E-PLUS MEDIA
الذهاب إلى القناة على Telegram
1 307
المشتركون
+124 ساعات
-27 أيام
-1330 أيام
أرشيف المشاركات
1 307
🚨BREAKING; MKUDE AWEKA RECORD MPYA
Jonas Mkude amekuwa Mchezaji wa Kwanza Ambaye timu Yake imeshinda kwenye #KariakooDerby
ℹ️Akiwa na Simba Mei 6, 2012 Simba Walishinda 5-0.
ℹ️Akiwa na Yanga November 5, 2023 Yanga Wameshinda 5-1.
1 307
UNAPOCHEZA dhidi ya Yanga sio rahisi kumjua atakayekufunga.MASTER GAMONDI ameitengeneza timu kwa namna ambayo kila Mchezaji kwenye Kikosi chake anaweza kufunga kwa namna yoyote ile na kwa wakati wowote ule (TOP CLASS COACHING 👏🏿👏🏿)
KABLA ya kuwafunga YANGA.....Anza Kwanza kushindana na GAMONDI Kisha malizana na na wachezaji wote wa ndani.Ukiwaweza hao ....Basi utawafunga.
KOCHA WA BOLI 🔥🙌🏿
1 307
Ukipanga Kikosi chako Langoni anakaa nani kati ya hawa?
A: Aishi Manula
B: Ally Salim
1 307
Kikosi cha Yanga kilikuwa cha kwanza kufika Uwanja wa Mkapa huku wenyeji wao Simba wakiwafuata kwa dakika mbili baadae.
Yanga licha ya kuwahi kuingia wakipitia geti kubwa la kawaida saa 9:08 alasiri ila wameingilia njia tofauti na iliyozoeleka kwenda kwenye vyumba vya kubadilishia nguo.
Mabingwa walitumia mlango wa karibu na njia ya kupitia waandishi wa habari.
Simba ambao ni wenyeji wa mchezo wamefika saa 9:10 alasiri huku wakipaki gari yao sehemu iliyozoeleka na kupitia mlango sahihi wa kuingia vyumba vya kubadilishia nguo.
1 307
AONDOKE au ABAKIE ?
Toa maoni yako Hapa ✍️
Follow ukurasa wetu wa Instagram 👇
https://instagram.com/e_plus_media?igshid=MzNlNGNkZWQ4Mg==
1 307
"Kutokana na nilipopitia kwa sasa nipo vizuri kila siku naimarika namshukuru sana Mhe Rais @SuluhuSamia yeye amenipigia kwenda India nilitamanii kukutana naye kitendo alichokifanya alikifanya kama Mama. Kwahiyo nina sababu ya kushukuru na kumpa maua yake" @ProfessorJayTz
1 307
UZEMBE WETU UMETUPONZA NANI ALIYEMRUDISHA GOLINI MANULA ?
✍️ @exmayor_bonifacejacob
Napingana na wanasimba wenzangu wote wanaosema kufungwa goli tano ni Jambo la kawaida.
Hapana,Historia inaonyesha Simba au Yanga mara zote kufungwa goli nyingi kunakuwaga na sababu kubwa ya Usaliti au Migogoro ndani ya hizi timu.
Rejea ushindi wetu wa 5-0 kwa Yanga,walikuwa ktk Mgogoro mkubwa sana.
Simba kwa mara ya kwanza tumefungwa na mtani wetu bila ya uwepo wa Mgogoro wowote ndani ya timu.
Tumezidiwa mbinu,Uwezo na Ubora wa Mchezaji mmoja mmoja.
Tukiwa serious hiki kipigo tunaweza kukitumia kama darasa dhidi ya usajili wa makocha,Wachezaji na Uendeshaji wa timu wa kisasa.
Hakuna timu serious inaweza kumtoa Mchezaji kutoka majeruhi kuja uwanjani katika mechi kubwa tena bila sababu ya msingi ya kuacha wachezaji wenye ubora kwa wakati huo.
Simba imefungwa ikiwa watu wote muhimu ni sehemu ya uongozi wa timu.
Ukweli,Uwazi,uwajibikaji,weredi na upendo kwa timu ndiyo hitaji la simba kwa sasa.
Sikuwahi kujua mpira unamaumivu sawa na Msiba mzito.
1 307
The beauty of Kariakoo derby. Mnatambiana na kufanyiana kejeli za kimpira. Lakini mwisho wa siku aliyekanda na aliyekandwa wanabaki kuwa ndugu. Mkandaji anaweza kumpa lift mkandwaji na utani ukaendelea wakiwa njiani. Ukiona mtu anahubiri chuki kwenye mpira huyo ni zwazwa, mpuuze. Mpira sio uadui. - Malisa GJ
1 307
"Kwa sasa siwezi kusema nipo single au nipo kwenye mahusiano, lakini nikitaka kuolewa naolewa muda wowote na mwanaume yoyote hata sasa hivi nikiamua naolewa"- Zaiylissa
1 307
"Kiwango cha wananchi wanaopata maji safi na salama kimeongezeka hadi kufikia asilimia 88.6 mijini na asilimia 78 vijijini."
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji
Kitila Mkumbo
1 307
"Kiwango cha ukuaji wa uchumi kwa mwaka 2022 kilikuwa asilimia 4.7 na kinatarajiwa
kufikia asilimia 5.2 mwaka 2023 na asilimia 6.1 mwaka 2024. Aidha, mfumuko wa bei uliendelea kuwa tulivu ambapo ulikuwa asilimia 4.3 kwa mwaka 2022 na ulipungua na kufikia asilimia 3.3 katika kipindi kilichoishia Septemba 2023."
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji.
Kitila Mkumbo
#MpangowaMaendeleowaTaifa20242025
1 307
"Tathmini ya muda mrefu inaonesha kuwa uchumi wa Tanzania umekuwa ukikua kwa kiwango cha wastani cha 6% kwa mwaka katika kipindi cha miaka 20 iliyopita. Aidha, uchumi wa Tanzania ulionesha hali kubwa ya ustahimilivu hata katika kipindi cha misukosuko mikubwa ya kiuchumi duniani, ikiwemo wakati wa janga la ugonjwa wa UVIKO - 19 na vita vinavyoendelea kati ya Urusi na Ukraine."
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji
Kitila Mkumbo
#MpangoWaMaendeleo20242025
