E-PLUS MEDIA
الذهاب إلى القناة على Telegram
1 307
المشتركون
+124 ساعات
-27 أيام
-1330 أيام
أرشيف المشاركات
1 307
⚠️😳 Taharuki !! Aliyefariki apiga simu kuwatakia kheri ya mwaka mpya ndugu zake
Familia ya Mzee Masengwa iliopo Kata ya Itenka Halmashauri Nsimbo mkoani Katavi imezua taharuki baada ya ndugu yao wanayedai alifariki dunia na kuzikwa kuonekana akiwa hai baada ya kupigia simu kuwatakia heri ya mwaka mpya
Wakizungumzia tukio hilo ndugu wa marehemu wamesema walipigiwa simu ya kifo cha ndugu yao na rafiki zake aliokua akifanya nao kazi kisha kufika hospitali aliokua akipatiwa matibabu na kuonyeshwa mwili baada ya kuutambua walichukua na kwenda kuzika
"Baada ya hiyo simu tulifika tukapelekwa chumba cha kuhifadhia maiti ndugu yake huyu akaingia kuangalia mwili akatoka akasema ni yeye ila anasema mwili ulikua umeharibika sisi tukabeba kwenda kuzika. Siku ya mwaka mpya, Masanja aliyefariki akapiga simu kututakia heri ya mwaka mpya kwakweli tuliogopa sana tukasema amefufuka hatukuamini akasema mimi sijafa nilikua kijiji ambacho hakuna mtandao nilikua sipatikani," amesema shemeji yake Doto Shilinde
Mwenyekiti wa Kijiji cha Itenka, Misungwi Mikoba amesema familia hiyo ilizika mwili ambao sio wa ndugu yao huku akidai hakuna mtu aliefufuka katika kijiji chake kama inavyodaiwa
Source: Nipashe
1 307
***Morgan Freeman mwenye umri wa miaka 86 na Enzi Zile**
**Ni filamu ipi unayoipenda zaidi aliyoshiriki?**
1 307
***DALILI NYINGINE YA UMASIKINI NI KUTUMIA MSWAKI ULIOKUWA UNAPIGIA MWAKA JANA*** 😁😁😁😁😁😁
#Vijimambo...
1 307
UNAIKUMBUKA FILAMU YA JOTO LA ROHO YA JENIFER MGENDI NA BAHATI BUKUKU? HII HAPA
Mwaka 2005 kama sio 2006, wengi wetu tukiwa wadogo na wengine mkiwa vijana wa enzi hizo, ilitoka Filamu ya (Joto la roho) ambapo ndani kuna washiriki kadhaa lakini zaidi walitazamwa Jenifer Mgendi na Bahati Bukuku ambao ndio walikuwa top in Tanzania kwa kipindi hicho.
Mtunzi na Mwandishi wa Filamu hiyo ni Jennifer Mgendi, mpiga picha ni Salum Mchome lakini mtayarishaji akiwa ni (GMC Wasanii Promoters LTD). Filamu inamuelezea Datti (Jennifer Mgendi) kama mwanamke ambaye yupo kwenye kipindi cha ujana haelewi anataka nini, licha ya familia yake kuwa walokole sana lakini yeye alikuwa wa tofauti, hali inayomfanya akutane na rafiki wa hovyo ambaye anamuunganisha na mwanaume wa hovyo.
Pasipokujua, Datti anajikuta anaingia kwenye mikono ya mwanaume jambazi sugu (Mikka), anafundishwa kunywa pombe lakini mwanaume huyo jambazi anafanikiwa kuutoa usichana wa Datti, anamdanganya kuwa anataka kumuoa na anafanya kazi ya kuuza magari na anamiliki maduka makubwa ya nguo. Kwa tamaa za pesa Dati anafanikiwa kuishawishi familia yake wamkubali aolewe na Mikka na mwisho familia inakubali japo kishingo upande na hatimae mchungaji anawafungisha ndoa kwa kigezo cha kuokoka.
Ndoa ikiwa changa tu, Datti anagundua kuwa mume wake anamiliki bunduki, anapomuuliza anamjibu kuwa anamiliki kwasababu inamsaidia katika kazi zake kisha anamkanya asimuulize kuhusu kwenda kanisani tena, baadae Datti anaenda kucheki afya hospitalini na kwa bahati mbaya anajikuta ameathirika ana Virus vya UKIMWI, na hapo unazaliwa wimbo pendwa wa (Nalia). Baadae Mikka anaambiwa akacheki afya ili aangalie pia kama ameathirika, lakini anakataa kwasababu anajua yeye ndiye aliyemuambukiza Datti.
Anapoendelea kusisitizwa akapime, Mikka anakasirika anamnasa kibao cha shavu Datti, jambo ambalo linamfanya Datti arudi nyumbani kwa wazazi wake kuwaomba msamaha, baadae familia inagundua kuwa Mikka ni jambazi sugu, na wanaishia kuangua kilio cha familia, Datti anafanikiwa kutulia baada ya kufunzwa na dunia lakini tayari ni muathirika.Tuishie hapa, Filamu hii kwa miaka hiyo ilikonga mioyo ya watu wengi, ilikuwa na funzo kubwa kwasababu kipindi hicho ndio gonjwa la UKIMWI lilikuwa limeshika kasi.
Sasa hivi ukiitazama utagundua ni Filamu ambayo ilikuwa na makosa mengi sana, kuanzi waigizaji, sauti n.k lakini kwa kipindi hicho ilikuwa ni zaidi ya dhahabu, tupate wapi tena Filamu ya aina hii, (Joto la roho).
1 307
"Nashukuru Mungu nimeumbwa Mwanamke, hivi ningetolea wapi nguvu za kumpa mtu hela mimi"- Kidoa Salum (Tima).
1 307
"Unapoenda kumfariji mfiwa angalia maneno ya kuzungumza ili usimuachie maumivu zaidi badala ya faraja, unakuta mtu umeenda kumfariji mfiwa unaanza kumwambia ooh (usijali Mungu atakupa mtoto mzuri zaidi huenda huyo hakuwa fungu lako), (Muache aende muachie Mungu maana hawa wanaume huwa wanabadilika huenda angekuja kukuumiza baadae utapata mume mwingine)"
"(Acha kumuwaza sana muache aende maana yeye sio wa kwanza kufariki), (Usijali utazaa watoto wengine). Hayo sio maneno ya kumwambia mfiwa, mtu anayepitia maumivu, mtu anayeumia kwa kumpoteza mume/mtoto/ mzazi/rafiki yake, wewe unamwambia habari za kupata mwingine, unajuaje kama atapata mwingine? wewe ni Mungu? je kama Mungu alimpatia kizazi cha mtoto huyo huyo?"
"Mwambie mwenzako maneno mazuri, mwambie pole utavuka salama, utavuka taratibu, muonyeshe mifano ya watu waliopita kwenye majaribu mkubwa kisha wakashinda, mwambie fulani alipitia kitu flani lakini leo yuko ngangali na wewe utashinda, tuwe makini sana tunapoongea na wafiwa"- Jenifer Mgendi
1 307
MWIJAKU AJIZAWADIA JUMBA LA BILIONI 1.3 KATIKA SIKU YAKE YA KUZALIWA.
Ikiwa leo anatimiza miaka 39, Mwijaku amejizawadia jumba hilo lenye hadhi yake ambalo lina thamani ya Tsh Bilioni moja na milioni 300.
Katika maelezo yake Mwijaku amesema alinunua kiwanja mwaka 2022, alianza kujenga mwezi Machi 2023 na akamaliza ujenzi Oktoba 2023, na leo ameamua kuizindua, tayari kwa kuanza kuishi yeye na familia yake.
1 307
"Nyimbo zangu sio za kulalamika kama watu wengine wanavyodhani, mimi naimba nyimbo za kutia moyo, namlenga yule mtu aliyekata tamaa, aliyevunjika moyo, anayepitia kwenye majaribu. Nilipoimba Naiona Kesho na Nifundishe kunyamaza nilibariki mioyo ya watu wengi"
"Zile nyimbo ziligusa mamilioni ya watu, kuna walionipigia simu kuwa umejuaje kama napitia kwenye kipindi kigumu. Kwahivyo silalamiki ila naimba nyimbo zenye kuleta faraja na matumaini kwa waliokata tamaa"- Martha Mwaipaja
1 307
"Juzi kati hapa nilikutana na rafiki yangu wa muda mrefu ambaye tulisoma wote shule moja, kiukweli nilishindwa kumtambua kwa haraka kwasababu alikuwa amechoka sana, amebadilika amekaa kama mtu aliyechanganyikiwa. Nikamuita pembeni tukakaa kisha nikamuuliza nini kimemkuta hadi kupelekea awe katika hali ile, akasema yeye na wenzake walienda kwa mganga ili wawe matajiri na masharti waliyopewa ni kuwatoa kafara wazazi wao (mama zao)"
"Walikubali masharti wakala viapo kwamba wakishindwa kutimiza masharti wao ndio watakufa, kwa bahati mbaya/nzuri wale mama zao walikuwa na imani mnoo, mmoja alikuwa mama wa Kikristo na mwingine mama yake alikuwa wa Kiislamu na wote walikuwa watu wa maombi kwahivyo maombi yao yakazizidi nguvu za giza, jambo lililopelekea wale vijana kushindwa kutimiza masharti na kama kawaida, waliambiwa wakishindwa watakufa wao, na kweli walikufa"
"Akasema yeye pekee ndiye aliyebaki hajui lini atakufa, ila kwa kumtazama tayari alikuwa amechanganyikiwa anatapatapa. Kiukweli niliumia sana. Ninachoweza kuwashauri vijana ni kwamba kijana usiwe na tamaa ya kufanikiwa haraka, kila kitu ni hatua kwa hatua, usione watu wanaonyesha maisha mazuri huku mtandaoni ukatamani kumbe haujui wanayopitia nyuma ya Pazia, pesa bila amani haisaidii, msiharakie maisha"
"Mimi mwenyewe kuna kipindi niliwahi kuwa na pesa nyingi lakini hazikunisaidia kwasababu sikuwa na amani kwa wakati huo, usitamani kuwa mtu fulani tamani kuwa wewe ipo siku utafanikwa, hii sio movie ni kweli"- Irene Uwoya
1 307
Ajali imetokea Ipuli mkoani Tabora barabara kuu ya Tabora Nzega bajaji kugonga gari la mafuta uso kwa uso hakuna maafa ila chanzo ni matumizi ya simu wakati anaendesha chombo cha moto.
Usitumie simu wakati unaendesha chombo cha moto!!
Cc:
RSA Tanzania
1 307
Kim Jong Un, Kiongozi wa Korea Kaskazini akiwa na bintiye walitembelea kiwanda cha kutengeneza makombora na kuingia kwenye mojawapo ya sehemu ya makombora hayo.
Kiongozi huyo wa Korea Kaskazini na bintiye walivaa mavazi yaliyofanana walipokuwa wakitembelea kiwanda cha kutengeneza makombora.
Yeye na binti yake, aitwaye Kim Ju Ae - ambaye anadaiwa na wengi kuwa huenda akamrithi Kim - wote walikuwa wamevalia mavazi meusi walipokuwa wakipita kwenye kituo cha kijeshi, picha zilizotolewa Alhamisi na vyombo vya habari vya Serikali ya Korea Kaskazini.
Kim ametoa wito wa kuimarishwa kwa utengenezaji wa magari mbalimbali ya kurusha makombora. Katika mkutano na maafisa wa chama tawala nchini humo wiki iliyopita, Kim alisema Korea Kaskazini itapanua juhudi za ushirikiano na nchi "zinazopinga ubeberu" huku ikijitayarisha kwa vita, shirika la habari la serikali KCNA liliripoti.
1 307
TUKUMBUSHANE KIDOGO KUHUSU HAPPINESS MAGESE
MISS TANZANIA WA MWAKA 2001,
Madogo wa miaka ya 2000 hii wanaweza kuibishia,
Kwanini???
Kwa sababu hawaamini kama kuna warembo zaidi ya Wema Sepetu walilivaa taji la Miss Tanzania,
Wanaamini Wema Sepetu ndio mrembo bomba kuwahi kutokea kwenye shindano la Miss Tanzania, kwa sababu alishinda taji hilo mbele ya warembo kama Jokate Mwegelo, Lisa Jensen, Irene Uwoya na wengineo,
Oya sasa ngojeni niwaambie, hakuna shindano la Miss Tanzania ambalo lilikuwa na ushindani kama la mwaka 2001,
Kulikuwa na warembo wawili ambao waliiteka nchi na kuwagawa watu kimakundi, hapa namuongelea Happynes Magese na Miriam Odemba...
Wadada hawa walikuwa ni moto ule wa kuotea mbali kabisa, na kila mmoja alikuwa na kigezo cha kulitwaa taji la Miss Tanzania, hakika kazi ilikuwa kazi kweli kweli,
Kwanini???
Happynes Magese aliamini kuwa yeye ndiyo ataibuka mshindi wa taji la Miss Tanzania,
Vivyo hivyo hata kwa Miriam Odemba, hata Mashabiki pia tulijigawa kimakundi mawili,
Wapo walioamini taji hili ni la Happynes Magese, na wengine waliamini taji hilo ni la Miriam Odemba, Lakini siku ya shindano matokeo yalikuwa tofauti kwa Timu Miriam Odemba, kwani mrembo wao hakuweza kufurukuta kwa Happynes Magese, Mrembo ambaye alitokea wilayani Temeke, Happynes Magese aliibuka mshindi, na baadaye kuja kuwatingisha na washikiri kutoka barani Afrika kwenye Miss World ambayo ilifanyika nchini Afrika Kusini.
Hata mshindi wa Miss World aliyetokea Nigeria, Agbani Darego alikiri kuwa mwanadada Happynes Magese ndiye ambaye alikuwa tishio lake.
Sina mengi ya kumzungumzia,
lakini kama ukitaka nimzungumzie , basi nitakwambia Mrembo huyu baada ya kumaliza mwaka wake mmoja alipata kazi kwenye Kampuni ya Mitindo ya Elite nchini Afrika Kusini kisha kuzunguka nchi mbalimbali duniani kabla ya kuhamia Marekani. Baada ya hapo alibadilisha jina na kujiita Millen, sasa sijui bado anaendelea na kazi za unamitindo???
Naamini kuna wengine wenye kumjua Happynes Magese, karibu katika ulingo wa maoni kunijibu Happynes Magese bado yupo kwenye mitindo??? au alishatoka huko na sasa anaendelea na Shughuli nyingine....
1 307
Wakija vibaya wanakaa
Wambea vikao watakaa
Mauwaki nafasi ya kuongea siwapi waga nawanyanyapaa
Nimewapa nafasi ya kunijua jina wakataka na ninapokaa
Leo napendwa sabab nnachokikosa habari zitatapakaa
Kung'aa ndio zetu
#fimbooo
1 307
Mwanamuziki kutoka Nchini Senegal 🇸🇳, Youssou N'Dour bado anashikilia nafasi ya kwanza kwa Wasanii wenye utajiri mkubwa barani Afrika kwa mwaka huu 2023. Kwa mujibu wa Forbes, N'Dour anakadiriwa kuwa na utajiri wa Dola milioni 145 za Kimarekani.
1. Youssou N'Dour 🇸🇳 (Milioni 145)
2. Akon 🇸🇳🇺🇸 (Milioni 80)
3. Black Coffee 🇿🇦 (Milioni 69)
4. Wizkid 🇳🇬 (Milioni 30)
5: Davido 🇳🇬🇺🇲 (milioni 28)
6. ASA 🇳🇬 (milioni 28)
7. Don Jazz 🇳🇬 (milioni 18)
8. Burna Boy 🇳🇬 (milioni 17)
9. 2FACE Idibia 🇳🇬 (milioni 16)
10. Rude Boy 🇳🇬 (milioni 16)
11. Timaya 🇳🇬 (milioni 14)
12. Mr P 🇳🇬 (milioni 12)
13. DBanj 🇳🇬 (milioni 12)
14. Diamond Platnumz 🇹🇿 (milioni 10)
15. Sarkodie 🇬🇭 (milioni 9.5)
NB : Pesa hizo ni kwa thamani ya Dola ya Kimarekani ambapo kwa thamani ya Pesa ya Nchi yako, utachukua kiasi cha Msanii kisha (×) na Pesa ya Nchi yako, utapata kiasi hicho cha Pesa kwa thamani ya Nchi yako. Mfano 143×2500 (Tanzania)
Toa maoni yako
1 307
WaTu wa Moshi Ndo Wanarud DAR sasa 😁😁🙌 Apoo walienda Kijjini na MIKATE Miwili, na Carton la Soda 🙌🙌😁
