jiji la Crocus wataadhibiwa kwa haki.
8. Tutawatambua na kuwaadhibu kila mtu ambaye yuko nyuma ya shambulio hilo
9. Tunajua tishio la ugaidi ni nini, na tunatarajia kufanya kazi na majimbo yote yanayoshiriki maumivu yetu
10.Magaidi watakabiliwa na adhabu ambayo hawataisahau
-
1 307
KUTOKA MITANDAONI
Follow ukurasa wetu wa Twitter👇
https://twitter.com/EplusMediaTv?t=OOCtdqDd1L27Uq8rLZ1UJg&s=09
1 307
Jackline Wolper amekiri kwamba kwa miezi tisa sasa ndoa yake imekuwa ikipumulia mipira Kwasababu yeye na mume wake hawako sawa tangu mwezi wa sita mwaka jana. Amesema kwa sasa wanalea watoto tu lakini suala la wao kuwa karibu kimahusiano limekuwa likileta mgongano kila kukicha.
Pia Wolper ametengua kauli yake aliyowahi kuisema mwaka jana kuwa hata akimkuta mume wake anachiti na mwanamke mwingine atamuacha au atamvisha nguo kabisa na kumrudisha nyumbani Kwasababu pesa ambayo mume wake anaipata kwa huyo mchepuko inasaidia familia.
Amesema anafuta kauli hiyo Kwasababu aliiongea akiwa amelewa chakali, amesema akimfumania mume wake ndio utakuwa mwisho wa mapenzi yao. Rich ambaye amezaa na Wolper amekuwa na matukio vululu_vululu ya kuhusishwa kutoka kimapenzi na wanawake mbalimbali wa mjini licha ya kuwa na sura ya upole mfano wa kondoo anayekiribia kuchinjwa.
Toa maoni yako
1 307
MZEE WA MJEGEJE APUMZISHWA NA MARAFIKI ZAKE/ NDUGU WAACHWA NJIA PANDA
Baada ya Mvutano Kati ya Ndugu na Marafiki wa Karibu wa Msanii wa Vichekesho Umar Iahbedi Issa almaarufu Mzee wa MJEGEJE wakivutana ni wapi Msanii huyo aa vichekesho AZIKWE
Hatimae Marafiki wamekataa Katu katu Kutoa Mwili wa Msanii Huyo Kwa Ndugu na jioni ya Leo Amepumzishwa Katika Makaburi ya Chango'mbe .
Ikumbukwe Mzee wa MJEGEJE kabla ya Kufariki aliacha Usia kuwa Atakapofariki Azikwe na Marafiki zake na Sio Ndugu zake kutokana na Ndugu Hao kumtenga Katika Kipindi chote Cha Ugonjwa.
Ndugu walitaka Akazikwe Nyumbani kwao Bagamoyo, Pwani
1 307
MAS'HAFU NA MILIONI 100 NACHAGUA MILIONI 100 "DULLA MAKABILA"
"Kati ya MAS'HAFU na Milioni 100 nikiambiwa nichague kimoja nitachagua Milioni 100...sina Imani hiyo ya kukataa Milioni 100 eti kwasababu ya mwezi wa Ramadhan"- Dullah Makabila ameiambia Mashamsham ya Wasafi fm
1 307
UKIWA TAJIRI HAUZEEKI KIZEMBE
Ukiwa tajiri huzeeki kizembe, Wanawake pambaneni kutafuta pesa. Ile kauli kwamba Mwanamke anazeeka haraka kuliko Mwanaume ni uongo. Mwanamke utazeeka mapema kama huna pesa ila kama mzigo upo huwezi kuzeeka.
Ninachowasifu Wanawake wa sasa kiukweli wameanza kujitambua, wengi wameanza kubadili mitazamo yao, hawaamini tena katika kuhongwa na Wanaume bali wanapambana wenyewe kupata pesa.
Pongezi za kutosha ziwaendee Wanawake wote mnaopambana wenyewe bila kutegemea nguvu ya Wanaume.
@hopetygatz
1 307
Rais wa Uganda, Yoweri Museveni amefanya mabadiliko kwenye vikosi vya ulinzi na usalama vya nchi hiyo akimteua mtoto wake wa kwanza, Jenerali Muhoozi Kainerugaba kuwa Mkuu wa Jeshi la Uganda.
Kainerugaba anachukua nafasi ya Jenerali Wilson Mbasu Mbadi aliyeteuliwa kuwa waziri wa biashara.
Mabadiliko mengine yaliyofanywa na Rais Museveni ni pamoja na uteuzi wa Luteni Jenerali Samuel Okiding kuwa naibu Mkuu wa Jeshi akichukua nafasi ya Jenerali Peter Elwelu aliyeteuliwa kuwa miongoni mwa washauri waandamizi wa Rais.
1 307
KUTOKA MITANDAONI
Kwa habari zaidi SUBSCRIBE kupitia YOUTUBE channel yetu kwa ku bonyeza hapa chini.👇.kwenye link
https://youtube.com/@E-PlusMediaTv?si=JjehK80_nkzrHGNK
