ar
Feedback

لا تقع ضحية للمخادعين! تيليمتريو يكتشف ويُميّز هذه القنوات 👉 إذا كنت تريد رؤية العلامة، اشترك

E-PLUS MEDIA

E-PLUS MEDIA

الذهاب إلى القناة على Telegram

Get the latest news,videos,and more everyday.

إظهار المزيد
1 307
المشتركون
+124 ساعات
-27 أيام
-1330 أيام
أرشيف المشاركات
⚠️ Wanaojihusisha na kiwanda cha kutengeneza biskuti za bangi watiwa mbaroni Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kul
⚠️ Wanaojihusisha na kiwanda cha kutengeneza biskuti za bangi watiwa mbaroni Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini DCEA imekamata watu wanaojihusisha na shughuli za utengenezaji wa biskuti kwa kuchanganya na bangi aina ya skanka katika eneo la Kawe Jijini Dar es Salaam. Kamishna Jenerali wa DCEA Aretas James Lyimo amesema watuhumiwa hao wamekutwa wakiendelea na uzalishaji wa biskuti hizo kwa kutumia mtambo mdogo wa kusaga skanka na vifaa vya kutengenezea biskuti hizo za bangi ya skanka. Kutokana na operersheni hiyo watu 16 wamekamatwa na Kilogramu 423.54 za bangi iliyosindikwa ya skanka yenye kiwango kikubwa cha sumu ya TetraHydroCannabinol THC ambapo asilimia 75 ikizalishwa kutokana na bangi aina ya Sativa na asilimia 45 bangi ya Indica ikiwa na sumu zaidi ya asilimia 45 ikilinganishwa na asilimia 3 hadi 10 zilizo katika bangi ya kawaida Credit: Clouds TV

Kwenye asilimia 10% unampa asilimia ngapi za umaridadi wa kuigiza mwingizaji Taiya Odero?
Kwenye asilimia 10% unampa asilimia ngapi za umaridadi wa kuigiza mwingizaji Taiya Odero?

Shamsa Ford alipojaribu kuuva muonekano wa Mama muuza genge.
Shamsa Ford alipojaribu kuuva muonekano wa Mama muuza genge.

C E O.Mstaafu wa Klabu ya Simba SC Barbara Gonzalez anatajwa kuwa ndie Mwenyekiti Mpya wa Bodi ya Wakurugenzi ya Klabu ya Sim
C E O.Mstaafu wa Klabu ya Simba SC Barbara Gonzalez anatajwa kuwa ndie Mwenyekiti Mpya wa Bodi ya Wakurugenzi ya Klabu ya Simba sc 🦁 #Tetesi

Mwanaume anaekupenda ndie mwanaume atakaekupa furaha ya kweli. Mwanaume anaekupenda ndie atakae kuvumilia. Mwanaume anaekupen
Mwanaume anaekupenda ndie mwanaume atakaekupa furaha ya kweli. Mwanaume anaekupenda ndie atakae kuvumilia. Mwanaume anaekupenda atakujali hata kama hana kitu mfukoni. Usichokijua wanaume wenye mapenzi ya dhati huwa kawaida sana hana mambo mengi. Abdulrazaki issa. Follow Ukurasa Wetu wa Instagram 👇 https://instagram.com/e_plus_media?igshid=MzNlNGNkZWQ4Mg==

SIMBA IKISHINDA NI YA MO DEWJI, IKIFUNGWA NI YA MANGUNGU. Simba SC tangu baada ya kubondwa 5-1 na Yanga wameendelea kuweweseka, wamefukuza makocha wawili lakini bado kuna shinikizo kutoka nje kwamba viongozi waondoke pia. Katika viongozi wanaotajwa na wengi kutaka waondoke ni Mwenyekiti wa Simba SC Murtaza Mangungu wala sio Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Salim Abdallah Muhene ‘Tryagain’ au MO DEWJI. Nimetafakari kidogo tu kwanini kwenye hili jambo baya anatakiwa Mangungu kuondoka na sio MO Dewji na kwenye mambo mazuri kote anaonekana MO Dewji au mwakilishi wake Tryagain na sio Mangungu? Ukimuona Tryagain ndio umemuona Mo Dewji kwakuwa SALIM anatokana na upande wake na ukimuona Salim ndio umemuona MO Dewji kwakuwa ndiye aliyemteua. Wakati wa usajili MO yeye mwenyewe au kupitia Salim atasema ametoa kiasi gani kusajili msimu huu na watu watafurahi sana na kumsifia, timu ikifanya vibaya au usajili kubuma anatajwa Mwenyekiti wa Simba Mangungu kwanini amemsajili Onana kwa mfano. Simba Day waliokuwa karibu na Rais na pengine hata kuongea ni Salim na MO Dewji, Mangungu hakuonekana sana na hakuna aliyejali. Ikaja African Football League, Rais wa CAF Dr Patrice Motsepe akamtambulisha MO Dewji kama Mwenyekiti wa Simba na watu wote wakafurahi ilihali Mwenyekiti yupo na hakutambulishwa na hakuna aliyejali. Leo timu imekula mbao 5 watu wanamtaka Mangungu apishe na sio aliyetambulishwa pale kwenye steji ya AFL. Labda Simba watuambie kuanzia leo ni wakati gani Mangungu anakuwa Mwenyekiti wao na wakati gani au kwenye matukio yapi anakuwa sio Mwenyekiti? Kinyume chake ni kumuangushia jumba bovu tu. Kama huko nyuma walikosea kutolisema hili kikatiba au kwa kulitolea maelezo sio vibaya wakasema hata sasa kwakuwa muda wanao, vinginevyo watakuwa wanachanganya watu wenye uwezo wa kuchanganua mambo. Ukimuona Mangungu vyovyote alivyo leo ni kutokana na katiba yao wakati wanafanya marekebisho kumuingiza muwekezaji, walipoambiwa wanapokosea majibu yalikuwa rahisi tu “tunataka furaha na timu inashinda ndiyo furaha yetu” leo wanapigwa wanataka nguvu za Mwenyekiti wao ambazo hazipo kikatiba, huwezi kula keki ukaimaliza yote kisha ukabaki nayo mkononi. @jemedarisaid .

photo content

Et wale mlikuwa mkisema amkuwahi kuliona sheli apa niwapi 😂😂😂😂
Et wale mlikuwa mkisema amkuwahi kuliona sheli apa niwapi 😂😂😂😂

Kufuatia agizo la mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamila kuwataka wamiliki wa nyumba zinazofanya biashara haramu ya k
Kufuatia agizo la mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamila kuwataka wamiliki wa nyumba zinazofanya biashara haramu ya kuuza miili ya watu, kuvunja nyumba hizo mwitikio umeonekana mkubwa huku wamiliki wa nyumba hizo wakiomba serikali kutoa muongozo wa mapema kwenye maeneo hayo ili yasiweze kutumika na wahalifu. EATV imefika na hapa baadhi ya nyumba na kushuhudia asilimia kubwa ya nyumba zikiwa tayari zimeezuliwa Mapaa na hapa wamiliki wa nyumba wanaelezea. Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Albert Chalamila, November 3, alifika kwenye eneo la madanguro na kutoa maagizo ya ubomoaji wa nyumba hizo.

Waziri wa Miradi wa Saudia Asema: "Nia yakuwa na mahusiano ya amani na Israel bado iko kwenye meza." "Hatuta tumia mafuta kam
Waziri wa Miradi wa Saudia Asema: "Nia yakuwa na mahusiano ya amani na Israel bado iko kwenye meza." "Hatuta tumia mafuta kama chombo cha kuwatia adabu wamagharibi." "Bado tuna mahusiano mema na Amerika." Moja ya matokeo ya wazi kabisa ya jihadi huko Palestina kama ilivyotokea pia wakati wa vita vya Mtume صلى الله عليه وآله وصحبه وسلم ni kuwaweka hadharani wanafiki wanaomfanyia khiyana Mwenyezi Mungu, Mtume wake na Umma wa Kiislamu!!!

Nadhani wahenga wenzangu mnaikumbuka hii MOVIE...Mwamba anaitwa SOLO, Jina lake halisi ni MARIO VAN PEEBLES ambae alizaliwa 1
+1
Nadhani wahenga wenzangu mnaikumbuka hii MOVIE...Mwamba anaitwa SOLO, Jina lake halisi ni MARIO VAN PEEBLES ambae alizaliwa 1957....Sehemu niliyokuwa naipenda katika movie hii ni pale alipochukua Sigara na kuivuta ili ajifunze kucheka kama wale watu wengine😆😆

*RAIS MUSEVENI: NCHI ZA MAGHARIBI ZINAJIONA BORA KUPITA KIASI* Rais wa Uganda, Yoweri Museveni ametoa kauli hiyo kwa kuonesha
*RAIS MUSEVENI: NCHI ZA MAGHARIBI ZINAJIONA BORA KUPITA KIASI* Rais wa Uganda, Yoweri Museveni ametoa kauli hiyo kwa kuonesha kutokuwa na wasiwasi kuhusu kuondolewa kwa Nchi yake katika mpango maalum wa Kibiashara wa Marekani na Afrika (AGOA) Museveni ameikosoa Marekani akisema "Wanajiona bora kupita kiasi na wanafikiri Nchi za Afrika haziwezi kusonga mbele bila uungwaji mkono wao. Tuna uwezo wa kufikia malengo yetu ya ukuaji na mabadiliko, hata kama hawatuungi Mkono"

Hapa Ndio Nyumbani Kwa Mheshimiwa Spika Wa Bunge Mh.Tulia Ackson.
Hapa Ndio Nyumbani Kwa Mheshimiwa Spika Wa Bunge Mh.Tulia Ackson.

✍️ “Ukweli usemwe, ushindi wa bao tano dhidi ya mtani si kila timu inaweza. Hii ndo Yanga ya Dkt Samia, Tupewe maua yetu, na
✍️ “Ukweli usemwe, ushindi wa bao tano dhidi ya mtani si kila timu inaweza. Hii ndo Yanga ya Dkt Samia, Tupewe maua yetu, na huu ndio mwendo wetu mpya. Hongereni sana Wananchi kwa ushindi wa kishindo dhidi ya mtani.” WAZIRI WA Fedha Dkt Mwigulu Nchemba.

"Hata vitabu vya dini vinatuelekeza kuwalea watoto katika maadili mazuri, ukimzoesha mtoto nyimbo za mapenzi kama zile mtoto
"Hata vitabu vya dini vinatuelekeza kuwalea watoto katika maadili mazuri, ukimzoesha mtoto nyimbo za mapenzi kama zile mtoto anakuwa hajui na ndiyo maana muda mwingine tunawadhibiti kwamba nyimbo hizi msiangalie au muvi, tunajaribu kulinda maadili yao wakiwa wadogo" - Mwalimu George

Mkuu wa Mkoa wa Mara Ndugu Said M. Mtanda ametuma salamu za pole kwa familia ya kijana Girimoru Sindano miaka 36 Mkazi wa Kij
Mkuu wa Mkoa wa Mara Ndugu Said M. Mtanda ametuma salamu za pole kwa familia ya kijana Girimoru Sindano miaka 36 Mkazi wa Kijiji cha Iharara Wilayani Serengeti kufuatia kifo cha kijana huyo. Kifo kilichotokana kufuatia furaha aliyoipata wakati Timu ya yanga ilipopata goli la tatu dhidi ya Simba alinyanyuka na kushangilia kwa nguvu akiwa amenyanyua mikono juu na kukauka ghafla kwa mshtuko na mara baada ya kuketi chini alifariki.

UKIWA KONDE GANG NI SAWA NA KUUKALIA UMASIKINI, BOSS NI BAHILI KWA WASANII WAKE HATA IBRAH ANATAKA KUTOKA; ANJELLA. Kwenye mo
UKIWA KONDE GANG NI SAWA NA KUUKALIA UMASIKINI, BOSS NI BAHILI KWA WASANII WAKE HATA IBRAH ANATAKA KUTOKA; ANJELLA. Kwenye moja ya sauti inayozagaa Kwenye mitandao ya kijamii ambayo ni sauti ya Mwanamuziki Anjella imeleta gumzo baada ya Anjella kuyafichua ya sirini ambayo hakuwahi kuyasema popote tangu atoke Konde Gang. Anasema maisha ya Konde Gang ni maisha magumu mnoo, ni maisha ambayo huwezi kutamani kuyarudia mara ya pili ikiwa ulifanikiwa kutoka kwa mara ya kwanza kwasababu ukiwa Konde Gang ni sawa na umeukalia umasiki na hiyo inatokana na ubahili wa kupitiliza alionao Harmonize ambaye ndiye Boss wa lebo hiyo. Anjella amesema Harmonize ni mwepesi wa kuhonga wanawake kuliko wafanyakazi wake, yupo radhi kumhonga mwanamke pesa nyingi huku wasanii wake wakikoroma kwa kukosa chakula na hiyo inatokana na kupenda sana ngono. Amesema kutokana na hali hiyo hata Ibrah yupo mbioni kung'ooka kwenye lebo hiyo na siku si nyingi mtaona amepotea kisha zitakuja taarifa kwamba ameondoka Konde Gang.

NIMEFANYA SURGERY YA KUONDOA UUME NA KUBANDIKA UKE KWA FAIDA YANGU, WATANZANIA ACHENI KUNIOMBEA KIFO NINA MUNGU KULIKO NYIE; DAYON Njemba huyo pichani ambaye ni Mtanzania na mkazi wa Arusha ingawa kwa sasa anaishi nchini Canada amewashangaza watu baada ya kubadili jinsia kutoka kwenye uanaume na kuwa mwanamke, tukio zima la kufanya mabadiliko hayo linapatikana kwenye Mange Kimambi App. Baada ya Watanzania wengi kulaani kitendo hicho, Dayon amewashukia na ujumbe huu. "Aisee huku nilipo nikisema nimetokea Tanzania kitu cha kwanza watu wanasema ni nchi yenye upendo, siku zote nimekuwa nikijifurahia kusema natokea Tanzania. Ila kiukweli kabisa Watanzania mlioko huku Instagram sijui sio Watanzania ama sijui" "Mimi nimeonyesha safari yangu ya kuwa mtu niliyetamani kuwa toka nikiwa na miaka 7, 8 hadi ukubwani nilitaka kuwa mwanamke siyo kwasababu ya pesa, kwetu kila kitu tulikuwa navyo tayari. Mimi nimezaliwa Tanga mama akiwa mfanyakazi wa Serikali tena anayemfuata boss wa bandari ya Tanga, mama yangu amenifunza kupenda watu na kuwaheshimu hata kama ni wezi, nimetoka kwenye familia ya upendo maisha yalikuja kubadilika baadae ila haikunibadilisha mimi" "Maamuzi niliyofanya ya kufanya surgery ya kuondoa uume na kubandikwa uke ni maamuzi yangu binafsi siyo maamuzi ya taifa wala maamuzi yenu, na kama ikiwa mbaya ni mimi ndio nita suffer sio nyie, sasa why mnachukizwa na mtu ambaye hamumjui? Kuna wengine hadi wananiombea kifo eti Mungu aje aniue, mimi nipo karibu sana na Mungu, Mungu huyu alinitoa mahabusu ya Monduli na kuninyanyua na niko hapa na wale wote walio tekeleza ubaya nifungwe walikosa kazi zao na wengine kushushwa vyeo na uhamisho" "So jueni Mungu anafanya kazi tofauti, alafu huyu Mungu kanitoa huko na kunileta huku na kanipa nafasi nyingine kimaisha, so watu jueni mimi huongea na Mungu kila siku kabla ya kufanya jambo lolote. Nilimuomba Mungu naomba upasuaji wangu usiwe na complications na ikawa hivyo hivyo, ninapona na ninapona tena🙏 alafu nyie mko bize mnampangia Mungu aniue, Mungu akawafunge midomo yenu na azidi kuwabariki, mimi siombei mtu ubaya hiyo ni kazi yake Mungu"- ameandika Dayon ambaye anaishi nchini Canada.

photo content

SIJAOZA MAKALIO NA MATITI, PUUZENI TAARIFA ZA UONGO; NICOLE. Baada ya kuwepo kwa taarifa kwamba amechangiwa pesa na watu wa Tamthilia ya Huba na yupo Nigeria anafanyiwa surgery ya makalio yake ambayo yanamsumbua sana kutokana na Silcon kuachia na kuanza kusumbua, Nicole amejibu madai hayo. Kwa mujibu wa mdaku alisema kwamba mpaka sasa Nicole yuko hoi bin mahututi. Sababu kubwa ya ugonjwa wake ni Silcon za makalio na matiti kuisha muda wake na waliomchangia pesa za matibabu ni watu wa Tamthilia ya Huba. Sasa Nicole amekanusha taarifa hizo na amesema yuko salama kabisa, ni kweli yupo nje ya nchi lakini sio kwamba anaumwa, ameenda kula good time na mpenzi wake. " Hivi kweli mimi ndo wakuchangiwa pesa ya matibabu? Yaani watu na akili zao waache kufanyia pesa zao vitu vya maana wahangaike kunichangia pesa nikatibiwe tak*!! hamna akili nyinyi eeeh. Mimi ambaye nalipa zaidi ya laki nane kwa siku mahali ninapolala leo hii nichangiwe pesa? Mimi ni miongoni mwa mastaa wanaoishi vizuri Tanzania na hata nikiwa huku nje ya nchi " "Nikiwa Tanzania naishi gorofani na chini nimepaki ndinga na nikiwa huku nchi za watu naishi gorofani na pia chini nimepaki ndinga, mnaoniombea niumwe mtangoja sana, viungo vyangu viko sawa havina shida puuzeni taarifa za wasionipenda"- amejitetea Nicole